JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Ikidaiwa kuwa wahusika wanaofanya hivyo wanajitambulisha kuwa wanafanya Ulinzi Shirikishi.
Wamedai kuwa ukikutana nao hujitambusha kama Watu wa Usalama na baada ya hapo hutekeleza uovu huo kwa kukutolea mapanga, visu, nondo kisha kufanya uhalifu huo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa mtaa huo ambao wawili walikataa kutotajwa kwa majina, wamedai kumekuwepo kwa vitendo hivyo katika eneo Hilo ambalo ni karibu zaidi na Kituo cha Polisi Kawe.
Wadai hivi karibu mmoja wa Askari wa Jeshi anadaiwa kukabwa akiwa na mpenzi wake katika eneo hilo jambo ambalo linaongeza wasiwasi miongoni mwao.
Williams Nashoni ni mmoja wa mkazi wa mtaa huo amesema kuwa kumekuwepo kwa vitendo hivyo kwa kiasi kubwa japo hivi karibuni vimepungua kutokana na baadhi ya walinzi wa Mchungaji Mwamposa kuongeza walinzi, hata hivyo akidai bado jitihada zinatakiwa kuongezwa kutokana na walinzi hao kutokudhi mahitaji.
Nashoni amesema kinachowaumiza ni vitendo hivyo kutokea eneo ambalo si mbali na Kituo cha Polisi Kawe huku akiwaomba wahusika kujitathimini.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kinondoni, ACP Mtatiro Kitinkwi amesema wamejipanga kuendeleza kudumisha ulinzi na usalama eneo nzima la mkoa wa Kipolisi ikiwemo Kawe na Tanganyika Packers.
Amedai kuelekea Mwisho wa mwaka kuna tukio la mkesha eneo la Tanganyika Packers na wao kama Jeshi wamejipanga kuongeza ulinzi na usalama ili kuhakikisha hakuna vitendo viovu vinavyojitokeza hata kwa bahati mbaya.
Amewaomba Wananchi kuendelea kutoa taarifa zote za uhalifu katika mkoa huo ili kuwarahisishia kazi na kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa.
Pia soma = IGP Wambura na PT yake wamelishindwa Pori Hatari kwa Uhalifu Tanganyika Packers Kawe!
> Serikali ya Mtaa Kawe: Kweli kuna kundi la Wahalifu wanatumia kivuli cha Ulinzi Shirikishi, wanatuchanganya sana