Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

mate.jpg
 
Uache u zombie wewe,mwaka jana kwenye mkutano wa vyama vya upinzani pale jangwani,alikuja na V8 mpya nyeupe,akiwa na dereva wake na mabodyguard,waliohudhuria mkutano ule ni mashahid,sasa unataka uniambie gari ile ya kifahari anaipaki hapo kwenye hcho kibanda?
 
huyu mleta uzi huo anatuona sisi watoto au.....kakobe kakutuma uje umpigie promo
 

Vipi kuhusu Mwingira, Gwajima, Lusekelo na Rwakatare, nao wanaishi nyumba za design gani?

Swala la Kakobe kuishi nyumba ya kawaida na gari moja haisaidii kama ana mambo yake ya ziada,sema tu mambo labda hayajamwendea,ila bado siamini maana anaenda mikutano mpaka nchi za nje kama china,nadhani zamani alikuwa na kipindi kwenye tv station flani kwa sasa sina uhakika,hela za kuendesha hayo yote waumini walikuwa wanachangia?sijaelewa.
 
Uache u zombie wewe,mwaka jana kwenye mkutano wa vyama vya upinzani pale jangwani,alikuja na V8 mpya nyeupe,akiwa na dereva wake na mabodyguard,waliohudhuria mkutano ule ni mashahid,sasa unataka uniambie gari ile ya kifahari anaipaki hapo kwenye hcho kibanda?

anaishi wapi sasa tuambie wewe unayejua
 
siku kakobe akiwa hayopo kanisani nani anaendesha misa?
maana nasikia huwa wanaweka CD's za mahubiri,ni kweli haya?
 
tuambie kwanza dhaka na sadaka zinaenda wapi afu ndyo ulete prnpangada zako

Zaka na sadaka zimefanya kazi kubwa ya Mungu nchi nzima. Majengo ya Makanisa yamejengwa kila kona ya nchi, kila wilaya Tanzania bara, mpaka vijiji vya ndani ndani kabisa. Nenda katika tovuti ya Kanisa: www.fgbfchurch.org katika ukurasa wa matawi ya Kanisa, ili ujionee picha makumi kwa makumi za majengo ya Makanisa haya.
 
Ni kweli kabisa, hizo tu ndiyo mali zake binafsi Askofu Kakobe. Mimi nimekuwa muumini wa Kanisa la FGBF, kwa miaka 25 sasa, yaani tangu lilipoanzishwa 1989. Muda huu mrefu, umenipa kumfahamu kwa karibu sana, Mchungaji wangu huyu. Ninathibitisha kwamba haya ndiyo maisha halisi ya Askofu Kakobe, tofauti na uzushi mwingi wa mashetani. Mtumishi huyu wa Mungu, analiishi hasa Neno la Mungu analolihubiri; ndiyo maana waumini tunampenda, kumwamini na kumheshimu; na makelele yote ya mashetani, hayawezi kututenganisha naye. Ninapafahamu mpaka kijijini kwake Askofu Mkuu Kakobe, huko Kakonko, Kigoma. Kijijini kwake, nako, hana hata banda. Miaka yote hii, akienda kijijini, amekuwa akifikia kwenye nyumba ndogo ya wazazi wake, Frank Kakobe, na Debora Kakobe, waliofariki muda si mrefu uliopita.

Ewe ujiitae UMEOKOKA NA HUNA dhambi.Hayo mamlaka ya kuita binadamu alieumbwa na Mungu 'MASHETANI' Umeyatoa wapi?? Hata hivyo najua nyie ni wasanii tu bali mnatumia jina la Mungu kutapeli watu.
 
Mwenyezi Mungu amjalie maisha ya kumtumikia yeye aliyemleta duniani ili atumike kwake na Wanadamu
 
Uache u zombie wewe,mwaka jana kwenye mkutano wa vyama vya upinzani pale jangwani,alikuja na V8 mpya nyeupe,akiwa na dereva wake na mabodyguard,waliohudhuria mkutano ule ni mashahid,sasa unataka uniambie gari ile ya kifahari anaipaki hapo kwenye hcho kibanda?

Ameshaeleza hilo gari alipewa na washirika na anakaa hapo kwenye hiyo nyumba ambayo wewe unaita kibanda".......jiwekeeni hazina mbinguni ......"

 
Kama hayo unayosema na kuandika hapa ni kweli basi mimi binafsi natilia shaka huduma ya askofu Kakobe.
Mungu ni tajiri sana, kila kitu anacho, na mtumishi wake yeyote akiomba lolote atapata, leo Askofu kakobe amejenga nymba kabla ya kuwa mchungaji kisha askofu, na tangu apate ufunuo na kumtumikia Mungu wake amempa nini? na je anamtumikia huyu mungu mwenye nguvu mwenye kila kitu? je yeye amemuomba nini huyo mungu wake?
Labda pia unisaidie, kujua hili Je kuna sifa gani kwa mtumishi wa Mungu mwenyewe kuwaombea waumini wake na kupata mafanikio kutoka kwa huyo mungu ili hali yeye hana mafanikio? au ina maana yeye hana uwezo wa kuwaombea waumini/wafuasi wake wakapata mafanikio?

Pengine labda utuambie Askofu kakobe kuishi nyumba hiyo na wewe kuwa muumini wake wa miaka 25, inatufundisha nini?, au wewe umejifunza nini kutoka kwa askofu wako huyo? unaposema hana Hela wala nyumba (hivo hana mali zingine) zaidi ya hiyo nyumba unataka sisi tuelewe nini?, hapokei sadaka kanisani? au ana matumizi mabaya ya fedha za kanisa?, mtu wa anasa asiye penda maendeleo? hebu tuelezee kwa mapana

nakutakia ibada njema mlokole wa FGBF
SP
 
Back
Top Bottom