Hebu tushauriane kidogo

Hebu tushauriane kidogo

Fixed Point, afadhali umetangulia kutoa hili dukuduku, wajua ni ngumu sana eti upo karibu na home sasa unaenda kulala hotelini, kwangu ni ngumu sana, napata shaka sana mahusiano yaliyokuwapo baina ya mume na mke....
wajua angekuwa nyumbani hata hao wauwaji wangepata shida sana kutekeleza suala lao, kwangu mimi kulala kwake kula kumenipa mashaka sana na kifo chake...
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke atakushauri vizuri sana kwenye mambo mengine lakini si maswala ya vitisho vya mauaji!! Sana sana atapanic na kuanza kulia lia hovyo na kuchanganyikiwa tu labda huyo mwanamke awe naye ni bedui kweli kweli ndo mana nakwambia kwenye maswala haya hakuna cha mwanamke msomi.
kama ni hivyo basi hakuwa na haja ya kumwambia mkewe kuwa anatafutwa kuuawa, angepiga kimya ili asimpanikishe mkewe. kitendo cha kumwambia na kuondoka ndo kimeleta picha ngumu zaidi
 
Huyo mwanamke atajilaumu maisha yake yote coz hakutakiwa kumuacha mume wake peke yake,angekuwa mume wangu cdhan km ningemwacha peke yake hata dakika moja na ambavyo kashaniambia katishiwa kuuliwa wauwaji wangefurah
 
Mwanamke atakushauri vizuri sana kwenye mambo mengine lakini si maswala ya vitisho vya mauaji!! Sana sana atapanic na kuanza kulia lia hovyo na kuchanganyikiwa tu labda huyo mwanamke awe naye ni bedui kweli kweli ndo mana nakwambia kwenye maswala haya hakuna cha mwanamke msomi.

si kweli mkuu. ..msomi atleast anakuwa na uelewa wa mambo yanavyoenda duniani..naongea hili with experience
 
Fixed Point, afadhali umetangulia kutoa hili dukuduku, wajua ni ngumu sana eti upo karibu na home sasa unaenda kulala hotelini, kwangu ni ngumu sana, napata shaka sana mahusiano yaliyokuwapo baina ya mume na mke....
wajua angekuwa nyumbani hata hao wauwaji wangepata shida sana kutekeleza suala lao, kwangu mimi kulala kwake kula kumenipa mashaka sana na kifo chake...
hata kama wangemuua basi kusingekuwa na maswali mengi toka kwa watu. wanasema kajiua na tai, wengine kauawa, which is which?
Mke angejua ukweli kama kajiua au kauawa
 
Mmmh! How? Sijaelewa hapa usomi na maelewano ndani ya ndoa yanahusiana vipi.....kuna watu wengine hawajasoma lkn wana uelewa na busara na kuna wasomi wa madesa...akili yao ya maisha ni ndogo kupita maelezo
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Huyo mwanamke atajilaumu maisha yake yote coz hakutakiwa kumuacha mume wake peke yake,angekuwa mume wangu cdhan km ningemwacha peke yake hata dakika moja na ambavyo kashaniambia katishiwa kuuliwa wauwaji wangefurah
ndo maana mimi nikasema ningemweka chini ya ulinzi watu hawaamini.
yaani hata job ningempeleka na kwenda kumfwata. akiwa job najua yupo na watu wengine......
hapa ambacho ningehakikisha tu ni asiwe peke yake
 
yaani maswali ni mengi rafiki!
inawezekana mume hakutaka kuwa na mtu....... sasa kama hakutaka kuwa na mtu kwa nini alionyesha wasiwasi na kulalamika?
yaani mimi kunionyesha wasiwasi tu ningemweka chini ya ulinzi.....

Mwenye ukweli kamili ndio huyo kaondoka, nimesoma mahali kajinyonga na tai, tai? mtu mzima? huyu nadhani alijiamini kwamba wangeweka mambo sawa na wabaya wake then mambo yakawa sivyo, kinachonishangaza ni kwamba alienda hoteli ya mtaani kwake,(kama nilielewa vizuri) kwanini asingeenda mbali au angeamua basi tu kulala kwake? haya mambo ya siri humu manyumbani kwetu yanaponza,inaonekana mume alitaka hii kitu iwe siri hata kwa mke wake, hakutaka kushirikisha yoyote, sasa kaenda kaacha watu njia panda.
 
Labda wote walichanganyikiwa wakashauriana mwanaume akajifiche hotelini ili wakija home wasimkute, labda...wauaji walimuita wana maongezi nae!! Labda....labda...!!!

Labda ilishafahamika kwamba atakufa tu hivyo ilikuwa ni suala la kuchagua tufe wote au ufe peke yako mimi mama nibaki nilee watoto, bado sijapata majibu ni kwanini ulimboka yupo kimya sana, ghafla anakufa Mgimwa, nikiwa naendelea kujiuliza kifo cha mgimwa kilikuwaje kuwaje ghafla linatokea hili la Bosi wa Ewura. Ngoja nisubirie Gazeti la M'nahalisi lifunguliwe huenda hizi Labda labda zitaisha.
 
ndo maana mimi nikasema ningemweka chini ya ulinzi watu hawaamini.
yaani hata job ningempeleka na kwenda kumfwata. akiwa job najua yupo na watu wengine......
hapa ambacho ningehakikisha tu ni asiwe peke yake

unaamini kwa kufanya hivvyo huyu baba angenusurika na mauti? hiki kitu kinaonekana kilipangwa kikapangika, kama walidhamiria hata angelindwaje wangetekeleza tu, hao polisi wenyewe ndio wale wale tu, labda ungefanikiwa kushuhudia kifo chake tu, huyu mtu inaelekea alikuwa na siri nzito sana ambayo ingeharibu/chafua watu sana.
 
si kweli mkuu. ..msomi atleast anakuwa na uelewa wa mambo yanavyoenda duniani..naongea hili with experience

Mkuu may be sijajua unamaanisha nini unaposema msomi. Uwezo wa kupambanua mambo ni akili ya mtu binafsi....haihusiani na elimu...umeshawahi kuona mtu yupo chuo kikuu lkn hata kuwasha computer ni tatizo licha ya kwamba anazion kila siku? Elimu hii ya darasani inatusaidia tu kupanua ufahamu na kujua baadhi ya mambo yanaenda vipi....lkn katika suala kama hili elimu sidhan kama inahusika...inategemea akili ya mtu na kiwango cha hekima alichonacho tu.
 
Mwenye ukweli kamili ndio huyo kaondoka, nimesoma mahali kajinyonga na tai, tai? mtu mzima? huyu nadhani alijiamini kwamba wangeweka mambo sawa na wabaya wake then mambo yakawa sivyo, kinachonishangaza ni kwamba alienda hoteli ya mtaani kwake,(kama nilielewa vizuri) kwanini asingeenda mbali au angeamua basi tu kulala kwake? haya mambo ya siri humu manyumbani kwetu yanaponza,inaonekana mume alitaka hii kitu iwe siri hata kwa mke wake, hakutaka kushirikisha yoyote, sasa kaenda kaacha watu njia panda.
siri ni nzito sana. lakini mke anasema alijua kuwa mumewe anataka kuuawa, yaani mume alimwambia mkewe.
hilo la kulala hoteli ya karibu na home nayo ni siri nyingine.
Ndo maana nikajiuliza hata hicho kifo, kuna wanaosema kauawa na wanaosema kajiua..... yaani ni michanganyiko tu
 
mimi mwenyew nimekuwa na maswali pia bila kuwa na majibu sahihi

ila nikawa na ile kauli ya kwamba ndoa/nyumba za watu kuna siri na ni vigumu sisi kujua
ndoa nyingi watu wana usiri wa kutoweka mambo bayana na pia kuna ile ya kutokuwa na mawasiliano mazuri

mwanamke ni msaidizi wake ina maana hajui siri za mumewe??hta kama hajui iweje mwache hotelin peke yake na kwenye kipindi kigum ambapo ndo anahitaj ulinzi na mtu wa kumfariji ...

je ina maana mkewe hakutambua hil???
hajajua mumewe anahitaji ulinzi hta kama sio wa polis bsi hta ndugu au yye mkewe alale nae pale hotelini
nimesoma gazet a mwananchi la leo naona utata tu kwa maana mwanamke hakujtoa kwa ajili ya kumlinda mumewe kwenye hiki kipindi
 
unaamini kwa kufanya hivvyo huyu baba angenusurika na mauti? hiki kitu kinaonekana kilipangwa kikapangika, kama walidhamiria hata angelindwaje wangetekeleza tu, hao polisi wenyewe ndio wale wale tu, labda ungefanikiwa kushuhudia kifo chake tu, huyu mtu inaelekea alikuwa na siri nzito sana ambayo ingeharibu/chafua watu sana.
nina uhakika kabisa angekufa, lakini nisingejiuliza kafaje, kajiua au kauawa?
hilo nalo ni swali kubwa sana, kama kauawa au kajiua, maana yote yanatajwa.
 
si kweli mkuu. ..msomi atleast anakuwa na uelewa wa mambo yanavyoenda duniani..naongea hili with experience

vipi unamfahamu mke wa marehemu? labda tujue kiwango chake cha elimu! Huku kujua sana kumetufanya tukadumaa na kujipa moyo kwa sababu ya elimu unadhani unaweza kuwa sahihi katika mambo yote si kweli hata kidogo!!! kuna vingi vya kuangalia ktk hili jambo, wewe mojakwamoja unaona kifo hiki kimesababishwa na mkewe kutokumshauri vizuri.

Hapa issue ilikuwa makubaliano na mawasiliano marehemu alikuwa msomi na alifahamu haki zake za msingi, kama aliona mashaka na kwa uwezo aliokuwa nao basi angeweza kutoa taarifa polisi na akapata ulinzi wa kutosha.
 
Huyo mwanamke atajilaumu maisha yake yote coz hakutakiwa kumuacha mume wake peke yake,angekuwa mume wangu cdhan km ningemwacha peke yake hata dakika moja na ambavyo kashaniambia katishiwa kuuliwa wauwaji wangefurah

Ni kweli kabisa mkuu...lazima ajilaumu,ingetokea wamemuua wakiwa pamoja angejifariji kwambs at least I tried kumlinda mume wangu ila tu nilizidiwa nguvu.....lkn huwezi jua pengine kwenda kulala hotelini ilikuwa ni idea ya mkewe
 
Dada Fixed Point hii michezo ipo sana sana, kuna many dirty games going on everywhere..... Si mlaumu mkewe maana yeye alimwamini MUNGU na ndio maana baada ya pale alimwambia waombe kwa MUNGU awaepushie jambo hilo. Kuna watu wako nyuma ya huo mchezo wa hizo Billion 83 kosa lake inawezekana ni kwenda kinyume na wenzake, na kwenda kwake kinyume ina maana alisimamia ukweli, therefore the best option ilikua ni kumuondoa at any cost.
 
Last edited by a moderator:
mimi mwenyew nimekuwa na maswali pia bila kuwa na majibu sahihi

ila nikawa na ile kauli ya kwamba ndoa/nyumba za watu kuna siri na ni vigumu sisi kujua
ndoa nyingi watu wana usiri wa kutoweka mambo bayana na pia kuna ile ya kutokuwa na mawasiliano mazuri

mwanamke ni msaidizi wake ina maana hajui siri za mumewe??hta kama hajui iweje mwache hotelin peke yake na kwenye kipindi kigum ambapo ndo anahitaj ulinzi na mtu wa kumfariji ...

je ina maana mkewe hakutambua hil???
hajajua mumewe anahitaji ulinzi hta kama sio wa polis bsi hta ndugu au yye mkewe alale nae pale hotelini
nimesoma gazet a mwananchi la leo naona utata tu kwa maana mwanamke hakujtoa kwa ajili ya kumlinda mumewe kwenye hiki kipindi
ukisoma ile habari inaonyesha mkewe alikuwa anajua kuwa mumewe anataka kuuawa..... ingawa inawezekana kabisa asijue sababu ya kuuawa, lakini alijua kuwa anatafutwa kuuawa.
cha kujiuliza hapa ni kwa nini alimwacha peke yake kipindi hiki kigumu? hiyo nayo ni part and parcel ya ndoa, lol!
 
Back
Top Bottom