Haya maneno ni kweli kwamba ndio maneno ya mwisho kusemwa na Magufuli?

Aliekwambia kifo cha RAIS wa Nchi kinatangazwa hovyo hovyo ni Nani?
Huo ni utaratibu(PROTOCOLS) wa wapi?

Unao Uhuru mkubwa wa kutangaza hovyo kifo cha rais mstaafu na viongoz wengine lakini sio Rais alie fia madarakani

Hivi wewe MZIMA kweli shekhe?
Sasa CDF Mabeyo amuweke Nani tena wakat huo yeye ndie mkuu wa Majeshi? Nchi inakua chini ya JESHI sio yeye aweke mtu wake kama ulivyosema

Khaaa Watu wengine bwana basi tuu
 
Haya meneno yanatrend sana mtandaoni kwamba ndio maneno ya mwisho ambayo magufuli alimwambia Pengo hospitalini dakika zake za mwisho kabla hajaaga dunia,Maneno yenyewe ni haya.

"Mheshimiwa Pengo na baba Paroko, Mungu ni mkubwa kuliko chochote,tumtangulize Mungu kwa kila jambo.Nchi yetu inahitaji viongozi wacha Mungu,watakao kubali kufa na kujitoa sadaka kwa faida ya wengi.

"Nilitamani kuiona Tanzania ya ndoto yetu,Tanzania mpya lakini kwa hali yangu sita ishuhudia.

Natoa wito wangu wa mwisho kwa watanzania kuungana kupinga rushwa na ufisadi yaani, endelezeni mapambano msirudi nyuma!!

Mheshimiwa Cardinal Pengo na baba paroko niombeeni kitubio nilale kwa matumaini,naipenda nchi yangu,niliahidi kuilinda mpaka kufa"

Haya maneno ni ya kweli? Kuna mahali Pengo kanukuliwa akiyasema?..
Hayo ni maneno ya kutungwa tuu

Kama Majaliwa aliweza kudanganya msikitikini mchana kweupeeeee, atashindwa kutunga maneno kama hyo ?
 
" Niliwasiliana na Hayati Rais Dkt. Magufuli Siku tano tu kabla ya Kifo chake na akiniambia tuendelee Kuchapa Kazi, tuiendeleze Tanzania, ila akasisitiza sana tusiogope Kukisema Chama chetu cha CCM pale Kikikosea "

" Ni matumaini yangu makubwa Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan atayaendeleza yote na hatotusahau Sisi Wakazi wa Geita na hata Mwanza ambao Kiukweli ni Masikini mno hadi hivi leo "

" Hata hivyo nimtahadharishe tu Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ajiepushe na Makundi ndani ya CCM ambayo kiukweli bado yapo na yamejaa Unafiki, Majungu na Uzandiki tupu. Akitaka msaada Wetu tupo na tutamsaidia asiogope na tuna Imani nae Kubwa tu
"

Hizi Nukuu zote All - Rounder nimezisikia akisema alipokuwa akihojiwa na Mtangazaji wa TBC Taifa mara baada tu ya Mwili wa Hayati Rais Dkt. Magufuli kuwasili Geita mida ya Saa Saba ( 7 ) Mchana leo. Najua kuna wengine pia mlimsikia vyema tu

Hata hivyo Kupitia tu hizi Kauli Tatu Kuu nilizoziweka hapa nimejikuta napata Maswali Fikirishi mengi sana ila pia nimeanza Kunusa Jambo kuwa kuna Fukuto Kubwa lilikuwa likiendelea na japo Binadamu tunasema Kifo hupangwa na Mwenyezi Mungu lakini naanza Kuhisi huenda wengine Wameondoka ( Wametuacha ) kwa ' Mipango Maalum na ya Siri kwa Mafia Wakuu ndani ya Chama ' ambayo ilikamilika rasmi tarehe 17 March, 2021.
 
Back
Top Bottom