Helkopter katika chaguzi zinasaidia nini ktk Jimbo moja?

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,555
8,552
Kama siyokufuja pesa za walipa kodi nini?naomba hapa tuwekane wazi mimi sioni mantiki kwa vyama kutumia gharama zilizopitiliza kwa kukodi helkopiter kwa ajili ya chaguzi ndogo kama Igunga kwani ni rahisi kufikika!

Gharama inayotumika kwa jimbo moja ni ufujaji wa kodi! Au helkopiter ni turufu katika uchaguzi? Mimi hili napingana nalo labda nasema labda kama hizo helkopiter hazitumii sehemu ya ruzuku ambayo nikodi yangu!

Naomba maelezo yenu.
 
Helikopta ni chombo cha usafiri kinachoruka juu kwa juu na kwa muda wa haraka kuliko magari hivyo kuwafikia wananchi kwa uharaka zaidi. Kuhusu matumizi ya pesa hilo halikuhusu kwasababu kila chama kinapokea ruzuku kutoka serikalini.
 
Hakika hiyo ni kuonyeshana ufahari katika kampeni.

Wilaya moja helkopta tatu si zitagongana angani.

Tuombe kheir itawale shari. mambo yaende shwari.
 
Helikopta ni chombo cha usafiri kinachoruka juu kwa juu na kwa muda wa haraka kuliko magari hivyo kuwafikia wananchi kwa uharaka zaidi. Kuhusu matumizi ya pesa hilo halikuhusu kwasababu kila chama kinapokea ruzuku kutoka serikalini.

Utumiaji wa helkopter ni ufujaji tu wa hela za walipa kodi na si vinginevyo
 
Hayo maneno nadhani ungewambia CDM wana miaka mingi wanatumia Helkopta.
Na posho za maandamano ni ufujaji mkubwa wa kodi zetu Watanzania wapenda amani
 
nyie magamba mbona mna akili fup hvyo? Hiv huwa hamuwezi kuandika chochote bila neno amani? Hivi ni aman gan mnayoizungumzia?
 
Zinasaidia usafiri. Hapa kwetu helikopta ni kitu cha ajabu kutumika, kwa ushamba wetu na kutokuwa na "exposure". Wenzetu wanazitumia kama Taxi na njia moja muhimu ya usafiri.

Hainishangazi kuwa helikopta ni ajabu kwetu, kwani hata magari bado ni anasa hapa kwetu na mafanikio ya mtu hadi hii leo hapa kwetu yanapimwa kwa kuwa na au kutokuwa na gari. Seuse "Helicopter".
 
Najiuliza hivi, Igunga ni ile ile ya mwaka jana, wananchi ni wale wale. Mbona mwaka jana helkopta hazikuwepo Igunga?
 
Zinasaidia usafiri. Hapa kwetu helikopta ni kitu cha ajabu kutumika, kwa ushamba wetu na kutokuwa na "exposure". Wenzetu wanazitumia kama Taxi na njia moja muhimu ya usafiri.

Hainishangazi kuwa helikopta ni ajabu kwetu, kwani hata magari bado ni anasa hapa kwetu na mafanikio ya mtu hadi hii leo hapa kwetu yanapimwa kwa kuwa na au kutokuwa na gari. Seuse "Helicopter".

na hayo yote yamesababishwa na nchi kuongozwa na chama gani??????
 
ina maana hizo ruzuku zinatoka mbinguni?
kodi zetu tunazolipa ndio ruzuku hiyo hiyo....

Hela yako ni pato linalotokana na shughuli unayoifanya. Kama Chadema au CCM watachangisha michango kutoka kwa wananchi hapo una haki ya kulalamika. Lakini ieleweke kila chama kina fungu lake kutoka serikalini na ni maamuzi ya chama husika juu ya matumizi ya hiyo hela. Waende na ungo, helikopta , treni, bodaboda ni juu yao wenyewe.
 
fungu kutoka serikalini linatoka wapi?
upeo wako ni aibu mno kuamini.....
 
Zinasaidia usafiri. Hapa kwetu helikopta ni kitu cha ajabu kutumika, kwa ushamba wetu na kutokuwa na "exposure". Wenzetu wanazitumia kama Taxi na njia moja muhimu ya usafiri.

Hainishangazi kuwa helikopta ni ajabu kwetu, kwani hata magari bado ni anasa hapa kwetu na mafanikio ya mtu hadi hii leo hapa kwetu yanapimwa kwa kuwa na au kutokuwa na gari. Seuse "Helicopter".

Ni kweli bibie ni ushamba tu ndio maana hawatumii hellicopter eti eeeh.........si ndio maana ni ushamba tu kutumia magari kama ambulance ndo mana tumetumia bajaji kama ambulance eeeh si unajua nchi nyingine zilizoendela bajaji zinafanya vizuri sana eeh. Ni ushamba kwa waziri kutembelea landrover eeeh bora watumie V8 au HUMMER eeeh.........CCM oYEEEEEEEE
 
fungu kutoka serikalini linatoka wapi?
upeo wako ni aibu mno kuamini.....

Linatokana na kodi. Labda kifupi ni hivi: kuwapangia Chadema au CCM juu ya matumizi yao ni sawa na mtu akupangie juu ya matumizi ya mshahara wako (kama unao)
 
akili zako zinafurahisha..
mshahara ni malipo ya kazi kwa mtu binafsi...
ruzuku ni pesa wanayopewa na ina masharti yake na marufuku yake...
ruzuku sio mshahara......
 
Kama siyokufuja pesa za walipa kodi nini?naomba hapa tuwekane wazi mimi sioni mantiki kwa vyama kutumia gharama zilizopitiliza kwa kukodi helkopiter kwa ajili ya chaguzi ndogo kama Igunga kwani ni rahisi kufikika!

Gharama inayotumika kwa jimbo moja ni ufujaji wa kodi! Au helkopiter ni turufu katika uchaguzi? Mimi hili napingana nalo labda nasema labda kama hizo helkopiter hazitumii sehemu ya ruzuku ambayo nikodi yangu!

Naomba maelezo yenu.

Helkopta zinasaidia kufika maeneo ambayo kwa njia za magari hayawezi kufika huko.Kuhusu gharama hilo ni jambo la kawaida sana na hakuna njia ya kukwepa gharama pia kodi zetu wananchi masikini unazozilalamikia na kuziona ktk helkopta tu ungekuwa muungwana kidogo kwa kuballance mambo.DOWANS WAMEKOMBA BILIONI 112 PMJ NA RIBA NDANI YAKE,hizi pesa nyingi zinazoibwa kiuwazi chini ya Serikali hii ya Tanzania iliyotokana na chama cha Mapinduzi hujaziona kabisa Kama ni wizi mkubwa!!!?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom