Kwani wewe umesoma shule?Elimu ni maarifa yanayofundishwa toka kizazi kimoja hadi kingine katika kuhama na tabia, mwenendo, ujuzi, maarifa na sayansi ya kubadli mazingira yawe ya manufaa kwa umma.
Huwa najiuliza hii elimu inayosifiwa kuwa ni ya bure.
Kiuhalisia hii sio elimu bure kama wanavyosema maana kuondoa ada haimaanishi elimu ni burebali bila malipo ya ada lakini mambo mengine kama daftari, kalamu, nauli nk mzazi bado anagharikia ila ile elimu ya Nyerere ndio ilikuwa bure maana vyote vililipiwa na serikali. Tuliosoma enzi zile utakumbuka kuna daftari lilisomeka "haliuzwi"
Bado najiuliza hii elimu ya sasa ni watoto wangapi wa vigogo wanasoma hizo shule za elimu bure? Kuanzia rais na viongozi wote wa kisiasa tujue wanavyotunga sheria na mitaala kama ina tija hadi watoto wao wasome katika shule hizi za bure italeta sensi ya kuwa wametuletea vitu vya maana.
Pili hizi shule za bure kuna ndugu wa karibu mfano wake, waume, kaka, dada wa hao viongozi wanafundisha katika shule hizi?
Tatu. Hizi shule kwa elimu inayotolewa inaendana na kasi ya dunia ya teknolojia? Tunachofundiaha kina shabihiana na dunia tuliyopo? Elimu yetu tukienda china, uingereza tunaweza kuapambana nao kwenye uvumbuzi na ajira?
Je vyuoni tuna vifaa vya kisasa vya kufundishia au bado tuko analogy na vifaa vya mwalimu nyerere ndio tinafundishia karne hii? Bado tuna xray wakati wenzetu wana ctscan, mri nk?
Shule zetu za technical zikoje je zinavifaa vya karne hii au bado tuna enzi ya mwalimu ambapo tunawataka wakitoka wajiajiri lakini wao wameajiriwa nawananchi?