Helkopter katika chaguzi zinasaidia nini ktk Jimbo moja?

Hayo maneno nadhani ungewambia CDM wana miaka mingi wanatumia Helkopta.
Na posho za maandamano ni ufujaji mkubwa wa kodi zetu Watanzania wapenda amani

Tumia akili tunaongelea helikopter
 
Matumizi ya Helkopter yanaashiria mambo mengi.

Kwa mfano.

Ukosefu wa barabara nzuri ambazo mtu anaweza kutumia kusafari kwa haraka.

Ukubwa wa eneo la jimbo

Kuokoa muda

Vyama vya siasa vina pesa nyingi sana(matajiri)
 
Ndugu wana Jf ningependa tujiulize swali hili juu ya faida ya Helicopter katika kampeni huko Igunga,
kwani imekuwa ni kama mashindano walianza wana CDM na baadae CCM na CUF wakaleta zao,sasa nacho jiuliza hapa ni vipi wananchi wa igunga watakavyo rudisha gharama za kurusha Helicopter 3 juu ya anga ya Igunga,kwani tunatambuwa kuwa Helicopter zile hazitumii maji na ni gharama sana kuzirusha angani lakini bado vyama vya siasa vimeamua kuzipeleka Igunga na hata hatujui ni gharama gani wametumia kuzirusha angani Je atakaye chaguliwa atazirudisha vipi gharama hizo?

Je bila hizo Helicopter wana Igunga hawataweza kupiga kura? ama tumewaonaje wana Igunga yaani bila Helicopter hawawezi fika katika mikutano?

Nina wasiwasi na hizo Helicopter kwani wanaIgunga watahitajika kuzilipia gharama zote pindi mgombea yeyote yule achaguliwapo,
 
Waulize CUF waliokurupuka kuazima helkopita bila kujua faida na hasara yake.
 
Helkopta zinasaidia kufika maeneo ambayo kwa njia za magari hayawezi kufika huko.Kuhusu gharama hilo ni jambo la kawaida sana na hakuna njia ya kukwepa gharama pia kodi zetu wananchi masikini unazozilalamikia na kuziona ktk helkopta tu ungekuwa muungwana kidogo kwa kuballance mambo.DOWANS WAMEKOMBA BILIONI 112 PMJ NA RIBA NDANI YAKE,hizi pesa nyingi zinazoibwa kiuwazi chini ya Serikali hii ya Tanzania iliyotokana na chama cha Mapinduzi hujaziona kabisa Kama ni wizi mkubwa!!!?
Wote wanaofuja pesa za walipa kodi ni wezi watupu!!
 
Waulize CUF waliokurupuka kuazima helkopita bila kujua faida na hasara yake.

ukimaanisha mgombea wao akichaguliwa ni lazima kwanza watafute mikataba feki ya madini ili warudishe deni la kukodisha hiyo ndege?

kwa hiyo wanaigunga wajiandae kupata likizo ya maendeleo mpaka hapo deni litakapo rudi,hii ni hatari sana mwa maendeleo ya Taifa hili kwa ujumla
 
Kama siyokufuja pesa za walipa kodi nini?naomba hapa tuwekane wazi mimi sioni mantiki kwa vyama kutumia gharama zilizopitiliza kwa kukodi helkopiter kwa ajili ya chaguzi ndogo kama Igunga kwani ni rahisi kufikika!

Gharama inayotumika kwa jimbo moja ni ufujaji wa kodi! Au helkopiter ni turufu katika uchaguzi? Mimi hili napingana nalo labda nasema labda kama hizo helkopiter hazitumii sehemu ya ruzuku ambayo nikodi yangu!

Naomba maelezo yenu.
Wabongo kwa kurukia mabingwa mimi sijasema chama chochote miminilichokuwa najaribu kueleza nikuhusu udogo wa jimbo maana jimbo la igunga barabara zake nyingi zinapitika ajabu kuona mihelikopiter inavuma utadhani ni afghanistan!Kajimbo kenyewe kadogo!Kwa CHADEMA kwa nini walikuwa wanatumia Helkopiter siku nyingi mimi naweza kusema hivi!:-
(a) Kwanza wao hawana nyenzo za usafiri wakati wa uchaghuzi mkuu!hivyo wao walilazimika kuwa na nyenzo kama helkopiter kwakuwawezesha kukimbiza mda kutokana na ratiba yao waliyokuwa wanapewa kwani nyingi ilikuwa zinaishia jioni na mikutano zaidi ya miwili!
(b) Pili CCM wana supoti kuwa mikoani kuanzia ngazi ya RC,DC mpaka tarafa wao wanapewa nyenzo hivyo unakuta ushindani wa uwanja ni mpana kwa CDM.Lakini kwa jimbo kama Igunga hapana hapa ni ufiujaji kwa wote waliotumia Helkopiter fullstop!
 
una uhakika kama barabara za Igunga ni nzuri? hebu fanya mahesabu yako.. unaweza kufanya mikutano zaidi ya tano kama utatumia gari? hata kama barabara ni nzuri!
 
Zinasaidia usafiri. Hapa kwetu helikopta ni kitu cha ajabu kutumika, kwa ushamba wetu na kutokuwa na "exposure". Wenzetu wanazitumia kama Taxi na njia moja muhimu ya usafiri.

Hainishangazi kuwa helikopta ni ajabu kwetu, kwani hata magari bado ni anasa hapa kwetu na mafanikio ya mtu hadi hii leo hapa kwetu yanapimwa kwa kuwa na au kutokuwa na gari. Seuse "Helicopter".

CHADEMA ni chama kinacho tawala mioyo ya watanzania wakiwemo CCM. Kila CDM wanacho anzisha lazima CCM na mkewe waige. Miaka ya nyuma CCM na Mkewe walianza kuwabeza CDM kwa kutumia Helkopta, baada ya kuwa na msimamo nao wameiga. Hii ni dhahili CCM hawana ubunifu tena kila kitu KIZURI wanawaiga CHADEMA.
 
si kila chama cha siasa kinapata ruzuku toka serikalini, bali ni vile vyama ambavyo vimekidhi masharti ya kupata ruzuku; masharti hayo ni pamoja na chama kuwa na wabunge/mbunge au madiwani/diwani
 
Back
Top Bottom