HESLB: Batch One Out Now

HESLB: Batch One Out Now

Hivi kwenye kuappload image nn kinahitajika maana picha niliyoappload wakat wa kuomba mkopo sasa hivi inagoma.
 
robbinhood mkuu nisave apa kwenye kusign boom maana hizo otp au code zinakuja after 5 mins ambapo ndiyo muda zinaexpire sasa imefika mara ya pili ikagoma kabisa na mfumo unaandika error occured try again later 🙏🙏
 
Rufaa sasa kufungwa Ijumaa Novemba 17, 2023

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuongeza muda wa siku nne zaidi hadi Novemba 17, 2023 ili kuwawezesha wanafunzi ambao hawajapangiwa au wanaohitaji kuongezewa viwango vya mikopo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kuwasilisha maombi ya rufaa zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema uamuzi wa kuongeza muda umetokana na tathtmini iliyofanywa ili kuwawezesha wanafunzi wahitaji watumie muda wa nyongeza kuwasilisha maombi ya rufaa zao kwa usahihi.

“Tulifungua dirisha siku ya Jumatano (Novemba 8, 2023), na baada ya tathmini tumeongeza muda wa siku nne zaidi hadi Ijumaa, Novemba 17 mwaka huu ili kutoa muda wa kutosha kwa waombaji kuwasilisha rufaa zao”, amesema Badru na kusisitiza maombi yote ya rufaa yanawasilishwa kwa njia ya mtandao (OLAMS).

Mkurugenzi Badru amewashauri waombaji wa mikopo wanaokata rufaa kusoma maelekezo kwa umakini na kuyazingatia ikiwemo kuambatisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao ambazo awali hawakuwa wamezipakia kwenye mfumo na kuongeza kuwa waombaji wanapaswa kutembelea akaunti zao walizotumia kuomba mikopo (SIPA) ili kupata taarifa za mikopo yao.

Serikali kupitia HESLB imepanga kutoa mikopo kwa wanafunzi 220,000 kwa mwaka
 
Nimeona boom inatoka kwa awamu sijui waliojisajili mapema ndiyo wanaowahi kuingiziwa boom.

Sasa sijui kwa waliojisajili awamu ya mwisho wataingiziwa boom lini.
Samahani, hivi account ya DiDis ni ipi, na unaingiaje?
 
Rufaa sasa kufungwa Ijumaa Novemba 17, 2023

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza kuongeza muda wa siku nne zaidi hadi Novemba 17, 2023 ili kuwawezesha wanafunzi ambao hawajapangiwa au wanaohitaji kuongezewa viwango vya mikopo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kuwasilisha maombi ya rufaa zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema uamuzi wa kuongeza muda umetokana na tathtmini iliyofanywa ili kuwawezesha wanafunzi wahitaji watumie muda wa nyongeza kuwasilisha maombi ya rufaa zao kwa usahihi.

“Tulifungua dirisha siku ya Jumatano (Novemba 8, 2023), na baada ya tathmini tumeongeza muda wa siku nne zaidi hadi Ijumaa, Novemba 17 mwaka huu ili kutoa muda wa kutosha kwa waombaji kuwasilisha rufaa zao”, amesema Badru na kusisitiza maombi yote ya rufaa yanawasilishwa kwa njia ya mtandao (OLAMS).

Mkurugenzi Badru amewashauri waombaji wa mikopo wanaokata rufaa kusoma maelekezo kwa umakini na kuyazingatia ikiwemo kuambatisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao ambazo awali hawakuwa wamezipakia kwenye mfumo na kuongeza kuwa waombaji wanapaswa kutembelea akaunti zao walizotumia kuomba mikopo (SIPA) ili kupata taarifa za mikopo yao.

Serikali kupitia HESLB imepanga kutoa mikopo kwa wanafunzi 220,000 kwa mwaka
Hii taarifa hii
 
Kitufe cha kuappeal kwangu hakionekani na kile kilichopo kwenye sehem ya application hakirespond,nn shida?
 
Back
Top Bottom