Maridhiano ya CCM na CHADEMA yangesimamiwa na Viongozi wa Dini au Rais Mstaafu kutoka nje ya Tanzania

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,304
Wanajamii nawasalimu.

Kumekuwa na Maridhiano baina ya vyama vikubwa Nchini yaani CCM na CHADEMA. Msingi wa Maridhiano hayo ni mambo yaliyojitokeza wakati wa utawala katili wa awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli. Katika kipindi hicho CHADEMA kilikumbwa na utitiri wa majanga ikiwa ni pamoja na kupigwa risasi kwa kiongozi wake, viongozi kukamatwa na kufunguliwa kesi mbalimbali zikiwemo za uhujumu uchumi, ugaidi, mauaji na kutakatisha fedha. Kesi ambazo zilifunguliwa wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020.

Kesi hizo zote zilifunguliwa katikati ya uchaguzi ili kuwazuia wagombea wa CHADEMA wasigombee na kusababisha wanachama na viongozi wengi kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu. Pia kulikuwa na suala la ruzuku kwa chama kuzuiliwa.

Matukio yote hayo baada ya kifo cha Hayati Magufuli, Rais Samia alikubali kufanya Maridhiano na CHADEMA.
Sasa najiuliza;
1. Nani anayasimamia hayo Maridhiano?
2. Je, Maridhiano hayo yapo Kisheria au Kuaminiana tu?
3. Je, upande mmoja ukikiuka Maridhiano itakuwaje?
4. Je, Maridhiano hayo wananchi wanayajua au watajulishwa?

Binafsi niliamini yangefanyika kisheria ili kusitokee upande mmoja ukakiuka na pia yangesimamiwa na viongozi wa dini au mtu kutoka nje ya Tanzania (Rais Mstaafu).

Wasiwasi wangu ni kuwa kuna upande unaweza kutokutekeleza maazimio yatakayofikiwa.
 
Back
Top Bottom