Kijana wangu bado mapema sana kukata tamaa 24yrs wewe bado kinda Sana na huo ndio umefika wakat wako wa kustruggle badala ya kukaza wewe ndo unaanza kukata tamaa?why
Jikumbuke umezaliwa wa kiume upambane,usisubiri tu michongo ije..zama posta kapige vibarua vya zege huku unaendelea kuitafutia fani yako pa kuiweka ,usisubiri siku iishe bila kuingiza pesa yoyote.Kuna wenzako Wana matatzo makubwa kuliko wewe..hivi huwaoni walemavu na ombaomba ,tazama wagonjwa na wengine walio na mattzo kuliko wewe.tatiz lako unaangalia walio juu yako Kisha unajikatia tamaa!
Tumepitia mengi kijana hakuna mafanikio kwa kulalamika tu.
Tatiz lako ulikariri ukitoka tu veta utapata kazi ya fani yako kumbe mtaani hapako hivyo! Tafuta kibarua chochote mdogomdogo utatoboa kwa rizki yako bado ipo.
Kaza kijana wangu,asubuhi ikifika amka nenda mjini katafute vibarua hata vya ujenzi.kesho usisubiri chai nyumbani kwa ndugu safar yako ya maisha itaanzia hapo dogo.
Amka,pambana
Usichanganywe na vijaa wenzio wanaovaa pamba Kali na kumiliki mademu wakali.