Nataka idadi ya wadahiliwa wenye Diploma walioomba mkopo na waliopata mkopo.Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya
20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
I. Vipaumbele vya kitaifa vinavyoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa viungo
118
o Wadahiliwa wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali 87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine 9,867
Jumla 20,183
Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483 , kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717 , na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295 .
Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Kingine wanachosahau hawa kubwa kwamba zamani mtumishi wa umma alikuwa anakopea mshahara wake ili ampeleke mtoto wake shule za kulipia kwa sababu alikuwa anapata viallowance huko kazini,sasa hv havipo na mshahara ndo huo una makato,kwa hiyo naye sasa hv maskini tu!watoto wote wapewe mikopo ili wapate elimu,baadae watakuja kulipa wenyewe.wasitegemee km kuna mzazi atamudu kulipia,vyuo vitakuwa vitupu mwaka huu!Watu wanadhan gharama za chuo ni sawa na za secondary!!! Kule ni pagumu especially ktk accommodation, kwa hiyo kuyamudu hayo na wakati mwingine mzazi hata km mtumishi anao watoto wengine wanasoma na kimshahara chake chenye makato kibao, after all hiyo ni mikopo watailipa so wapewe tu
Nyahanga Mkuu.....[/QUOTE]kijiji gani? Lamadi, Nyamikoma, Kabita, Nyakabhoja, Nyashimo, Nassa Ginery, Mwamanyili, Masanza, BUsami, badugu, Shigala..... etc?
Hela? Numhonagi mahela a'walwa! Hela ja nokho nkoyi!Yah...ndio nyumbani najivunia kuwa Msukuma niliyesoma.....na ambaye Nina hela.
Mkuu mbona kwa mzee Madete walikuwaga wanatokeapo wenye akili nzuri sasa wewe umekuwaje tena hivyo?Madete moja....
Acha porojo, zile zama zimepita! Kama hauna sofa za kupata mkopo raindi hiii sahau.Huenda unafurahia kwa sababu umepata au nduguyo kapata lakini tambua kuwa kuna asilimia kubwa sana ya watoto wa Maskini hawajapata mkopo.
Nikueleze tu ukweli,wanaotokea Diploma wengi hata watoto wa Kimaskini hawajapata mkopo.
Usijiaminishe sana kwa unachokisema.
Hv hamuelewi ama kujitia hamnazo..!!??Tunapokusanya sana mapato tunapodhibiti sana matumizi unapopunguza sana wafanyakazi hewa bila shaka tunaokoa pesa nyingi sana swali mbona huduma zinazorota kila siku badala ya kuboreka kwa mapato yanayoingia matokeo, dawa hospital hakuna tumepunguza idadi ya wanapewa mikopo, biashara zinazorota kila siku why?
Nyahanga Mkuu.....[/QUOTE]kijiji gani? Lamadi, Nyamikoma, Kabita, Nyakabhoja, Nyashimo, Nassa Ginery, Mwamanyili, Masanza, BUsami, badugu, Shigala..... etc?
Labda kwa kuwa mi ni kitukuu
Mkuu mbona kwa mzee Madete walikuwaga wanatokeapo wenye akili nzuri sasa wewe umekuwaje tena hivyo?
Shigala moja hiyo mkuu!wewe kwenu wapi? au Susuma moja??
Safi sana mkuu, maelezo yamejitosheleza.Sema utaratibu tu ni wahovyo kila mwanafunzi haijalishi hali ya wazazi wake kiuchumi ana stahili mkopo google uone mfumo wa utoaji mikopo kwenye nchi kma za norway,sweden,deenmark,finland na nyinginezo
Unaposema wafanyakazi hawasitahili mikopo sijui una maana gani kwani uliambiwa mshahara wa mfanyakazi ni wakulipa ada,hv hujui sheria za kazi zinasema ni lazima mwajiri amuendeleze mwajiriwa tena ,usione watu wanatoa fedha zao kujosomesha ukadhani ndivyo inavyotakiwa
mchawi haswaaMtoa mada atakuwa mchawi