Hebu tujiulize undani wa hili ‘Tishio la UGAIDI’

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,337
29,140
Wengi wetu humu Tumeona, tunesikia na tumesoma tamko la Ubalozi wa Marekani kuhusu uwezekano wa kutokea shambulio la ugaidi hapa nchini.
IMG-20230125-WA0033.jpg

Tumesikia mwitikio wa jeshi la polisi kuhusu hatua wanazochukua dhidi ya tahadhari hiyo huku wakituhakikishia usalama na ulinzi. Lakini mimi nineona hapo kuna jambo la kutafakari kuhusu uwezo wetu katika usalama wa ndani ya nchi yetu sambamba na uhusiano wa dola na wananchi.

Iwapo taifa la nje linaweza kuchunguza na kupata uthibitisho wa kuwepo na tishio la usalama nchini na wakatoa tahadhari maana yake kuna kulegalega na kuzembea kwa vyombo vyetu vya ulinzi hususani espionage ya ndani ya nchi.

Serikali ya Tanzania imeeza kupitia viongozi waandamizi kuhusu uwekezaji mkubwa walioufanya katika kununua mitambo ya kudukua mawasiliano ya mitandaoni hususani ikiwalenga wahalifu wa mitandaoni. Hapo awali nilisema kuwa tambo za serikali zinathibitisha kuhusu kuingilia uhuru wa wananchi wake binafsi kwa sababu mifano ya waliochukuliwa hatua hata kufikishwa mahakamani ni wale waliotuhumiwa kutoa kauli ama maneno ya kuudhi dhidi ya watawala. Hatujawahi kuona ama kusikia wahalifu ambao wanafanikisha matukio ya kihalifu ama wanaotoa matishio ya usalama wetu wa ndani waking'amuliwa ama kuchukuliwa hatua.

Marekani kupitia taasisi zake za nje wamejijengea uwezo wa kuwez kupenya vihunzi vya usalama vya makundi ya kiuhalifu dhidi ya binadamu na wakaweza kutambua mipango yao na kwa nia njema kabisa wametoa tahadhari.

Watanzania wenzangu nyie ni mashahidi wa namna ambavyo serikali yetu chini ya mkoloni mweusi CCM inavyotushughulikia raia wake huku ikivunja katiba inayotoa uhuru wa maoni. Ushshidi wa hili ni namna ambavyo asilimia kubwa ya members wa JamiiForums tunatumia pen names au majina bandia ili kuficha utambulisho wetu kwa sababu ya kuhofia vyombo vya dola ambavyo vimekuwa vikitumia kodi zetu kutufanyia uhalifu badala ya kutimiza wajibu wake muhimu wa kikatiba na kisheria.

Wachache wetu tunafahamu kinachoendelea maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pamoja na juhudi kubwa sa serikali kudhibiti utoaji wa taarifa kwa umma. Ndugu zetu wanauawa na magaidi ambao wamejikita kaskazini mwa Msumbiji. Wahalifu hao inasemekana ni wale magaidi waliofurushwa Kibiti na Rufiji hivyo wameamua kuweka base eneo ambalo wanaamini watajiimarisha na kurudi nchini kuleta tafrani.

Tishio la ugaidi kama lilivyotolewa na ubalozi wa Marekani ni wazi kwamba hatupo salama kwa sababu taarifa ya awali ilipaswa kutolewa na vyombo vyetu na kuchukua tahadhari zote.

Tunahitaji kuona vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikitimiza wajibu wao muhimu kisheria na kikatiba kwa kutuhakikishia usalama wetu wa ndani kwa sababu uwepo wao ni muhimu kwetu na si kwa viongozi pekee.

Tufike mahala tuangalie kwa uwiano bajeti ya ulinzi wa viongozi na bajeti ya ulinzi wa umma ili kutenda yatupasayo na si kuelemea eneo moja pekee huku nchi ikiwa ktk hekaheka na matishio ya usalama

TUSIJEKUPUUZA HILI TISHIO..
 
Tishio la ugaidi kama lilivyotolewa na ubalozi wa Marekani ni wazi kwamba hatupo salama kwa
Polisi hawa hawa wewe unaamini wanachosema ?,hata panya road wao ni shida ndio useme ugaidi?

. USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima Jeshi pamoja na serikali kwa ujumla wamereconcile na Serikali ya Marekani kujua ni lini na wapi kunaweza kuwa na utishio wa Ugaidi.

Baada ya kuwasililiza, ndiyo wakaja na Statement yao. Siamini kuwa, wanaweza kukurupuka kutoa taarifa bila ya kujua haswa ni kipi Marekani inamaanisha.

Siyo Tanzania tu, Marekani imekuwa ikitoa tahadhari ya matukio ya Ugaidi katika nchi nyingi. Haimaanisha espionage imefeli. Muda mwingine hizo taarifa wanazipata kupitia taasisi hizo hizo ndani ya nchi husika.

Kutoitolea majibu taarifa ya tahadhari ya Marekani ni kuliacha taifa katika hofu. Ni lazima usafishe hali ya hewa huku harakati za kuzima majaribio hayo yakiendelea.
 
Kuna kitu Marekani kaona
Hakuna chochote Cha maaana kaona isipokuwa makomandoo wa Marekani wamemuua kiongozi wa IS hapo Somalia. Wanachofanya ni kujihami maana wanajua Islamic state Wana wafuasi sehemu nyingi na hapa ni karibu Sana na Somalia lolote linaweza kutokea.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kuna kitu Marekani kaona
US forces have killed an Islamic State leader, Bilal al-Sudani, and 10 of his operatives in northern Somalia, American officials say.
He was killed after US special forces raided a remote mountainous cave complex hoping to capture him.

"Al-Sudani was responsible for fostering the growing presence of ISIS in Africa," Defence Secretary Lloyd Austin said.

He also allegedly funded the group's activities globally, Mr Austin added.

Analysts say the fact that US troops were sent to kill or capture Sudani, rather than using a less risky drone strike, indicates his significance.

In recent years, the Islamic State group has reportedly expanded its activities into several African countries, including Mozambique and the Democratic Republic of Congo.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
....Muda mwingine hizo taarifa wanazipata kupitia taasisi hizo hizo ndani ya nchi husika....
Mkuu
Vyombo vyetu vinawajibika kikatiba na kisheria huku wahusika namba moja ni wananchi. Sasa kama unakuja hapa kuelezea uzembe wa kuvujisha taarifa muhimu kwa mashirika ya nje maana yake ni kwamba hatupo makini na hatuwajibiki ipasavyo.

Ulinzi wa nchi ni kulinda wananchi na rasilimali za nchi.

Na ukiona Marekani anatoa taarifa kwa umma ujue upo uwezekano wa taarifa kufikishwa ngazi husika na kukaendelea uwepo wa uzembe ktk ngazi hizo kama ambavyo udhibiti wa taarifa za Cabo Delgado unavyofanywa kwa manufaa ya wanaodhibiti
 
Wengi wetu humu Tumeona, tunesikia na tumesoma tamko la Ubalozi wa Marekani kuhusu uwezekano wa kutokea shambulio la ugaidi hapa nchini.
View attachment 2497876

Tumesikia mwitikio wa jeshi la polisi kuhusu hatua wanazochukua dhidi ya tahadhari hiyo huku wakituhakikishia usalama na ulinzi. Lakini mimi nineona hapo kuna jambo la kutafakari kuhusu uwezo wetu katika usalama wa ndani ya nchi yetu sambamba na uhusiano wa dola na wananchi.

Iwapo taifa la nje linaweza kuchunguza na kupata uthibitisho wa kuwepo na tishio la usalama nchini na wakatoa tahadhari maana yake kuna kulegalega na kuzembea kwa vyombo vyetu vya ulinzi hususani espionage ya ndani ya nchi.

Serikali ya Tanzania imeeza kupitia viongozi waandamizi kuhusu uwekezaji mkubwa walioufanya katika kununua mitambo ya kudukua mawasiliano ya mitandaoni hususani ikiwalenga wahalifu wa mitandaoni. Hapo awali nilisema kuwa tambo za serikali zinathibitisha kuhusu kuingilia uhuru wa wananchi wake binafsi kwa sababu mifano ya waliochukuliwa hatua hata kufikishwa mahakamani ni wale waliotuhumiwa kutoa kauli ama maneno ya kuudhi dhidi ya watawala. Hatujawahi kuona ama kusikia wahalifu ambao wanafanikisha matukio ya kihalifu ama wanaotoa matishio ya usalama wetu wa ndani waking'amuliwa ama kuchukuliwa hatua.

Marekani kupitia taasisi zake za nje wamejijengea uwezo wa kuwez kupenya vihunzi vya usalama vya makundi ya kiuhalifu dhidi ya binadamu na wakaweza kutambua mipango yao na kwa nia njema kabisa wametoa tahadhari.

Watanzania wenzangu nyie ni mashahidi wa namna ambavyo serikali yetu chini ya mkoloni mweusi CCM inavyotushughulikia raia wake huku ikivunja katiba inayotoa uhuru wa maoni. Ushshidi wa hili ni namna ambavyo asilimia kubwa ya members wa JamiiForums tunatumia pen names au majina bandia ili kuficha utambulisho wetu kwa sababu ya kuhofia vyombo vya dola ambavyo vimekuwa vikitumia kodi zetu kutufanyia uhalifu badala ya kutimiza wajibu wake muhimu wa kikatiba na kisheria.

Wachache wetu tunafahamu kinachoendelea maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pamoja na juhudi kubwa sa serikali kudhibiti utoaji wa taarifa kwa umma. Ndugu zetu wanauawa na magaidi ambao wamejikita kaskazini mwa Msumbiji. Wahalifu hao inasemekana ni wale magaidi waliofurushwa Kibiti na Rufiji hivyo wameamua kuweka base eneo ambalo wanaamini watajiimarisha na kurudi nchini kuleta tafrani.

Tishio la ugaidi kama lilivyotolewa na ubalozi wa Marekani ni wazi kwamba hatupo salama kwa sababu taarifa ya awali ilipaswa kutolewa na vyombo vyetu na kuchukua tahadhari zote.

Tunahitaji kuona vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikitimiza wajibu wao muhimu kisheria na kikatiba kwa kutuhakikishia usalama wetu wa ndani kwa sababu uwepo wao ni muhimu kwetu na si kwa viongozi pekee.

Tufike mahala tuangalie kwa uwiano bajeti ya ulinzi wa viongozi na bajeti ya ulinzi wa umma ili kutenda yatupasayo na si kuelemea eneo moja pekee huku nchi ikiwa ktk hekaheka na matishio ya usalama

TUSIJEKUPUUZA HILI TISHIO..
Hivi unaona ni hali ya kawaida watalii kutoka Arabuni kuletwa na ndege ya mizigo?
 
Juzi Marekani kauwa gaidi huko Somalia
Somalia ni divided state ambapo mpaka sasa bado hawajaweza kusimama kama Taifa moja.

Hali ya Tanzania ni amani hakuna guerilla wala civil chaos na serikali imerelax ambapo imewekeza kuchunguza wanachowaza wananchi dhidi ya viongozi
 
Hivi unaona ni hali ya kawaida watalii kutoka Arabuni kuletwa na ndege ya mizigo?
Usikute mizigo waliyokuja nayo haikupaswa kupitia security check ndo maana ikaenda kuwashushia mbugani.

Watawala hawana mahaba na Tanzania na watanzania lakini vyombo vya dola vinahakikisha wanasemwa kwa mazuri hata kama hawana hayo mazuri
 
Somalia ni divided state ambapo mpaka sasa bado hawajaweza kusimama kama Taifa moja.

Hali ya Tanzania ni amani hakuna guerilla wala civil chaos na serikali imerelax ambapo imewekeza kuchunguza wanachowaza wananchi dhidi ya viongozi
Wakati Ubalozi wa US unalipuliwa pale Selender bridge ulikuwa umeshazaliwa?
 
Kuna kitu Marekani kaona
Kuna dhania 2:-
1. Marekani anajua kuwa mtandao wa ugaidi unaofungamana na Al Sudani aliyeuawa Somalia uko hadi pande hizi. Hivyo anatahadharisha akimaanisha wafuasi wake wanaweza kupanga kulipa kisasi
baada ya mauaji hayo.
2. Uhakiki wa mali za bakwata. Mosi, zoezi haliwafurahisha wanaohodhi mali hizo. Pili, bakwata inajitenga na project zinazotumia mgongo wa dini kufadhili ugaidi. Hili nalo hawatalipenda. Hapa ndo inakuja hofu kuwa hata misikiti haiko salaam.
 
Bakwata tena?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom