Hii inapendeza sana kwa wapenzi

If he was somebody mbona alikuwa anaomba vibarua vya kazi alipokuwa chuo. Ukweli unauma. Ukisoma story jamaa walianza relationship wakiwa chuo. Na kabla ya kuanza kibarua jamaa kipatochake kilikuwa mkopo wa chuo kikuu
Mkuu mimi nshaona hapa kinachogombaniwa ni nini
nshaelewa.
Haha
 
Hakuna haja ya kutukana mpendwa tushindane kwa hoja ...sitaendelea kubishana nawe mana inaonekana una chuki binafs na wanaume na zaid unaona wanaume wote ni Miungu watu kama unavyosema which sio kweli, mwanaume mmoja aliekutenda usipake matope wanaume wote ....
nilichoona hapa ni kwamba wanawake they cant stand mwanamke mwingine akisifiwa, mtaingiza sababu zenu kua wanaume waongo sijui tunajifanya miungu watu had mnaprovoke na kutoa lugha mbaya kisa tu mwanamke fulan kasifiwa alivyo kwa mumewe....
hatuwalazimish muwe [HASHTAG]#michelle[/HASHTAG] ...kila mtu abebe msalaba wake na kila mtu achague wa kuish nae maishan hamlazimishwi wala ambae atakubaliana na matakwa yako well mtaendana nae mkaoane.
Kila mtu mwanamme kwa mwanamke ana mapungufu yake kwa namna yake
kusifiwa kwa michelle na jins aalivyoish na barack msifanye mkatokwa na povu itaendlea kuwepo kua they are best couple ever na ni mfano wa kuigwa... but hamlazimishwi kua kama wao,,
 
Matunda ya uvumilivu kwa wapenz ndo hayo ..!!
Hakuna mapenzi duniani yanayoweza kushamiri bila uvumilivu. Mtu asipokuwa na moyo wa uvumilivu katika mapenzi basi kila mtu utamuona hafai. Kila siku utakuwa mtu wa kuanzisha mahusiano mapya kitu ambacho si kizuri.
 
Walaaa sina chuki binafsi na wanaume kabisaaaa!! Mimi nikitendwa na mmoja ni yeye na walaa siwezi wachukulia wanaume wooote kuwa ni kama yete japo wapo wengine kama yeye!

Nilikuwa napingana na hoja iliyomezani ambayo inakandamiza tu wanawake as if hakuna mwanamke mwema tz hii,kwahiyo nawe ulivokuwa unaponda kuhusu wanawake ni kwakuwa una chuki binafsi na wanawake? Kwakuwa umtendwa na mwanamke mmoja basi waliobaki wote wameoza?

Ibakie kuwa wanawake wema wapo nawanaume wema wapo pia, na msiwasimange wanawak tuu as if nyie ni malaika.
 
Na nna conclude kwa kusema hivi, mahusiano ambayo hamna upendo wa dhati, hamna kuheshimiana, hamna kujaliaana, na hata mkipendana kuna mmoja wenu anampenda mwenzie kinafiki kwa sababu anacho, mahusiano ya kutanguliza pesa badala ya utu, mahusiano ambayo hamvumiliani, mahusiano ambayo hamna muda wa kuomba pamoja, mahusiano ambayo hamjui mlango wa kanisa ukoje ama mlango wa msikiti ukoje, mahusiano ya kuweka mbele pride and ego, mahusiano ya kutanguliza degree na masters, mahsiano ambayo mmoja akianguka mwingine anakimbia,mahusiano ambayo hamuombeani mapungufu yenu, mahusiano ambayo hamridhiki na mlichonacho, mahusiano ya kutoheshimiana na kudharauliana kisa mmoja hana kitu, hakika nawaambia hakuna kitakachoendelea kati yenu na hamtafika mbali. Unless uamue kubadilika.
Lakin vise versa na hayo niliyosema hapo juu basi mmoja wenu either mwanaume ama mwanamke anaweza kusimama na kusema bila kutetemeka kuonyesha shukran kwa mwenzie mbele ya watu na mkawa mfano wa kuigwa hata na watoto wenu watakapokua na familia zao.
 
Mbona hajatukana...?
 
Great! Itawasaidia wanandoa watarajiwa kwa kiasi flani kuzikabili chanagamoto za maisha ya ndoa.
 
Profesa uko sahihi.
 
Hahahahaha! Reciprocate the love to be safe.
 
Maisha ya kitamthilia yametawala siku hizi kwa wadada wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…