Napoongelea maridhiano kati ya Wananchi na Serikali naomba nieleweke kuwa, simaanishi aina Ile ya maridhiano kati ya CCM na ACT kule visiwani,
Maridhiano nayoongelea Si yake ya Mh Mbowe na kinana na team yake ambayo yaliendelea zaidi ya mwaka huku tukiendelea kukandamizwa na TOZO na Mfumuko wa bidhaa tukipewa sababu hafifu,
Maridhiano nibayoongelea yalenge yafuatayo;
1. RUSHWA iwe historia
Hatufurahishwi kusikia Majina ya viongozi wastaafu yakionekana kujirudia kijirithisha madaraka.
Hatutaki kusikia madawa hospitalini yakigawiwa Kwa upendeleo.
Mbolea Kwa wakulima ya ruzuku itufikie Kwa wakati bila Kutoa RUSHWA. Nk nk nk
2. Tunataka Sanduku la kura lirudi mahala pake
Tumechoka kusikia idadi ya wapiga kura kituoni ni 200 Kwa mfano, lakini katika matokeo zikihesabiwa tunapata idadi jumla ikiongezea na kufikia 250.
Wananchi tunajiuliza, hizo kura 50 Huwa zinaingizwa na maruhani ndani ya ballot box?
Wananchi pia tunataka wagombea tunaowataka ndio Majina Yao yarudishwe, hatutaki kuletewa wagombea wa mfukoni.
3. Umeme, maji na huduma za JAMII za uhakika
Hatutaki blaa blaa, pesa za kulipa bill ya umeme tunazo lakini umeme hamna,
Pesa ya kulipa bill ya maji IPO lakini maji hayatoki bombani!!
Tukilipia vifurushi vya data mitandaoni hatutaki kusikia hamna mtandao, hayatuhusu.
3. Huduma za AFYA
Maridhiano tuyatakayo ni dawa ziwepo za kutosha mahispitalini, Kumwambia mgonjwa kuwa hakuna madawa Hilo halimuhusu.
4. Miundombinu ya barabara
Maridhiano tuyatakayo ni barabara zijengwe za kutosha zitakazohimili msimu mzima.
Hatutaki kusikia mawasiliano ya barabara yakikatika na kutuzuia kufika tupatakapo.
5. Bima za AFYA
Maridhiano kati ya mama Serikali na mama mjamzito yafanyike Ili ijulikane mtoto atakayezaliwa anastahili matibabu ya bima Bure au la!!
Si sawa watoto wa maskini wazuiwe kupata bima wakati viongozi wakitibiwa Bure nje ya nchi Kwa Kodi za sirikali.
6. KILIMO
Maridhiano yafanyike, Kila Kijiji kikopeshwe tractors za KILIMO kupitia Benki ya KILIMO Ili kuepuka KILIMO Cha jembe la mkono.
7. ELIMU
Maridhiano yafanyike kuhakikisha chakula Bure mashuleni kinarudishwa kama enzi za Mwl Nyerere.
Walimu wapewe overtime wanaposahihisha mitihani au kutunga mitihani nje ya muda wa KAZI.
8. Madini
Maridhiano yafanyike wananchi tupate 50/50 katika mgao wa madini yetu.
Wazawa wakopeshwe na wasaidiwe zana za kisasa za kuchimba madini bila kuharibu mazingira.
9. UTUMISHI wa Umma
Maadili ya viongozi yarudi mahala pake, watumishi wa umma waache kufanya biashara ndani ya Serikali. Hili linahitaji maridhiano.
Ndugu Mwananchi unakaribishwa kuongeza eneo ambalo ungependa maridhiano yafanyike kati yetu na sirikali Ili Nchi ipumue.
Angalizo: Wananchi hatufurahishwi na TABIA ya viongozi Wachache wa Vyama vya siasa kujifungia sirini kujadili issues tusozijua Wala kushirikishwa, maridhiano yanatakiwa yawe ya WAZI peupe, sababu hii ni Nchi yetu sote, Nchi hii si ya CCM, CHADEMA na ACT pekee.
ASALI ni tamu, hivyo ni muhimu wote turambe Kwa haki, Si Wachache Kwa RUSHWA.
Karibu🙏. Amen
Itaendelea......!!