gemmanuel265
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 8,485
- 18,053
Ubabe upo sana kuanzia rais mwenyewe, rc, dc n.k hawa wanavunja sheria makusudi ili kunyanyasa watu, kama huyajui haya pole sana.Mabadiliko sio sherehe ya harusi kwamba tutaimba na kucheka. Mabadiliko yana uchungu wake mwanzoni.
Hata kulima, kupalilia na kutunza shamba ni mbinde, kunachosha na kunakatisha tamaa. Ila wakati wa mavuno maumivu yote yanasahaulika.
Miradi mikubwa tunayoibeza siyo hewa, ipo dhahiri na inaonekana kwa macho. Ni uwezekaji mkubwa ambao manufaa yake ni very promising in the future. Sio chumvi uweke kwenye mboga itakolea hapo hapo.
Nidhamu Serikalini ipo juu. Leo hii hakuna ubabe wa kipuuzi na kutambiana mitaani kisa unaendesha STK kama zamani.
Halafu hizo political statements zinazotajwa zipo tu ili kuwajaza ari wananchi. We all need that to be able to move as a country. Sasa Serikali isiyohamasisha itasongaje?
Kwa ufupi, kuna sehemu tulikwama. Acha tubadili hali na kuchukua uelekeo mpya kama taifa. Wengine mtakuja kuelewa baadae sio lazima muelewe sasa.
Hesabu hazijagoma!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mnaposifia miradi isiyoisha mtwambie mmepambanaje na tatizo la ajira? Tatizo la umasikini mmepambana nalo vipi? Je, kuna takwimu zinazoenesha namna gani umasikini unapungua nchini?
Serikali yoyote iliyopo madarakani kazi yake kubwa ni kuboresha hali ya maisha ya wananchi kuanzia huduma bora za afya, maji, miundombinu, elimu bora na siyo bora elimu, lakini hayo yote serikali ya awamu hii imefail, angalau hiyo miundombinu lakini kwenye suala la umasikini awamu hii ya 5 hali ni mbaya zaidi ya awamu ya 4