MKANDAHARI
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 5,756
- 6,684
Mambo ni mengi muda ni mchache! nikikumbuka zile milioni 50 nachoka kabisa!
Imekuwa vice versa…kutoka million 50 kwa kila kijiji hadi elfu 20,000 kwa kila mnyonge…
Namba hazidanganyi mkuu, wanapenda namba lakini hawajuui hesabu.Hii serikali ya wanyonge na viwanda ilipoingia madarakani mwaka 2015 iliingia na matamko mengi ya yasiyo na kikomo, ni serikali iliyotoa matumaini makubwa sana kwa watanzania kwa matamko, kila kukicha ni matamko, matamko matamko juu ya matamko. Miaka mitano ndio hiyo inaisha hesabu zinagoma. Kwa mwaka 2015, mwaka 2020 ilionekana mbali sana, matamko juu ya 2020 yalikua mengi mno, utasikia 2020 tutakua na umeme MW 5000, nchi itakua na uchumi wa kati, SGR itakua imefika Mwanza na mambo kede aa kede, hadi sasa hesabu zinagoma.
Serikali ya wanyonge ilipoingia madarakani ilianza na biti kali ya kutangaza bajeti kubwa ambalo IMF ilitoa tahadhari kua haiko realistic, wao serikali ya wanyonge wakasema pesa ipo, hili li nchi ni litajiri, tutakua donor country. Mwisho wa siku hesabu zinakataa, bajeti Trilioni 32, makusanyo trilioni 25, mishahara, madeni na matumizi mengine trilioni 22, maendeleo trilioni 3.
Jana namsikia waziri wa fedha anasema hadi march hii 2019, bajeti ya maendeleo ya mwaka huu wa fedha ilikua trillioni 12, hadi sasa zimepatikana trillioni 2 tu, bado miezi 3 mwaka uishe. Maana yake hadi sasa utekelezaji ni 17%, maana yake ni kua miradi mikubwa yote utekelezwaji wake unaweza kushindikana au ukachukua muda mrefu sana kinyume na matarajio ya serikali ya wanyonge ambayo hutaja unrealistic bajeti kufurahisha watu wajinga na kutoa matamko yasiyo na kichwa wala miguu.
Miaka 5 ya serikali ya wanyonge inafika mwisho, hakuna kitu tangible cha maana kilichofanyika, tuliahidiwa 2020 tutakua na megawati 5000, hata 2000 hatujafika, tuliambiwa 2020 tutakua na uchumi wa kati, hadi sasa haijulikani tuko uchumi gani, tuliahidiwa viwanda baadae tukaambiwa hata cherehani ni viwanda, tuliahidiwa SGR hadi Mwanza, hata ya Moro tu haijafika 50%, serikali ya wanyonge itahamia Dodoma kuwafuata wanyonge, serikali yote bado iko Dar.
Serikali hii ya wanyonge with inexperienced leaders walidhani kila kitu kitafanyika kwa matamko, sasa hesabu zinakataa, tuliambiwa mabeberu wanatunyonya,huku kinyume nyume lobbyist wa serikali wanawapigia magoti mabeberu wapewe misaada na mikopo.
Lets wait and see.
wanyonge tumeongezeka mkuu...na ndio maendeleo yenyewe hayo........maana kiwanda kinazalisha makontena mapya ya wanyonge kila kesho.....tunatimiza azma ya kuishi kama mashetwaini!Tangia wameingia madarakani wanyonge wako wangapi na wamepunguza wamebaki wangapi?
Hivi walimaanisha Geneva ya Uswisi au Jeneva ?Umesahau alitupiga kamba pale mwanza itakua kama Geneva.
Vip mrejesho
Waliruka ruka na kupiga mayowe ya furaha ..!
Donner countries si ndio "Mabeberu" ??Donner countries wamegoma kutupa misaada, out of 2 trillion, wametuba billion 144.
Jamaa kachachawa, nasikia kaenda Zonghwa Garden kuomba msaada
Ni mabuzi tunayachuna.Donner countries si ndio "Mabeberu" ??
Subiri kwanza ahamie Dodoma kabla ya December mwaka jana
HahahahaNi mabuzi tunayachuna.
Nchi inadanga
Mabadiliko sio sherehe ya harusi kwamba tutaimba na kucheka. Mabadiliko yana uchungu wake mwanzoni.
Hata kulima, kupalilia na kutunza shamba ni mbinde, kunachosha na kunakatisha tamaa. Ila wakati wa mavuno maumivu yote yanasahaulika.
Miradi mikubwa tunayoibeza siyo hewa, ipo dhahiri na inaonekana kwa macho. Ni uwezekaji mkubwa ambao manufaa yake ni very promising in the future. Sio chumvi uweke kwenye mboga itakolea hapo hapo.
Nidhamu Serikalini ipo juu. Leo hii hakuna ubabe wa kipuuzi na kutambiana mitaani kisa unaendesha STK kama zamani.
Halafu hizo political statements zinazotajwa zipo tu ili kuwajaza ari wananchi. We all need that to be able to move as a country. Sasa Serikali isiyohamasisha itasongaje?
Kwa ufupi, kuna sehemu tulikwama. Acha tubadili hali na kuchukua uelekeo mpya kama taifa. Wengine mtakuja kuelewa baadae sio lazima muelewe sasa.
Hesabu hazijagoma!
Sent using Jamii Forums mobile app