Tanzania ni nchi tajiri lakini wananchi wake ni masikini, ajabu sana

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania.jpg

Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania
Wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya...jpg

Wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Hifadhi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania​

Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.

Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.

Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.

Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.

''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.

Chanzo: BBC
 
tanzania ni nchi ya amani na utajiri lakini wananchi wake wanatumiwa na ccm kuongoza utumbo mpana kimawazo.
leo naangalia TBC uzinduzi wa vyoo,ccm vijana bukoba wakilima barabara,wananchi wakijengeshwa shule kwa kodi yao.

leo ukitaka kusema kuhusu DP world imetukosea nenda kwa ndugu zetu waislamu utasikia mwarabu kabarikiwa.
inamaana sisi tujabarikiwa .africa tuamke jamani binadamu wote sawa ila unafahamu matendo yao
 
Nikweli mkuu... lkn sijui ni lini tutakuwa matajiri, lkn hii nchi ngumu sanaa
 
Nikweli mkuu... lkn sijui ni lini tutakuwa matajiri, lkn hii nchi ngumu sanaa
Tutakuwa Matajiri siku tukipata Viongozi wetu wanao tutawala wakiwa wanawapenda Wananchi wao. Na hao hao viongozi wawe waadilifu katika uongozi na suala la ulaji wa Rushwa usikuwepo kabisa hapo ndipo Wananchi aka walala hoi tutakuwa na sisi matajiri. Pasipo na hivyo tutakuwa Masikini maisha yetu yote.
 
View attachment 2672170
Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania
View attachment 2672171
Wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Hifadhi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tz.​

Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.
''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford. chanzo.BBC
VIONGOZI WAKE NI MATAJIRI WA KUTUPWA CCM OYEE
 
Mngenilipa hii nchi, watanzania wangelikuwa hawalipi makodi ya ajabu ajabu, facilitations kwa wananchi kama makazi bora, ukiwa mtanzania unakopeshwa, huduma za tiba bure kama zambia
 
Wanaojua kutumia rasilimali zao warabu tu sie wafrica acha wafaidike watu wengine
 
tuna madini ya chuma cha pua liganga na mchuchuma lakini hatuwezi kuchimba wenyewe maskini. Ni ma billion ya Tons yamelala ardhini urithi wetu toka mwa Mungu baba.
Badala yake tunanunua chuma kutoka China cha kujengea mataruma ya reli yetu ya mwendo kasi.

Soma hii hekaya...

View attachment 2672170
Hifadhi kubwa zaidi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania
View attachment 2672171
Wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.

Hifadhi ya gesi ya Helium yagunduliwa Tanzania​

Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.

Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.

Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.

Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.

''Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford.

Chanzo: BBC
Waarabu kwenye helium MARUFUKU, tuwaachie wajukuu zetu waichimbe wenyewe
 
Nauliza tu, gesi ya Mtwara hatuwezi kui - liquify (LNG) then tukawa tunaiuza nchi za ulaya? Bandari si tunayo jamani hivi hapa tunakwapa wapi? ni mtaji, utalaam ama utashi? watalaam tufungueni macho.

Sasa hivi gesi ni kipusa kikubwa nchi la Ulaya, kwa nini tusitumie hii fursa ndani ya miaka 3 hadi 5 tukawa na mapato ya uhakika na mabillion ya dola.

Tutakuwa Matajiri siku tukipata Viongozi wetu wanaotutawala wakiwa wanawapenda Wananchi wao. Na hao hao viongozi wawe waadilifu katika uongozi na suala la uraji wa Rushwa usikuwepo kabisa hapo ndipo Wananchi aka walala hoi tutakuwa na sisi matajiri. Pasipo na hivyo tutakuwa Masikini maisha yetu yote.
Mimi ni mlipa kodi.. ukweli ni kwamba Kodi tunatozwa kubwa sanaaa hadi tunashindwa kuendeleza biashara zetu
 
Unajua Utajiri wa Congo ? Nini kinawapata ?

Kwa walamba asali hawa na walafi ambao hawana uzalendo na wabinafsi wasiotosheka shukuru hata kile kidogo unachopata (ukiondoa ulafi wa watawala watanzania ni watu poa sana)....,

Kuwa na Resources haku-translate directly kwenye utilization ya hizo resources... Hususan ukiwa na mentality kwamba hakuna unachoweza bali wengine ndio wakufanyie...

Resources in Africa are a curse rather than a blessing due to poor public management, mwananchi hapo hana lawama kabisa, espcially kwa Mtanzania ambaye sio mbishi, wana umoja wa kitaifa n.k. (Which means angepatikana mtu mwenye vision ni rahisi kuwa-ongoza na wakajikwamua) Tatizo walamba asali wanapandikiza chuki na kuwaminya hawa wananchi ambao watapoteza huo ubora wao walionao sasa.....
 
MRADI WA LINGANGA NA MCHUCHUMA SI NDOTO TENA
Na LEONARD MANG’OHA
MRADI WA LINGANGA NA MCHUCHUMA SI NDOTO TENA.jpg

MWELEKEO wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 uliotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, hivi karibuni unaonyesha kuwa bajeti hiyo imeelekezwa zaidi katika miradi ya maendeleo hususan ya ujenzi wa reli, miradi ya gesi na makaa ya mawe Liganga na Mchuchuma.

Kuelekezwa kwa fedha nyingi kwenye miradi ya ujenzi, kunagusa dhamira ya Rais Dk. John Magufuli kuhusu ukamilishaji wa miradi ya maendeleo itakayosaidia kuinua sekta ya viwanda.

Kuimarika kwa sekta ya viwanda kutapunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza bidhaa nje ya nchi ambazo zinaweza kuzalishwa nchini sambamba na kutoa ajira kwa wazawa.

Kutajwa kwa mradi wa Linganga na Mchuchuma kama moja ya vipaumbele, kunaibua matumaini mapya kwa Watanzania walio wengi ambao wamekuwa wakingoja kukamilika kwa mradi huo japo si mara ya kwanza kutolewa maneno ya matumaini kuhusu maendeleo yake.

Mradi wa Liganga na Mchuchuma

Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC), Abel Ngapemba, mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu hadi mitano, huku ukitarajiwa kugharimu zaidi ya Sh trilioni 6.564.

Anasema mikataba ya mradi huu ilikwishasainiwa na utafiti kiasi cha chuma na makaa ya mawe yaliyopo na teknolojia itakayotumika wakati ya uchimbaji tayari vipo wazi.

Anaeleza kuwa, uchimbaji wa chuma cha Liganga unahitaji teknolojia maalumu kutokana na chuma kinachopatikana eneo hilo kuwa na sumaku tofauti na madini ya aina hiyo yanayopatikana sehemu nyingine duniani.

Anasema ujenzi wa mradi huo unachukua muda mrefu kutokana na kuhusisha miradi mitano ambayo ni pamoja na migodi miwili ya makaa ya mawe na chuma, kinu cha umeme wa makaa ya mawe, kiwanda cha kutengenezea bidhaa za umeme na ujenzi wa njia ya kusafirishia nishati kutoka Mchuchuma hadi Liganga.

Megawati 600 za umeme kuzalishwa

Ngapemba anasema mradi huo utakaotekelezwa na Kampuni ya Kichina ya Sichuan Hongda Cooperation Limited, utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 600 ambapo kiwanda cha chuma kitatumia Megawati 250 na zitakazosalia zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Kati ya hizo Megawati 250 zitatumika katika kiwanda cha kufua chuma kitakachojengwa Liganga, huku Megawati 350 zikitarajia kuingizwa katika gridi ya Taifa.

“Umeme huu utapelekwa katika ‘sub-stantion’ ya Makambako hivyo ni wazi kuwa utapunguza tatizo la kukosekana kwa umeme na kusaidia kuanzisha kwa viwanda vingine na unaweza kuongezeka baada ya kuanza uzalishaji,” anasema Ngapemba.

Mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu za makaa ya mawe na tani milioni moja za chuma kwa mwaka, hivyo ni wazi kuwa itapunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza chuma kutoka nje ya nchi.

Kuwainua wananchi kiuchumi

Anasema katika kuhakikisha wanainua kiwango cha uchumi kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo unatekelezwa ambapo tayari wamekuwa wakiwapa semina kuhusu namna ya kutumia fursa zinazopatikana kutokana na utekelezaji wake.

“Tumekuwa tukiwashawishi wananchi kujihusisha na shughuli za uzalishaji, kuwaweka kwenye makundi na kuwawezesha ili waendeshe shughuli zao kwa urahisi.

“Hii itawasaidia kupata fedha kwa kutumia fursa za mahitaji kwa watu watakaokuwa wakifanya kazi hapa. Kwa mfano wakati wa hatua hizi za uchunguzi, wananchi walifanya biashara ya kuuza kuku kwa wingi,” anasema Ngapemba.

Ngapemba anasema ili kuhakikisha wananchi wananufaika na mradi huo, wameamua kuwajengea wale ambao maeneo yao yataingizwa kwenye mradi badala ya kupewa fedha ili kuwawezesha kupata makazi bora.

“Tutahakikisha tunaanzisha kijiji kwa kuwajengea na kuweka huduma muhimu kama shule kwa gharama ya mradi na kwa wale watakaochukuliwa maeneo au mazao yao pia watafidiwa,” anasema.

Ngapemba anasema mradi huo unalenga kuwezesha kuanzishwa kwa miradi mingine kwa kuipa nishati na kufungua fursa nyingine za uwekezaji.

Kuchochea maendeleo ya sekta nyingine

Mtaalamu wa uchumi na mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Kilimo (SUA), Profesa Damiani Gabagambi, anasema kukamilika kwa mradi huo pamoja na kutoa faida za moja kwa moja kama nishati na ajira, pia utatoa matokeo zaidi (multiplier effect) kwa sekta nyingine.

Anasema kwa wafanyakazi watakaoajiriwa, watanunua bidhaa mbalimbali kwa matumizi yao binafsi, hivyo kukuza biashara katika maeneo ya karibu na mradi.

Anasema wakulima wataweza kuuza mazao yao ya kilimo na mifugo, hivyo nao watainuka kiuchumi.

Bila shaka sekta za hoteli na nyumba za wageni zitaimarika kutokana na kuongezeka kwa mwingiliano wa watu katika eneo hilo.

Kuimarisha Bandari ya Mtwara

Kukamilika kwa mradi wa Mchuchuma na Liganga kutaongeza ufanisi wa Bandari ya Mtwara ambayo Serikali imeanza juhudi za kuiboresha, hivyo wafanyabiashara wataweza kupitisha mizigo yao wanayoagiza kutoka nje ya nchi.

Kuimarika kwa shughuli za bandari hii kutachagizwa zaidi na uwapo wa reli ya kiwango cha kimataifa (standard gauge) inayotarajiwa kujengwa katika ya Bandari ya Mtwara hadi Mbambabay, Mchuchuma na Liganga ambapo tayari upembuzi yakinifu umekamilika na Kampuni hodi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) wakiwa kwenye mchakato wa kumtafuta mshauri wa fedha ili kufahamu kiasi kitakachotumika kujenga mradi huo.

Bandari hiyo inaweza kuimarika zaidi ikiwa nchi jirani za Kongo DRC, Zambia na Malawi zahitaji kutumia reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1,000 ambako kutakuwa na gharama nafuu ikilinganishwa na Bandari ya Dar es Salaam ambapo hulazimika kusafiri umbali mrefu zaidi.

Kwa muda sasa, Bandari ya Mtwara imekuwa hoi kutokana na meli kubwa kutotia nanga bandarini hapo kwa kukosa gati kubwa linalostahimili mahitaji wa meli hizo.

Mapema mwezi uliopita akiwa ziarani mkoani Mtwara, Rais Dk. Magufuli aliwataka wakandarasi waliosaini mkataba wa kupanua bandari hiyo kuanza kazi mara moja na kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya miezi 20.

Bila shaka maboresho hayo yatafungua fursa za usafirishaji ambapo wafanyabiashara wa mikoa ya kusini na Kusini Magharibi wataingiza mizigo yao kupitia huko.

Kwa jitihada zinazooneshwa na Serikali ikiwa zitapewa nguvu inayostahili na miradi ya aina hii kutekelezwa kwa weledi, utaleta tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi. chanzo. MRADI WA LINGANGA NA MCHUCHUMA SI NDOTO TENA - Mtanzania
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom