Haya yakifanyika uhalifu utaisha, panya road watakwisha na raia watakuwa wanalala milango wazi hadi asubuhi

Nakumbuka bamdogo Kuveta aliuwawa siku ya tatu tu akiwa ametoka jela. Akiwa ameenda kulala kwa demu wake, siku hiyo ghafla usiku walivamiwa na kundi la watu zaidi ya 50 wakiwemo askari wenye silaha na sungu sungu wenye mapanga na kuanza kumshambulia. Maiti yake tulikuta ikiwa na majeraha makubwa kwenye maungio ya mikono yake, kifuani na kichwani.
Nimeguswa!. Very touching story.
Sijapenda jinsi starring alivyo uwawa bila kosa lolote!.
Wale wote walio husika kumuua kamanda huyu bila kosa lolote, karma inawahusu.

RIP Kuveta, Kamanda wa Commando Yosso.
 P
 
Yes, ni kama ulivyosema ni alikuwa!. Mtu ametoka jela juzi, hajafanya uhalifu wowote, yuko kwa demu wake, watu unamwingilia usiku kumvamia, kumkatakata mapanga, kumuua na kumjeruhi demu wake!. Wahusika wote karma itawahusu.
P
Kutoka jela hakumaniishi aliacha ujambazi! Tena awamu hizo ililikuwa tabu sana kutofautisha rushwa na takirima
 
Kutoka jela hakumaniishi aliacha ujambazi! Tena awamu hizo ililikuwa tabu sana kutofautisha rushwa na takirima
People changes, maadam alitoka jela na hakufanya uhalifu wowote, then, there is no any justified cause ya kumuua!.
Na kwa tukio hili lilitokea siku nyingi, wahisika wote kila mmoja ameisha lipwa na karma, kwa kadri ushiriki wake katika dhambi ya mauaji ya mtu asiye na hatia.
P
 
People changes, maadam alitoka jela na hakufanya uhalifu wowote, then, there is no any justified cause ya kumuua!.
Na kwa tukio hili lilitokea siku nyingi, wahisika wote kila mmoja ameisha lipwa na karma, kwa kadri ushiriki wake katika dhambi ya mauaji ya mtu asiye na hatia.
P
Kumbuka jela zetu hapa ni mara chache sana kumrekebisha mtu maana mara nyingi watu wanafungwa kwa kukomoana!
Ukiona mtu kamaliza kifungo chake na akarudi mtaani akatulia jua sana sana huyo alibambikiwa kesi! Mqenye tabia yake ya wizi na ujambazi hawezi kurekebishwa na mageteza zetu!
Mageteza zetu ni sehemu ya kwenda kuumia sio kunifunza!
 
Wamrudishe Mrema kuwa mshauri
Hakika mkuu, Mrema anatakiwa ashirikishwe kama mshauri kwenye mikutano yao ya ulinzi na usalama, huko wilayani Temeke, Ilala, Ubungo, Kinondoni nk. Nina imani amani itapatikana upya, na nchi itakuwa salama. Watanzania iombeni serikali irudishe OPARATION MREMA, bila hivyo hakuna uhalifu utakaoisha.
 
Na mbaya zaidi ni watoto wetu na tumawajua ila tunaoneana aibu kuwataja na mwisho wa siku wanatufedhehesha tu
Ya ni kweli kabisa hawa ni watoto wetu wenyewe. Lakini katika jamii kuna watu ambao hawana watoto wa aina hiyo, na wanachukizwa zaidi na matendo hayo. Ila ndo hivyo hawana pa kusemea kwa kuogopa usalama wao. Sasa ikianzishwa oparation kama ile ya Mrema ni wewe mwenyewe kwenda kimya kimya katika ofisi ya waziri wa mambo ya ndani (enzi hizo Mrema) unaacha kikaratasi tu cha jina au majina ya muhusika, na anuani yake afu unaondoka. Wazee wa kazi wanaangalia rekodi ya jina la muhusika au wanatuma vijana wao kimya kimya kuja kufanya upelelezi eneo hilo bila ww uliepekea jina kuhusishwa. Wakishajiridhisha tu basi usiku unaofata kazi inaanza, na watapumzika wakishamaliza lengo lao, afu ndugu/wazazi mnakwenda kubeba mzigo wenu mnazika. OPARATION MREMA inahitajika haraka iwezekanavyo.
 
Nimeguswa!. Very touching story.
Sijapenda jinsi starring alivyo uwawa bila kosa lolote!.
Wale wote walio husika kumuua kamanda huyu bila kosa lolote, karma inawahusu.

RIP Kuveta, Kamanda wa Commando Yosso.
 P
Kweli kabisa mkuu it was very sad wahusika wale wa OPARATION MREMA kuchukua uhai wa baba yetu mdogo, lakini kwa kipindi hicho hizi oparation zilikuwa haziangalii kama ulihusika na tukio la uhalifu kwa kipindi hicho au haukuhusika. Lengo lilikuwa ni kutokomeza vijana wote waliokuwa wanahusika na uhalifu mbali mbali miaka hiyo.
 
😂😂😂😂😂
Hahaha 😂🤣🤣 mkuu huyo Kuveta hakuwa wa kufanyiwa masihara hata sekunde 1. Iwe jela, makundini au mtaani, watu wote walifyata mbele yake. Nina hakika mkuu Mshana Jr , Pascal Mayalla na wengineo wengi wa miaka hiyo itakuwa aidha kama hawakuwahi kumuona kwa macho basi walikuwa wanamsikia mitaani.
 
Back
Top Bottom