Hebu tujiulize undani wa hili ‘Tishio la UGAIDI’

Bado hujajibu swali
Leading question linawafaa wasioelewa aina hiyo ya maswali.

Yaani nitaje jina la chama kinachofaa ilihali kila mtu ana itikadi anayoiona inafaa na wakati huo huo tunahudumia propaganda za CCM kuwa wapinzani hawajawa tayari kushika hatamu za nchi.

Think
 
WANANCHI-WAONDOLEWA-HOFU-KUHUSU-TAARIFA-ZA-UBALOZI-WA-MAREKANI.jpg
 
Nalipongeza jeshi la polish kwa kutoa tamko lenye maelekezo chanya kwa kadhia hii.

Athalan ninalishauri jeshi la polisi Tanzania kuanza kujenga haiba njema baina yake na jamii. Polisi ni jamii wanayotoka hivyo kunapokuwepo na kuaminiana na kuishi kwa viapo vyao ni njia sahihi ya kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi.

Polisi wahakikishe wanatuza siri ya vyanzo vyao vya taarifa kwa sababu kuna tabia ya baadhi ya polisi kuvujisha vyanzo vya taarifa kwa wahalifu hata kufikia wananchi kuhofia kutoa taarifa za mwenendo unaoashiria uhalifu.

Pongezi kwao
 
Wengi wetu humu Tumeona, tunesikia na tumesoma tamko la Ubalozi wa Marekani kuhusu uwezekano wa kutokea shambulio la ugaidi hapa nchini.
View attachment 2497876

Tumesikia mwitikio wa jeshi la polisi kuhusu hatua wanazochukua dhidi ya tahadhari hiyo huku wakituhakikishia usalama na ulinzi. Lakini mimi nineona hapo kuna jambo la kutafakari kuhusu uwezo wetu katika usalama wa ndani ya nchi yetu sambamba na uhusiano wa dola na wananchi.

Iwapo taifa la nje linaweza kuchunguza na kupata uthibitisho wa kuwepo na tishio la usalama nchini na wakatoa tahadhari maana yake kuna kulegalega na kuzembea kwa vyombo vyetu vya ulinzi hususani espionage ya ndani ya nchi.

Serikali ya Tanzania imeeza kupitia viongozi waandamizi kuhusu uwekezaji mkubwa walioufanya katika kununua mitambo ya kudukua mawasiliano ya mitandaoni hususani ikiwalenga wahalifu wa mitandaoni. Hapo awali nilisema kuwa tambo za serikali zinathibitisha kuhusu kuingilia uhuru wa wananchi wake binafsi kwa sababu mifano ya waliochukuliwa hatua hata kufikishwa mahakamani ni wale waliotuhumiwa kutoa kauli ama maneno ya kuudhi dhidi ya watawala. Hatujawahi kuona ama kusikia wahalifu ambao wanafanikisha matukio ya kihalifu ama wanaotoa matishio ya usalama wetu wa ndani waking'amuliwa ama kuchukuliwa hatua.

Marekani kupitia taasisi zake za nje wamejijengea uwezo wa kuwez kupenya vihunzi vya usalama vya makundi ya kiuhalifu dhidi ya binadamu na wakaweza kutambua mipango yao na kwa nia njema kabisa wametoa tahadhari.

Watanzania wenzangu nyie ni mashahidi wa namna ambavyo serikali yetu chini ya mkoloni mweusi CCM inavyotushughulikia raia wake huku ikivunja katiba inayotoa uhuru wa maoni. Ushshidi wa hili ni namna ambavyo asilimia kubwa ya members wa JamiiForums tunatumia pen names au majina bandia ili kuficha utambulisho wetu kwa sababu ya kuhofia vyombo vya dola ambavyo vimekuwa vikitumia kodi zetu kutufanyia uhalifu badala ya kutimiza wajibu wake muhimu wa kikatiba na kisheria.

Wachache wetu tunafahamu kinachoendelea maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pamoja na juhudi kubwa sa serikali kudhibiti utoaji wa taarifa kwa umma. Ndugu zetu wanauawa na magaidi ambao wamejikita kaskazini mwa Msumbiji. Wahalifu hao inasemekana ni wale magaidi waliofurushwa Kibiti na Rufiji hivyo wameamua kuweka base eneo ambalo wanaamini watajiimarisha na kurudi nchini kuleta tafrani.

Tishio la ugaidi kama lilivyotolewa na ubalozi wa Marekani ni wazi kwamba hatupo salama kwa sababu taarifa ya awali ilipaswa kutolewa na vyombo vyetu na kuchukua tahadhari zote.

Tunahitaji kuona vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikitimiza wajibu wao muhimu kisheria na kikatiba kwa kutuhakikishia usalama wetu wa ndani kwa sababu uwepo wao ni muhimu kwetu na si kwa viongozi pekee.

Tufike mahala tuangalie kwa uwiano bajeti ya ulinzi wa viongozi na bajeti ya ulinzi wa umma ili kutenda yatupasayo na si kuelemea eneo moja pekee huku nchi ikiwa ktk hekaheka na matishio ya usalama

TUSIJEKUPUUZA HILI TISHIO..
Sukuma Gang wanapanga kulipua mabomu kwenye mikutano ya Chadema ili kuwatisha watu wasihudhurie mikutano hiyo na pia kumprove wrong Samia kwa kuondoa zuio haramu aliloweka yule Mhutu. Tukumbuke kuwa hawa Sukuma Gang wengi siyo Watanzania bali ni wahamiaji haramu waliojivika usukuma,bado wanawasiliana na ndugu zao ambao huko kwao wamezoea kuuana.
 
Back
Top Bottom