Mama Obama
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 1,620
- 1,088
Cha kushangaza JR anaona sawa tu, na ndio maana kajifanya na kuendelea kuivaa rozari kama vile yeye mtakatifu! Na kwamba sisi hatujuwi tunachoongea, kinacholiza wananchi zaidi ni zile 1.6b za Tiba na Chenge, hawa ni wabunge majimboni, sielewi na siamini wanawatetea wanajimbo kivipi huku wakipokea rushwa kubwa kama hizo! Halafu wanadiriki kabisa kuomba miundo mbinu na maendeleo bungeni huku akaunti zao zimetuna kwa mabilioni na hata kuziita za mboga ua vijisenti! Some guts eehh?! Mafiriauni kabisa...
Tibaijuka nilikuwa namuheshimu sana, mwanamke aliyesoma, na yuko exposed kuja kuungana Na HUYU jamaa kupokea pesa kutoka kwa HUYU jamaa nilichoka. Kenya walimfukuza kazi nikafikiri walimuonea ukabila, lakini sio, nionyeshe rafiki yako nitakuambia nitajuwa tabia yako. . Chenge, sishangai. Yeye ni mmoja wa ngenge, waliofanya of Watanzania kupata shida nyingi. Wako bungeni sio kwa kuwakilisha watu, , ni kupata inside information na kuitumia kuwaibia Watanzania. Chenge angefungwa zamani kwa maovu mengi ya wizi aliyoyafanya ikiwa pamoja na rada. Kikwete akamuacha huru, ili aendekee na kazi ya kuwaibia Watanzania. Account yake iliyoko Isle of Man Grest Britain ambayo aliweka pesa za Rada zaidi ya million dola za kimerekani aliruhusuwa kuendelea nayo Wakati watoto Bariadi jimbo analoliwakilisha watoto wanakunywa maji machafu. Katiba yetu ni mbovu Watu kama Chenge, TIBAIJUKA hawatakiwi kuwa bungeni.