Kesi ya Mbowe na wenzake imethibitisha ubovu wa mahakama ya Tanzania. Ni dhahiri chombo hiki si huru na wala hakina uadilifu. Mahakama inashirikiana na mawakili wa Serikali kutoa nyaraka za mahakama kuwapa mashahidi wa upande wa Serikali. Jambo hili limethibitika wazi.
Jambo la kushangaza ni kuwa uongozi wa mahakama upo kimya! Kama tungekuwa na Jaji Mkuu mwenye hekima, angejiuzulu. Kashfa hii ni kubwa sana.
Mbowe na wenzake, kwa uthibitisho huu wa mahakama kushirikiana na washtaka wao, wana haki ya kutamka wazi kuwa hawana imani na hii mahakama, na hivyo utafutwe utaratibu mwingine wa kuendesha shauri lao, nje ya chombo hiki kilichotekwa nyara na Serikali.