Dokezo: Kujenga jamii ya Kitanzania inayowajibika: Kubalansi utoaji wa huduma bure na Uwajibikaji

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,241
4,466
Pamoja na changamoto nyingi, Tanzania, imepiga hatua katika kutoa huduma za elimu na afya. Huduma hizi zimepitia vipindi na sera tofauti. Kwa sasa elimu ya msingi hadi shule za upili inatolewa bure, huku upande wa afya makundi maalum yakisamehewa katika uchangiaji. Tena hivi karibuni kuna baadhi ya wabunge walitaka elimu ya chuo kikuu pia iwe bure. Si jambo geni kwa nchi kuwa na sera inayofanana na utoaji wa elimu (na afya) bure hadi chuo kikuu, kwani kuna nchi nyingi zilizoendelea zinazotoa elimu hadi ya chuo kikuu inayofanana na sera kama hizi au pendekezwa. Nchi kama Denmark, Finland, Germany, Iceland, Norway, Poland, Sweden, n.k zina sera kama hizi, lakini nchi zote hizo zina vyanzo vizuri vya mapato kupitia ukusanyaji mzuri wa kodi. Na walipa kodi wananufaika kwa sera kama hizi.

Pamoja na sera za kuchangia elimu na afya kubadirika, usimamizi wake ambao unapaswa kwenda sambamba na ulipaji kodi haujawahi simamiwa vizuri, na bila kukusudia umekuza utamaduni wa utegemezi na kujiona unastahiki haki fulani fulani miongoni mwa Watanzania wengi. Wakati umefika kwa Tanzania kuweka usawa, kuhakikisha ustawi wa raia wake na kukuza jamii inayowajibika, inayojitegemea.

Hali ya Sasa

Elimu bila malipo kuanzia shule ya msingi hadi sekondari na huduma za afya bila gharama kwa kundi fulani la watu ni hatua muhimu katika kuhakikisha jamii ina usawa. Hata hivyo, kwa sera hizi, kuna mwelekeo unaojitokeza wa wananchi wengi sasa wanatarajia serikali itabeba gharama za huduma nyingi, hata zile wanazoweza kuzigharamia wenyewe. Hii inadhihirishwa na matukio kama vile wanandoa wanaopanga kuzaa bila kuzingatia athari za kifedha, na kutegemea serikali baadaye kwa usaidizi wa huduma za uzazi, na malezi ya mtoto. Hii si sawa, maana inatengeneza jamii isiyowajibika. Wagonjwa wako radhi kulipia huduma za matibabu hospitali binafsi, lakini wakienda hospitali za serikali, wanaomba msamaha wa matibabu.

Utegemezi Kupita Kiasi

Jamii ambayo mara kwa mara hutegemea kusaidiwa na serikali, hata katika maeneo ambayo inaweza kujitegemea, ina hatari ya kudumaa. Jamii ambayo imezoea kupewa bure mbegu za kupanda msimu wa mvua, uvumbuzi na uwajibikaji wa kibinafsi unaweza kupungua. Sera za utoaji huduma bure isipodhibitiwa inaweza kukwamisha maendeleo ya taifa, na hivyo kuzalisha kizazi ambacho hakijajiandaa vyema kukabiliana na changamoto kwa kujitegemea.

Kukuza Uwajibikaji na kujitegemea

Ili Tanzania iweze kustawi, ni muhimu kukuza utamaduni wa kuwajibika. Hii inaweza kupatikana kwa:

- Kuelimisha Wananchi: Kuzindua kampeni nchi nzima kuhusu umuhimu wa kujitegemea, kupanga na kujiandaa. Simulizi za watanzania waliofanikiwa kwa uwajibikaji binafsi ziwe mwanga wa simulizi.

- Kulipa ada kulingana na kipato au kuwa mkopo: Tunaweza kuwa na mfumo ambapo wananchi wanachangia huduma kulingana na mapato yao. Wale ambao kwa kweli hawawezi kumudu wanaweza kusaidiwa, huku wengine wakilipa kiasi kidogo, kuongeza hisia ya umiliki na uwajibikaji. Lakini pia wengine wanaweza lipiwa ada, halafu wakadaiwa. Uzoefu unaonesha hata baadhi ya makongamano yakiandaliwa bila washiriki kutoa ada ya ushiriki, ushiriki wao katika konganano huwa duni, lakini kukiwa na ada inayolipwa, ushiriki wao huwa mzuri.

- Ushiriki wa Jamii: Kuhimiza jamii kushiriki katika utawala wa ndani, ikihusisha kujua bajeti iliyopo katika vituo vya huduma za kijamii kama vituo vya afya, hospitali n.k na kisha kufanya maamuzi na ugawaji wa rasilimali zilizopo. Hii inakuza hisia ya ushirikishi na kuwajibika.

Kuwalinda Wasiojiweza

Wakati wa kukuza uwajibikaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba wahitaji wa kweli hawaachwi nyuma. Serikali inapaswa kutambua na kusaidia watu walio katika mazingira magumu, kuhakikisha wanapata huduma muhimu bila kutengwa. Huduma hizi zisilenge tu kuwapa pesa kila mwezi, bali kuwafundisha stadi kazi na wengine kuwapeleka shule za upili hadi vyuo vikuu.

Wajibu wa sekta binafsi

Sekta binafsi ina jukumu muhimu katika kupunguza utegemezi kwa serikali. Kwa ushirikiano kati ya sekta za umma na sekta binafsi, Tanzania inaweza kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ufanisi. Serikali isione sekta binafsi kama washindani. TRA na mamlaka nyingine husika wahakikishe sekta binafsi inaboreka kama viwanda vya kutosha vinafunguliwa. Sekta binafsi ikishamili utegemezi kwa serikali utapungua.

Hitimisho

Tanzania ipo katika hatua muhimu ya maendeleo. Inaweza kukuza utamaduni wa utegemezi usio na mwisho au kutengeneza taifa la uwajibikaji, na kujitegemea. Kwa kuweka uwiano kati ya kutoa huduma muhimu na kukuza uwajibikaji, Tanzania inaweza kuhakikisha kuna ukuaji endelevu na mustakabali mzuri kwa raia wake wote.
 
Sera za ujamaa ziliharibu hii nchi,wananchi kila siku wanaililia serikali na kodi hayalipi?
 
Back
Top Bottom