Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
Heshima kwenu wakuu.
Tangu jana niliposoma uzi wa kuhusu yule meneja wa EWURA aliyekutwa amefariki hotelini nimekuwa nikisumbuliwa na maswali mengi sana ya mahusiano. Kwenye lile gazeti wanasema kuwa mke wa marehemu alimwambia mwandishi kuwa mumewe alilalamikia watu wanataka kuutoa uhai wake. Mnaweza kusoma habari kamili hapa...
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/660513-bosi-wa-ewura-akutwa-amefariki-hotelini.html
Swali la kwanza nililojiuliza ni kwa nini mke alimruhusu mumewe akalale hotelini peke yake? ina maana hao watu kama wangeweza kuja kumuua nyumbani ambapo yupo na familia yake ndo wangeshindwa kumfwata huko hotelini ambapo yupo peke yake? Swali la pili, kwa nini mke hakutoa taarifa polisi? kama mume ana wasiwasi kiasi cha kukimbia nyumba basi hilo swala ni serious sana, kwa mtazamo wangu nadhani ningeripoti polisi ili angalau wajue kuwa kuna shida fulani.
Mambo kama haya huwa yanatokea sana katika familia zetu. Inawezekana ni sababu ya pressure za kazi, biashara, familia, ndugu, n.k. nilitamani tu tujadiliane na kushauriana jinsi ya kuyakabili mambo kama haya.
Naomba hapa tujadili kimahusiano zaidi, hayo mambo ya kisiasa tuyaache huko siasani.
Karibuni kwa mjadala