HESLB Mikopo kuunganishwa na NIDA, TIN, Passport na kadi za benki

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,410
Abdul Razaq Badru Mkurugenzi wa Bodi amefafanua kwamba mnufaika ataanza kulipa baada ya miezi 24 [miaka 2 ] kama hana ajira.
Baada ya hapo Deni linakuwa kwa 10% kila mwaka.

Watu ambao hawajaajiriwa kwenye sekta rasmi wanapaswa kurejesha 100,000/= au ASILIMIA KUMI 10% ya pato analolipia kodi kwa mwezi.

Kwa sasa BODI ina wanufaika 14,021 wanaorejesha mikopo yao.

Baada ya marekebisho ya Bodi ya mwaka 2016, ni wazi sasa Bodi itaunganisha mishahara, TIN, Passport na kadi za benki ili wanufaika wote wapate kurejesha kwa wakati.
[Binafsi nashauri Bodi iyatake makanisa yote, watu wanaofunga ndoa pia waangaliwe kama wameanza kulipa deni, mtu anafunga ndoa kwa gharama ya sherehe milioni 50 ila halipi 100 ya Bodi, hii ni dharau kwa Magufuli]

TLS na JUDICIARY wameshauriwa kuwabana mawakili binafsi ambao wengi ni wanufaika na hawalipi kabisa. Mawakili wakati wa ku-renew PRACTICING CERTIFICATES watapaswa kuambatanisha uthibitisho kwamba wameanza kulipa deni.

Law firms nyingi Dar es salaam zina hela sana lakini hawalipi.
Kwa wale wote ambao ni professions , vyama vyao vihakikishe haviwapi leseni mpaka wawe wameanza kulipa deni la BODI, mfano TLS, WAKANDARASI, MADAKTARI, WAHASIBU CPA, MAREFARII, BOXING, TFF
BODI YA WALIMU inaanzishwa rasmi kisheria ambapo ili mwalimu aweze ku-practice/kufundisha lazma awe mwanachama an alipe ada ya Bodi hiyo kila mwaka.

WALIOSOMA NJE YA NCHI/ ULAYA
Assume ana mika 30 kwa sasa. Jumlisha 35 ya kulipa deni atakua na miaka 65. Umri wa kustaafu ni miaka 60. Maana yake atastaafu bila kumaliza kulipa deni. Ikitokea hivyo Bodi itaenda kukomba kiinua mgongo chake kumalizia deni (kama sheria inavyosema). Sasa jiulize je huku ni kumsaidia mtanzania au kumkomoa?

Kunapaswa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu mikopo ya elimu ya juu. Wazazi wanaoweza kusomesha watoto wao kwa kuwalipia ni vizuri wafanye hivyo, badala ya kuwaingiza kwenye mikopo hii inayoumiza. Pili, wazazi wasio na uwezo serikali iwape watoto wao ruzuku (bursary) si mikopo (loan).

Awamu ya kwanza na ya pili serikali iliwapa ruzuku wanafunzi wote wa elimu ya juu. Awamu zilizofuata zikaondoa ruzuku na kuleta mikopo. Nyerere na Mwinyi waliweza nini ambacho kimewashinda waliofuata?

Wakati wa Nyerere na Mwinyi wanafunzi wa vyuo vikuu walikula bure, kusoma bure, na kulala bure. Na bado walipewa pesa ya kujikimu. Kuna kipindi nchi ilipita kwenye hali ngumu kiuchumi Nyerere akapunguza bajeti ya mayai kwenye breakfast ya wanafunzi wa UDSM. Wakafanya mgomo. Akawaita Ikulu na kuwatia bakora.

Wakati ule mwanafunzi hana pressure ya ada, kula wala kulala. Anapewa pesa ya stationeries, field na research. Asubuhi anapewa breakfast yenye mapochopocho kibao (maziwa, mkate, mandazi, pancacke, chees, jam, mayai, juice, sambusa, sosage etc). Halafu wanapunguziwa mayai wanaamua kugoma. Nyerere akawatia bakora. Akawaambia msijifanye nyie ni muhimu kuliko watanzania wengine.

Sasa wale waliosomeshwa kwa ruzuku na kupata fursa zote hizo, ndio wameleta kitanzi kinaitwa mikopo ya elimu ya juu. Kitanzi hiki kimewatesa sana watoto wengi wa maskini. Hivi Nyerere nae angeweka mikopo hawa viongozi wa leo wangesoma? Nashauri MIKOPO ifutwe wanafunzi wapewe RUZUKU kama zamani. Rasilimali tulizonazo kama taifa zinatosha.
 
Abdul Razaq Mkurugenzi wa Bodi amefafanua kwamba mnufaika ataanza kulipa baada ya miezi 24 [miaka 2 ] kama hana ajira.
Baada ya hapo Deni linakuwa kwa 10% kila mwaka.

Watu ambao hawajaajiriwa kwenye sekta rasmi wanapaswa kurejesha 100,000/= au ASILIMIA KUMI 10% ya pato analolipia kodi kwa mwezi.

Kwa sasa BODI ina wanufaika 14,021 wanaorejesha mikopo yao.
Baada ya marekebisho ya Bodi ya mwaka 2016 , ni wazi sasa Bodi itaunganisha mishahara, TIN, Passport na kadi za benki ili wanufaika wote wapate kurejesha kwa wakati.

TLS na JUDICIARY wameshauriwa kuwabana mawakili binafsi ambao wengi ni wanufaika na hawalipi kabiusa.
Mawakili wakati wa ku-renew PRACTICING CERTIFICATES watapaswa kuambatanisha udhibitisho kwamba wameanza kulipa deni.

Law firms nyingi DAr es salaam zina hela sana lakini hawalipi.
yani ningejuaga kuna hiki kisanga haki ya mungu nisingechukuaga hii hela
 
yani ningejuaga kuna hiki kisanga haki ya mungu nisingechukuaga hii hela
Mkuu hujachelewa, kam UN waTOTO AMA mdogo wako , n a una uwezo wa kumsomesha fanya hivyo, achana na fedha za mateso.

Watu wengi wanaweza kusomeshwa na wazazi ila wanataka hela ya bodi wakifikiri ni ruzuku ya bure tu.

Mtu kasome FEZA BOYS ada ni Milioni 8 kwa mwaka ila akija CHUO anataka mkopo wa milioni moja na nusu.
 
Abdul Razaq Mkurugenzi wa Bodi amefafanua kwamba mnufaika ataanza kulipa baada ya miezi 24 [miaka 2 ] kama hana ajira.
Baada ya hapo Deni linakuwa kwa 10% kila mwaka.

Watu ambao hawajaajiriwa kwenye sekta rasmi wanapaswa kurejesha 100,000/= au ASILIMIA KUMI 10% ya pato analolipia kodi kwa mwezi.

Kwa sasa BODI ina wanufaika 14,021 wanaorejesha mikopo yao.
Baada ya marekebisho ya Bodi ya mwaka 2016 , ni wazi sasa Bodi itaunganisha mishahara, TIN, Passport na kadi za benki ili wanufaika wote wapate kurejesha kwa wakati.

TLS na JUDICIARY wameshauriwa kuwabana mawakili binafsi ambao wengi ni wanufaika na hawalipi kabiusa. Mawakili wakati wa ku-renew PRACTICING CERTIFICATES watapaswa kuambatanisha udhibitisho kwamba wameanza kulipa deni.

Law firms nyingi Dar es salaam zina hela sana lakini hawalipi.

Hii ishu nlijua tu lazma wailete. yan tangu nafatilia ktambulisho ch nida nlikua nahisi kabisa hii ishu itakuja laziiima
na hatmae imetimia.
 
Back
Top Bottom