Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Ewe ujiitae UMEOKOKA NA HUNA dhambi.Hayo mamlaka ya kuita binadamu alieumbwa na Mungu 'MASHETANI' Umeyatoa wapi?? Hata hivyo najua nyie ni wasanii tu bali mnatumia jina la Mungu kutapeli watu.

.
Ushetwani ni mambo yote anayoweza kutenda binadamu yanayokinzana na uhalisia wa mambo kama vile uongo, fitna, ubasha, usenge,uzinzi,kijicho,dhulma nk. Mwenye post kawaita wazushi/waongo mashetani sawa na neno la Mungu linavyowaita. Wewe kwani upo kundi gani hadi uhamaki?
.
 
Askofu Kakobe aambiwe kuwa kikulacho kiko nguoni mwake... Aliyeandika haya hapa ni mshirika wake wa Karibu sana ... Na hataki Kakobe afanikiwe kwa lolote...
 
Nimebahatika kuiona nyumba ya mama lwakatare iliyopo pembezoni ya bahari ana hekalu la maana limezungukwa na nyumba ndogo ndogo kama tatu hiyo fensi ya ukuta wa nyumba yake unajenga nyumba tatu za heshima mbagala chezea mlima wa moto wewe .

Mi nataka Wachungaji na Maaskofu wote waishi maisha ya raha ... Kwa sababu kwa kuwa Watumishi wamekuwa tayari kutumia maisha yao na muda mwingi kwa ajili ya waumini... Sasa kama ni utajiri kila mtu si awe mchungaji...
 
Leo nimeanza kuwachukia watu wa karibu wa Kakobe... Hamtakii mema kabisa...
 
Huyo Mzee wa upako kaingiaje hapa au ilikuwa ndiyo gear yenu ya kumuingia?

Kweli kabisa Mkuu. Anayetaka kuzungumza hapa juu ya Mzee wa upako, Rwakatare, au Mtumishi mwingine wa Mungu, akaanzishe thread yake, asitutoe kwenye mada.
 
attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.
Kwa mujibu wa katiba ya FGBF Kakobe ndio kanisa na kwa lugha nyingine mali zote na pesa zote za Kanisa ni za Kakobe ila zipo covered kwa jina la kanisa.

Hata wale mshitaki kakobe kwa ubadhirifu mahakamani wamekwama, Jaji aliwauliza hivi inawezekana vipi mtu kuitwa mbadhirifu kwa pesa zake mwenyewe? sawa na leo umshitaki Mengi eti ni mbadhirifu wa pesa za ITV.

Mwenye kuelewa na aelewe.
 
Jidanganye tu aliekwambia FaizaFoxy mwanamke ni nani? huyo ni dume la mbegu..ni ID ya Nape hiyo!

Umepata majibu kutoka kwa FF mwenyewe? Anakwambia mjinga uliwao.

FF angekuwa ni Nape kucha kuchwa angekuwa anamponda Nyerere? Na mimi nakuongezea wajinga ndio waliwao
 
Mtumishi wa mungu achafuriki wala kuchafuliwa.. unajua LUSEKELO MZEE WA UPAKO anaaishi wapi na anaendesha gari gani?

Hapa naona mimi ni kuwekana sawa tu.

achafuriki? Hii lafudhi ni kulekule alikozaliwa kakobe,bila shaka ni mjomba
 
Kwa mujibu wa katiba ya FGBF Kakobe ndio kanisa na kwa lugha nyingine mali zote na pesa zote za Kanisa ni za Kakobe ila zipo covered kwa jina la kanisa.

Hata wale mshitaki kakobe kwa ubadhirifu mahakamani wamekwama, Jaji aliwauliza hivi inawezekana vipi mtu kuitwa mbadhirifu kwa pesa zake mwenyewe? sawa na leo umshitaki Mengi eti ni mbadhirifu wa pesa za ITV.

Mwenye kuelewa na aelewe.

Siyo kweli, huijui Katiba ya FGBF. Katiba ya FGBF siyo tu kuwa ina General Overseer (Askofu Mkuu), bali ina Board of Trustees, ina Executive Council, ina Secretary General, Zonal Overseers (Maaskofu wa Majimbo), Treasurer, n.k. No research, no right to speak!
 
Mimi naifahamu hiyo Toyota Sprinter nyeupe, ni kweli sijawahi kumuona na gari lingne kama mzee wa Upako anaekuombea ili ununue prado!!
 
attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.

Hii nyumba mbona kama hakuna anayeishi humo?!!!
 
siku kakobe akiwa hayopo kanisani nani anaendesha misa?
maana nasikia huwa wanaweka CD's za mahubiri,ni kweli haya?

"Maana nasikia......" Hapa ndipo penye tatizo! Unaona sasa kuishia tu kusikia, badala ya wewe mwenyewe kutafuta ukweli, kumekufanya uishie kudanganywa! Maaskofu na Wachungaji makumi kwa makumi wa FGBF wamekuwa wakihubiri, na siyo Kakobe tu. Waumini wanajua. Siyo tu Maaskofu na Wachungaji wa FGBF, wanaohubiri, bali pia Watumishi wa Mungu wengine wengi wa Makanisa ya Kipentekoste wamekuwa wakihudumu hapo, na video/mikanda yao ipo. Baadhi yao ni Askofu Sylvester Gamanywa, Askofu Mbepela, Mchungaji Getrude Rwakatare, Mchungaji Mzungu Four, Hayati Askofu Mkuu Moses Kulola, Hayati Mchungaji Callisti Masalu, Askofu Emmanuel Lazaro, Askofu Eric Mwambigija, Askofu Lazaro Mayala, Askofu Mkuu Arthur Kitonga (Kenya), Dr K.A. Paul (USA), Askofu James Commey (Denmark), Askofu Mkuu Peter Ndhlovu (Zambia), Askofu Mkuu Edmund Kivuye (Burundi), na wengi wengine.
 
Siyo kweli, huijui Katiba ya FGBF. Katiba ya FGBF siyo tu kuwa ina General Overseer (Askofu Mkuu), bali ina Board of Trustees, ina Executive Council, ina Secretary General, Zonal Overseers (Maaskofu wa Majimbo), Treasurer, n.k. No research, no right to speak!
I have research & I have right to speak too.
Am christian lakini kuhusu Kakobe nilichosema ndio ukweli wenyewe na kama si kweli basi Jaji aliyekuwa au anayesikiliza shauri la kakobe kuhusu ubadhirifu ndio muongo.

Bahati mbaya hapa natumia simu ningekushushia vitu ungeshaa mwenyewe incase kama ulikuwa huujui ukweli.

Sina sababu wala maslahi yoyote ya kumzushia mtumishi huyu na mimi ni mmoja ninayevutiwa na mahubiri yake lakini hainibani kusema ukweli.

Kakobe anatembelea gari aina ya Nissan Patrol ambayo inamilikuwa na kanisa, na mwisho wa siku kanisa ni kakobe.
 
Back
Top Bottom