Ni kweli kabisa, hizo tu ndiyo mali zake binafsi Askofu Kakobe. Mimi nimekuwa muumini wa Kanisa la FGBF, kwa miaka 25 sasa, yaani tangu lilipoanzishwa 1989. Muda huu mrefu, umenipa kumfahamu kwa karibu sana, Mchungaji wangu huyu. Ninathibitisha kwamba haya ndiyo maisha halisi ya Askofu Kakobe, tofauti na uzushi mwingi wa mashetani. Mtumishi huyu wa Mungu, analiishi hasa Neno la Mungu analolihubiri; ndiyo maana waumini tunampenda, kumwamini na kumheshimu; na makelele yote ya mashetani, hayawezi kututenganisha naye. Ninapafahamu mpaka kijijini kwake Askofu Mkuu Kakobe, huko Kakonko, Kigoma. Kijijini kwake, nako, hana hata banda. Miaka yote hii, akienda kijijini, amekuwa akifikia kwenye nyumba ndogo ya wazazi wake, Frank Kakobe, na Debora Kakobe, waliofariki muda si mrefu uliopita.