Haya anayofanya Freeman Mbowe ni unafiki mkubwa kuwahi kutokea. Angefanya Zitto Kabwe wa ACT moto ungewaka

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Kwakweli nimechoka na siasa za bongo.

Miezi michache iliyopita Zitto Kabwe alikuwa anashambuliwa Kila Kona kwa sababu ya ruzuku. Wakamwita msaliti na matusi chungu nzima. Leo Chadema chini ya Freeman Mbowe wamechukua ruzuku na wamekausha kimyaaa. Unafiki!

Miezi michache iliyopita walimshambulia Zitto kila kona kwa kukubali kufanya kazi ya pamoja katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakamwita mnafiki akayaoga matusi mazito kabisa. Leo mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa BAWACHA ni Rais Samia. Duu, huu ndio upinzani wetu.

Joe Biden wa democratic anakuwa mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa Republican. Haijawahi tokea ni Chadema tu ndio utayaona haya maajabu. Wanachukua pesa wanasahau na malengo makuu ya upinzani.

Hongera Zitto Kabwe sasa tumewajua wanafiki halisi wa mageuzi ya Tanzania.
 
Sema Mbowe kamuwahi tu Zito kwenye hili. Zito angepata hii fursa asingeiacha. Mbowe mtoto wa mjini tena Posta Daslam
Yaaani inamaana chadema nzimaa hakuna mgeni rasmi?. Kwa kuwa mumeanza kutambuakazi nzuri ya mama SAMIA, Sasa tunawaomba Kwa UMOJA wao chadema na CCM tumpitishe raisi mama SAMIA bila kupingwaa 2025. Chadema+CCM OOOHYEEEEE
 
Back
Top Bottom