Helikopta ni chombo cha usafiri kinachoruka juu kwa juu na kwa muda wa haraka kuliko magari hivyo kuwafikia wananchi kwa uharaka zaidi. Kuhusu matumizi ya pesa hilo halikuhusu kwasababu kila chama kinapokea ruzuku kutoka serikalini.
Utumiaji wa helkopter ni ufujaji tu wa hela za walipa kodi na si vinginevyo
Utumiaji wa helkopter ni ufujaji tu wa hela za walipa kodi na si vinginevyo
Hayo maneno nadhani ungewambia CDM wana miaka mingi wanatumia Helkopta.
Na posho za maandamano ni ufujaji mkubwa wa kodi zetu Watanzania wapenda amani
Zinasaidia usafiri. Hapa kwetu helikopta ni kitu cha ajabu kutumika, kwa ushamba wetu na kutokuwa na "exposure". Wenzetu wanazitumia kama Taxi na njia moja muhimu ya usafiri.
Hainishangazi kuwa helikopta ni ajabu kwetu, kwani hata magari bado ni anasa hapa kwetu na mafanikio ya mtu hadi hii leo hapa kwetu yanapimwa kwa kuwa na au kutokuwa na gari. Seuse "Helicopter".
Nimekuambia kila chama kinapata ruzuku, au ulishawahi kuchanga hela ya helikopta?
ina maana hizo ruzuku zinatoka mbinguni?
kodi zetu tunazolipa ndio ruzuku hiyo hiyo....
Hela yako ni pato linalotokana na shughuli unayoifanya. Kama Chadema au CCM watachangisha michango kutoka kwa wananchi hapo una haki ya kulalamika. Lakini ieleweke kila chama kina fungu lake kutoka serikalini na ni maamuzi ya chama husika juu ya matumizi ya hiyo hela. Waende na ungo, helikopta , treni, bodaboda ni juu yao wenyewe.
Zinasaidia usafiri. Hapa kwetu helikopta ni kitu cha ajabu kutumika, kwa ushamba wetu na kutokuwa na "exposure". Wenzetu wanazitumia kama Taxi na njia moja muhimu ya usafiri.
Hainishangazi kuwa helikopta ni ajabu kwetu, kwani hata magari bado ni anasa hapa kwetu na mafanikio ya mtu hadi hii leo hapa kwetu yanapimwa kwa kuwa na au kutokuwa na gari. Seuse "Helicopter".
fungu kutoka serikalini linatoka wapi?
upeo wako ni aibu mno kuamini.....
Linatokana na kodi. Labda kifupi ni hivi: kuwapangia Chadema au CCM juu ya matumizi yao ni sawa na mtu akupangie juu ya matumizi ya mshahara wako (kama unao)
Kama siyokufuja pesa za walipa kodi nini?naomba hapa tuwekane wazi mimi sioni mantiki kwa vyama kutumia gharama zilizopitiliza kwa kukodi helkopiter kwa ajili ya chaguzi ndogo kama Igunga kwani ni rahisi kufikika!
Gharama inayotumika kwa jimbo moja ni ufujaji wa kodi! Au helkopiter ni turufu katika uchaguzi? Mimi hili napingana nalo labda nasema labda kama hizo helkopiter hazitumii sehemu ya ruzuku ambayo nikodi yangu!
Naomba maelezo yenu.
Utumiaji wa helkopter ni ufujaji tu wa hela za walipa kodi na si vinginevyo
akili zako zinafurahisha..
mshahara ni malipo ya kazi kwa mtu binafsi...
ruzuku ni pesa wanayopewa na ina masharti yake na marufuku yake...
ruzuku sio mshahara......