Hii elimu bure ya Magufuli watoto wao wanasoma hizo shule za bure? Ndugu zao wanafundisha huko? Inatusaidia kimaendeleo? Inaendana na teknolojia?

Mimi sio mkazi na wala sjawahi kufika chato ila kuhusu hili la airport kujengwa chato nadhan pia tungewaza kwanini international airport ilijengwa songwe na siyo mbeya,nadhan watu hawahoji sana kuhusu uwanja wa songwe sabab kikwete aliujenga halafu akawa hatokei songwe,ndo maana kelele ni chache au hazipo kuhusiana na uwanja wa songwe,,,,,,,!kitu msichokijua hii ilikuwa ni mikakati ambayo rais yeyote angetekeleza,hata kama lowassa angepita angeujenga uwanja huu ila kelele zisinhekuwepo sabab yy anatokea monduli,mkizipata sabab za kujengwa uwanja wa songwe mtazipata sabab za chato airport,mnadandia sana visabab vya kijinga visivyo na mashiko
Uwanja wa songwe upo mbeya na siyo songwe kama mkoa. Fuatilia usikurupuke na ulianza kujengwa kabla ya mgawanyo wa hiyo mikoa
 
Mwisho wa yote mtihani wa mwisho hutoka serikakini kwa kuwapima watahiniwa wote bila kujali u private au public schools

KUNA HABARI NILIAMBIWA NA MTU MMOJA,

JE, NI KWELI KWAMBA MITIHANI YA TAIFA HUTOLEWA KWA MAKUNDI MAWILI YAANI KWA SHULE ZA SERIKALI NA SHULE BINAFSI ZA MICHEPUO YA KIINGEREZA?
 
Mimi sio mkazi na wala sjawahi kufika chato ila kuhusu hili la airport kujengwa chato nadhan pia tungewaza kwanini international airport ilijengwa songwe na siyo mbeya,nadhan watu hawahoji sana kuhusu uwanja wa songwe sabab kikwete aliujenga halafu akawa hatokei songwe,ndo maana kelele ni chache au hazipo kuhusiana na uwanja wa songwe,,,,,,,!kitu msichokijua hii ilikuwa ni mikakati ambayo rais yeyote angetekeleza,hata kama lowassa angepita angeujenga uwanja huu ila kelele zisinhekuwepo sabab yy anatokea monduli,mkizipata sabab za kujengwa uwanja wa songwe mtazipata sabab za chato airport,mnadandia sana visabab vya kijinga visivyo na mashiko
Mkuu, una uhakika uwanja ndege wa Songwe hauko Mbeya?
 
Umewahi kufika mbeya ?

Mbeya ni mji wa kibiashara acha kuifananisha na Chato.

Halafu ikumbukwe ule uwanja ulijengwa kabla ya Songwe kutenganishwa na mbeya. So before ule uwanja ilikuwa mkoa wa mbeya.
Kwani sasa uwanja wa Songwe hauko Mbeya?
 
Acha hizo wewe, nani katika cooperate companies anashikilia cheo cha maana katoka Kayumba. Kayumba wanauwezo wa kukariri tuu. Nipe mifano mitatu au tano hapa. Halafu mie nikupe mifano mia hapa hapa bongo. Shule za serikali zina matatizo na product zake haziwezi kupambana nje ya TZ
Viongozi karibu wote waserikalini wanaoongoza sasa wamesoma shule za serikali ambazo wewe unaziita Kayumba
 
Elimu ni maarifa yanayofundishwa toka kizazi kimoja hadi kingine katika kuhama na tabia, mwenendo, ujuzi, maarifa na sayansi ya kubadili mazingira yawe ya manufaa kwa umma.

Huwa najiuliza hii elimu inayosifiwa kuwa ni ya bure.

Kiuhalisia hii sio elimu bure kama wanavyosema maana kuondoa ada haimaanishi elimu ni bure bali bila malipo ya ada lakini mambo mengine kama daftari, kalamu, nauli nk mzazi bado anagharamikia ila ile elimu ya Nyerere ndio ilikuwa bure maana vyote vililipiwa na serikali. Tuliosoma enzi zile utakumbuka kuna daftari lilisomeka "haliuzwi"

Bado najiuliza hii elimu ya sasa ni watoto wangapi wa vigogo wanasoma hizo shule za elimu bure? Kuanzia rais na viongozi wote wa kisiasa tujue wanavyotunga sheria na mitaala kama ina tija hadi watoto wao wasome katika shule hizi za bure italeta sensi ya kuwa wametuletea vitu vya maana.

Pili hizi shule za bure kuna ndugu wa karibu mfano wake, waume, kaka, dada wa hao viongozi wanafundisha katika shule hizi?

Tatu. Hizi shule kwa elimu inayotolewa inaendana na kasi ya dunia ya teknolojia? Tunachofundisha kina shabihiana na dunia tuliyopo? Elimu yetu tukienda china, uingereza tunaweza kupapambana nao kwenye uvumbuzi na ajira?

Je vyuoni tuna vifaa vya kisasa vya kufundishia au bado tuko analogy na vifaa vya mwalimu nyerere ndio tinafundishia karne hii? Bado tuna xray wakati wenzetu wana ctscan, mri nk?

Shule zetu za technical zikoje je zinavifaa vya karne hii au bado tuna enzi ya mwalimu ambapo tunawataka wakitoka wajiajiri lakini wao wameajiriwa nawananchi?

Toa suluhisho, nini kifanyike.
 
Marekebisho Songwe International Airpot(SIA) Ipo mkoa wa mbeya. Mkoa wa songwe hauna uwanja wa ndege. Jina la uwanja ni songwe ila halipo mkoa wa songwe
 
Elimu ni maarifa yanayofundishwa toka kizazi kimoja hadi kingine katika kuhama na tabia, mwenendo, ujuzi, maarifa na sayansi ya kubadili mazingira yawe ya manufaa kwa umma.

Huwa najiuliza hii elimu inayosifiwa kuwa ni ya bure.

Kiuhalisia hii sio elimu bure kama wanavyosema maana kuondoa ada haimaanishi elimu ni bure bali bila malipo ya ada lakini mambo mengine kama daftari, kalamu, nauli nk mzazi bado anagharamikia ila ile elimu ya Nyerere ndio ilikuwa bure maana vyote vililipiwa na serikali. Tuliosoma enzi zile utakumbuka kuna daftari lilisomeka "haliuzwi"

Bado najiuliza hii elimu ya sasa ni watoto wangapi wa vigogo wanasoma hizo shule za elimu bure? Kuanzia rais na viongozi wote wa kisiasa tujue wanavyotunga sheria na mitaala kama ina tija hadi watoto wao wasome katika shule hizi za bure italeta sensi ya kuwa wametuletea vitu vya maana.

Pili hizi shule za bure kuna ndugu wa karibu mfano wake, waume, kaka, dada wa hao viongozi wanafundisha katika shule hizi?

Tatu. Hizi shule kwa elimu inayotolewa inaendana na kasi ya dunia ya teknolojia? Tunachofundisha kina shabihiana na dunia tuliyopo? Elimu yetu tukienda china, uingereza tunaweza kupapambana nao kwenye uvumbuzi na ajira?

Je vyuoni tuna vifaa vya kisasa vya kufundishia au bado tuko analogy na vifaa vya mwalimu nyerere ndio tinafundishia karne hii? Bado tuna xray wakati wenzetu wana ctscan, mri nk?

Shule zetu za technical zikoje je zinavifaa vya karne hii au bado tuna enzi ya mwalimu ambapo tunawataka wakitoka wajiajiri lakini wao wameajiriwa nawananchi?
Mtoa mada unakiri kwamba ulisoma Elimu bure yenye ubora na kugharamiwa kila kitu na serikali. Lakini hujatuambia, baada ya kunufaika kwa kupata Elimu hiyo bora kwa gharama za serikali, umelisaidiaje Taifa laki?, umeshiriki vipi kuboresha Elimu ili iendane na mahitaji ya sasa?. Gharama na jitihada za serikali ya Mwl. Nyerere kukusimesha unazirejesha kwa kuishutumu serikali?, Kwakweli Taifa limepata hasara kukusomesha usie na msaada kwa jamii wala Taifa
 
Makazini wapi? Hakuna elimu pale acha ujinga. Pale ni vituo vya kutengeneza wajinga.
Shule nyingi za kata kwa maana za bure wanafunzi wake wanafanya vizuri sana kwenye masomo na hasa kwenye maisha wako very critical makazini kuliko hao mnaowaita English Medium. Tunawaona huku makazini wengi wao wanajua kucopy na kupaste ukimuliza kwanini umefanya hivi hawezi kukupa sababu ya maana wanajua sana kugoogle. Lakini hawa wa kayumba wanafikiri sana kabla ya kufanya kitu ndiyo maana wakijua kitu wanakuwa wamekijua kwelikweli. Hayo ndiyo maoni yangu mkuu!
 
Ulimsaidia kuamua? Who are you? Yaani hujui hata kama kesho utakula lakini uko bise humu kusapoti ujinga
Mkuu umenena vizuri sana. Humu wanyama wa serengeti wapo wengi sana ndiyo maana hawafikiri critically. Wanafikiri Rais Magu pekee ndiyo aliamua uwanja wa Chato ujengwe pale wangekuwa wanatumia ubongo wao vizuri wangeushughulisha ubongo wao angalau hata kidogo katika kufikiri hasa katika maswala ya kiusalama wa nchi na raslimali za nchi katika maeneo tajwa!
 
Shule nyingi za kata kwa maana za bure wanafunzi wake wanafanya vizuri sana kwenye masomo na hasa kwenye maisha wako very critical makazini kuliko hao mnaowaita English Medium. Tunawaona huku makazini wengi wao wanajua kucopy na kupaste ukimuliza kwanini umefanya hivi hawezi kukupa sababu ya maana wanajua sana kugoogle. Lakini hawa wa kayumba wanafikiri sana kabla ya kufanya kitu ndiyo maana wakijua kitu wanakuwa wamekijua kwelikweli. Hayo ndiyo maoni yangu mkuu!
Ni kweli lkn sasa hao wa kata wanaofaulu ni wachache. Na sio wote wanaofikiria kiasi icho medium zitabaki kuwa juu usidanganye watu
 
Mbona huliizi kwanini watoto wa "Watunga Sera" hawa qualify kupata mikopo ya elimu ya juu? Hayo madaftari na vitabu ya bure mashuleni wakati wa enzi za Nyerere sijawahi ona. Madaftari na vitabu vya shule kila mzazi alitakiwa kununua Elimu Supplies.
 
Hoja yako ni ipi hapo,au umejawa majungu tu? Kwani hii elimu msingi bila malipo isingekuwa bure watoto wa Magufuli wangesomea huko?

Kwani wewe mtu akipika chakula hana haki ya kusema hajisikii kula na asile chakula hicho?

Wewe ukiona haikugusi jua hauhusiki na haikuhusu,wapo watu (tena wengi tu) walioguswa na ndiyo hao inawahusu,uamuzi ni wako kama mzazi na wa Magufuli kama mzazi pia wapi mwao/mtoto wa Magufuli atasomea

Mnakoelekea mtakuja kuhoji hadi aina ya sabuni anayoogea Magufuli (ni gwanji au medicated)

Ujinga mtupu
nin Maana ya uzalendo na kuhubiri uzakendo wee kiswasawadu?
 
Haja ni kuwa serikali ifanye juhudi kuhakikisha elimu inaboreshwa ili hata viongozi wavutiwe kupeleka watoto wao huko.
Hoja yako ni ipi hapo,au umejawa majungu tu? Kwani hii elimu msingi bila malipo isingekuwa bure watoto wa Magufuli wangesomea huko?

Kwani wewe mtu akipika chakula hana haki ya kusema hajisikii kula na asile chakula hicho?

Wewe ukiona haikugusi jua hauhusiki na haikuhusu,wapo watu (tena wengi tu) walioguswa na ndiyo hao inawahusu,uamuzi ni wako kama mzazi na wa Magufuli kama mzazi pia wapi mwao/mtoto wa Magufuli atasomea

Mnakoelekea mtakuja kuhoji hadi aina ya sabuni anayoogea Magufuli (ni gwanji au medicated)

Ujinga mtupu
 
"Wanajua mjinga akielevuka mwelevu yu mashakani" sasa dawa ni kumjaza nadharia tupu kwa hisani ya watu wa (...) ili taifa litawalike kirahisi na kunyonywa vilevile. Wahenga wanajua alichokifanya Mungai; kufuta, EK(elimu ya kujitegemea) pamoja na michezo. Nakuwajaza watoto ukale vichwani kwa kuwa nyima nafasi ya uvumbuzi. Kifupi mfumo wa utoaji elimu wa chaki na ubao, kalamu na daftari, umepitwa na wakati hauna tija kabisa kwa jamii, japo ni mtaji mkubwa wa kisiasa. Vituo vya kuleana oyeee- ole wake anayepinga maarifa ya ukale kwa watoto wetu. "It used to be in a pyramid shape but now, it is in a square shape: from kindergarten to university, ... who cares? "
 
elimu ya tanzania inamanufaa

kama inamanufaa
Kuhusu elimu bora ya awali, msingi na sekondari, nadhani tuanzie hapa:

Hakuna neno "inamanufaa" kwenye Kiswahili. "Ina" ni kitenzi, "manufaa" ni nomino. Huwezi kuchanganya maneno mawili tofauti, kitenzi, nomino, au aina nyingine yeyote ya neno, viwe neno moja kwa sababu tu unayasikia yanatamkwa kama vile ni neno moja.

Andika hivi: Elimu ya Tanzana ina manufaa, au elimu ya Tanzania haina manufaa.

Labda utusaidie kuwa shauri mafunzo (case study), wewe umesoma shule zipi, hizi "za kata" zisizo na malipo au "za academy," ama zile za kwetu za zamani ''za Nyerere"?
 
Back
Top Bottom