Hesabu zinavyoigomea Serikali ya wanyonge na viwanda

Hesabu zinavyoigomea Serikali ya wanyonge na viwanda

UMESHA SEMA AHADI ,SASA UNALALAMIKA NINI..KWANI WEWE MALENGO YOTE ULIYOJIWEKEA MWAKA JANA UMEYATIMIZA YOTE KWA UKAMILIFU.
 
Tatizo kubwa hasa upande wa miradi kushindwa kukamilika ni kutaka kutekeleza miradi yote kwa pamoja kitu ambacho hakiwezekani hasa ukiangalia mapato yetu huwezi kujenga SGR, huwezi kununua ndege, huwezi kujenga Stigler's, huwezi kujenga viwanda na hili la baadaye la korosho uyafanye yote kwa pamoja haiwezekani ufanisi wake lazima uwe chini ya asilimia 20 tena kwa gharama kubwa hili wala halihitaji uwe na degree ya uchumi maana siku zote resource ni scarce ili uweze kufanya X lazima Y ipungue kidogo hizi ni principles za uchumi

Kitu ambacho kingefanyika ingechaguliwa angalau miradi miwili ambayo hiyo fedha zote kwa miaka hii mi5 ingeelekezwa huko na kwa kuwa sera ilikuwa ni viwanda then Stigler's ungeanza ili kuhakikisha uwepo wa umeme Kwa viwanda hivyo wakimaliza wangeingia SGR ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa au viceversa hii ingesaidia kwa kiasi kikubwa ukamilikaji wa angalau asilimia 70 ya hiyo miradi kama siyo 100 mpk sasa
 
Huyu jamaa akili yake sijui huwa unawaza nini !? Aliweza vipi kuzidisha bajeti hivyo ghafla wakati nchi ikiwa haijaongeza vyanzo mbali mbali vikubwa vya mapato !!!?

Sent using Jamii Forums mobile app

Alikuwa kapigia mahesabu hela za makinikia na bomba la mafuta la Uganda. Hajajua Museveni ni bonge mtapeli.
 
Siasa bana duh! Kila nikikumbuka ahadi za wanasiasa sidhani kama nitafanya tena ujinga wa kwenda kushinda kwenye vituo vya kupiga kura, labda niambiwe kupiga kura kunaongeza nguvu ya kiume[emoji849][emoji849][emoji849][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabadiliko sio sherehe ya harusi kwamba tutaimba na kucheka. Mabadiliko yana uchungu wake mwanzoni.

Hata kulima, kupalilia na kutunza shamba ni mbinde, kunachosha na kunakatisha tamaa. Ila wakati wa mavuno maumivu yote yanasahaulika.

Miradi mikubwa tunayoibeza siyo hewa, ipo dhahiri na inaonekana kwa macho. Ni uwezekaji mkubwa ambao manufaa yake ni very promising in the future. Sio chumvi uweke kwenye mboga itakolea hapo hapo.

Nidhamu Serikalini ipo juu. Leo hii hakuna ubabe wa kipuuzi na kutambiana mitaani kisa unaendesha STK kama zamani.

Halafu hizo political statements zinazotajwa zipo tu ili kuwajaza ari wananchi. We all need that to be able to move as a country. Sasa Serikali isiyohamasisha itasongaje?

Kwa ufupi, kuna sehemu tulikwama. Acha tubadili hali na kuchukua uelekeo mpya kama taifa. Wengine mtakuja kuelewa baadae sio lazima muelewe sasa.

Hesabu hazijagoma!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni hivi, Magu hiyo miradi alijua 2020 itakuwa imekamilika na ukweli unakataana na matamanio yake. Aliamini nchi ni tajiri sana ndio maana akaanza kiburi cha madaraka. Ukiangalia mradi wa stiegler gorge na SGR zinahitaji 10t+, sidhani kama hiyo reli itavuka Morogoro na mradi wa stiegler gorge utaenda kwa kusuasua sana kwani nchi yetu inaingiza fedha kiduchu za kigeni, na wazungu wamebinya hela zao kutokana na mwenendo wa kutoheshimu demokrasia hapa nchini. Mikopo nayo inazidi kusuasua. Kwa ujumla Magufuli ni kama kocha mkali mwenye mbinu hafifu.
 
Mimi binafsi nimeishi mikoa mitatu tofauti kwenye hii miaka minne ya huh utawala Na kote huko no Kama naishi kwani Mara kwa Mara nipo maeneo hayo hayo.
Kiukweli hospitalin kumeboresha vizuri.
Tarura wametuwekeea Barabara vizuri Na mifereji imesafishwa mvua ikinyesha MAJI hayaharibu barabara.jiulize Wewe ulipo unakosa nini kwenye maisha yako.

Nakosa ajira.
 
UMESHA SEMA AHADI ,SASA UNALALAMIKA NINI..KWANI WEWE MALENGO YOTE ULIYOJIWEKEA MWAKA JANA UMEYATIMIZA YOTE KWA UKAMILIFU.

Kwani umemuona akijigamba? Umesikia kainyima familia yake uhuru kisa aliwaahidi kuwatendea mambo makubwa?
 
Bado muda tunatekeleza kiki kwa kutumia mikopo, 2025 tukisepa mtalipa madeni mpk mfe ccm hoyee mble kwa mbele mafara mpo shangilieni basi.
Walipaji wapo akina chadema kodi mtatozwa kodi ya kuuzunguka mlima kwa sababu kila siku mnaona utalii mlima kilimanjaro si wa kuuangalia bure mlipie kwa utalii huo. Ccm hoyee. Kodi ya kichwa itarudishwa milioni kila kichwa. Maana miradi kiki hii haiwezi kuzalisha na kulipa deni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la nyongeza ya mishahara na ajira litampa shida sana mwakani. Sihitaji kusikia bombadieree wala Sgr wereva
 
Ni hivi, Magu hiyo miradi alijua 2020 itakuwa imekamilika na ukweli unakataana na matamanio yake. Aliamini nchi ni tajiri sana ndio maana akaanza kiburi cha madaraka. Ukiangalia mradi wa stiegler gorge na SGR zinahitaji 10t+, sidhani kama hiyo reli itavuka Morogoro na mradi wa stiegler gorge utaenda kwa kusuasua sana kwani nchi yetu inaingiza fedha kiduchu za kigeni, na wazungu wamebinya hela zao kutokana na mwenendo wa kutoheshimu demokrasia hapa nchini. Mikopo nayo inazidi kusuasua. Kwa ujumla Magufuli ni kama kocha mkali mwenye mbinu hafifu.

Wamewakimbilia mabeberu wa kichina hawa heri ya Mzungu ni muelewa na ana utu.Wachina watachukua kila kitu.Yap ndo majibu ya kusomesha watu no kuuwa secta binafsi ni sawa na kuukata mti ukupao pesa.Madhara ya kutokuwa na ABC za uchumi sawa na kumpa Fundi Bati ajifunzie nyumba yako kupiga Bati.Kanuni ya uchumi usema hivi,ukisomesha watu no wakishamaliza kuisoma nawe ni lzm uisome upande usipende.Hivo wawe wapole tu no zimegeuka zamu yao sasa sie tumaliza kuisoma
 
Siasa bana duh! Kila nikikumbuka ahadi za wanasiasa sidhani kama nitafanya tena ujinga wa kwenda kushinda kwenye vituo vya kupiga kura, labda niambiwe kupiga kura kunaongeza nguvu ya kiume[emoji849][emoji849][emoji849][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]

Sent using Jamii Forums mobile app

We kaa nyumbani cheza Na watoto Linda nyumba sie mapema tutakwenda kumaliza mchezo SAA 4 mapema Asubui,kuyaondoa majizi,mazulumati, wasiojulikana na mafisadi ya kodi zetu
 
Tatizo kubwa hasa upande wa miradi kushindwa kukamilika ni kutaka kutekeleza miradi yote kwa pamoja kitu ambacho hakiwezekani hasa ukiangalia mapato yetu huwezi kujenga SGR, huwezi kununua ndege, huwezi kujenga Stigler's, huwezi kujenga viwanda na hili la baadaye la korosho uyafanye yote kwa pamoja haiwezekani ufanisi wake lazima uwe chini ya asilimia 20 tena kwa gharama kubwa hili wala halihitaji uwe na degree ya uchumi maana siku zote resource ni scarce ili uweze kufanya X lazima Y ipungue kidogo hizi ni principles za uchumi

Kitu ambacho kingefanyika ingechaguliwa angalau miradi miwili ambayo hiyo fedha zote kwa miaka hii mi5 ingeelekezwa huko na kwa kuwa sera ilikuwa ni viwanda then Stigler's ungeanza ili kuhakikisha uwepo wa umeme Kwa viwanda hivyo wakimaliza wangeingia SGR ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa au viceversa hii ingesaidia kwa kiasi kikubwa ukamilikaji wa angalau asilimia 70 ya hiyo miradi kama siyo 100 mpk sasa

Walitaka wayafanye yote kwa pamoja ili wajisifu na kuwazodoa waliopita kwamba wameshindwa wao ndio wanaweza matokeo yake ndo hayo,Dodoma,uchumi wa viwanda,Milioni 50,laptop,Noah tunazisoma kwenye history, Mzee wa msiba atakuwa anabugia pop corn tu akilitazama greda lililotukana mamba limezama kwenye tope.
 
Hatimae Sera zimekuwa za Kupika Majungu,Kuteka na Kupoteza wananchi,Kupiga risasi Wananchi,Kutngeneza Matukio baada ya kuboronga;Kukurupuka kwa hali ya juu,kutengeneza matatizo halafu kuja kuyatatua,Kutengeneza Mazingira ya Hofu.Teuzi kufanywa mtaji wa Kisiasa,Njama dhidi ya Upinzani wa Kweli na Kuubeba Upinzani wa Uongo.
Umesahau na sheria ya kumpa "uungu" msajili wa vyama vya siasa, ununuzi wa wabunge na madiwani wa upinzani ili waunge mkono juhudi, sheria ya kuziba midomo vyombo vya habari na wenye ujasiri wa kusema ukweli au kuhoji "mambo hovyo" ya siri-kali na kuwarudisha ng'ombe waliokatwa mkia na "mafisadi" nyumbani aka kwenye chama chao ili wapate raha.
 
Back
Top Bottom