Helkopter katika chaguzi zinasaidia nini ktk Jimbo moja?

wewe mpuuzi ndesamburo akitumia helkopta hakuna tatizo hizo ni pesa zake na si za walipa kodi elewa wewe,ninawasiwais na upeo wako wa kufikiri
nI PESA ZAKE? Kazitoa wapi? hakuna pesa isiyo ya walipa kodi, hata kama ni za madawa ya kulevya lazima mkono wa mlipa kodi utahusika. Pole sana
 
wewe mpuuzi ndesamburo akitumia helkopta hakuna tatizo hizo ni pesa zake na si za walipa kodi elewa wewe,ninawasiwais na upeo wako wa kufikiri

Na Dr. Slaa nae Karatu, na Mbowe nae Hai, na hawa je walikuwa wanatumia pesa za nani walikuwa wanapaa na Helkopta?
 
na dr. Slaa nae karatu, na mbowe nae hai, na hawa je walikuwa wanatumia pesa za nani walikuwa wanapaa na helkopta?
ukipenda chongo utasema kengeza. Kipenda roho kula nyama mbichi.
 
wewe mpuuzi ndesamburo akitumia helkopta hakuna tatizo hizo ni pesa zake na si za walipa kodi elewa wewe,ninawasiwais na upeo wako wa kufikiri

Haya maneno angesema Mwita25, Ban siku nyingi lakini kayasema Pro-CDM hakuna tatizo endelea kunitukana mkuu
 
Hela yako ni pato linalotokana na shughuli unayoifanya. Kama Chadema au CCM watachangisha michango kutoka kwa wananchi hapo una haki ya kulalamika. Lakini ieleweke kila chama kina fungu lake kutoka serikalini na ni maamuzi ya chama husika juu ya matumizi ya hiyo hela. Waende na ungo, helikopta , treni, bodaboda ni juu yao wenyewe.
Mambo unayoandika nanakuengua na wazelendo wenye uerevu wa nchi hii. Swali la msingi ni kweli wewe huelewi kwamba ruzuku inatokana na kodi hivyo mtumiaji hata kama ni chama anawajibika kwa walipa kodi au unaandika unayoandika kutimiza lengo/kazi. Je watu kama wewe wanaipeleka wapi nchi yetu? Nasikitika bila kupata majibu ya maswali ninayojiuliza.
 
Matumizi ya helicopter mbili, gari la muziki na wasanii, kofia, tshirts na posho za chumvi na sabuni ni rushwa maradufu. Kila chama kiwe na style yake, Magamba wamekosa ubunifu!
 
Kama siyokufuja pesa za walipa kodi nini?naomba hapa tuwekane wazi mimi sioni mantiki kwa vyama kutumia gharama zilizopitiliza kwa kukodi helkopiter kwa ajili ya chaguzi ndogo kama Igunga kwani ni rahisi kufikika!

Gharama inayotumika kwa jimbo moja ni ufujaji wa kodi! Au helkopiter ni turufu katika uchaguzi? Mimi hili napingana nalo labda nasema labda kama hizo helkopiter hazitumii sehemu ya ruzuku ambayo nikodi yangu!

Naomba maelezo yenu.
Hakuna maelezo zaidi ya haya "wajinga ndiyo waliwao"
 
Helikopta ni chombo cha usafiri kinachoruka juu kwa juu na kwa muda wa haraka kuliko magari hivyo kuwafikia wananchi kwa uharaka zaidi. Kuhusu matumizi ya pesa hilo halikuhusu kwasababu kila chama kinapokea ruzuku kutoka serikalini.
Jamaa ana hoja za msingi. Kwa mfano kama Igunga kungeripuka kipindupindu, hizi Helkopta tunazoziona leo zingepelekwa kusaidia kuwawaisha wagonjwa kwenye Hospitali ya mkoa? Hizi nguvu za kuomba kura Igunga mbona huwa hatuzioni kwenye mambo ya msingi ya kujenga nchi yetu?

Ni asilimia 10 tu ya Tanzania ndiyo Ardhi yake imepimwa, na hata Igunga sijui ni asilimia ngapi ya Ardhi yake imepimwa, hizi Helkopta zingekodishwa kupeleka wataalamu wa kupima ardhi vijijini huoni kama zingeleta mabadiliko ya maana zaidi kuliko kwenda kuombea kura? Baada ya 2/10/2011 hizo helkopta zitabakia Igunga?

kuhus hela za ruzuku lazima ujue ni kodi zetu.
 
Ukitetea hili mimi binafsi sitakuelewa tuongelee swala la msingikatika hoja siyo katika itikadi!!
 
Back
Top Bottom