Hawezi kunioa kwasababu hana "MSIMAMO WA MAISHA"

valid statement

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
2,851
870
Habari zenu wana MMU, Siku hizi kumekuwa na msemo kwa wasichana wengi kuwa hawezi olewa na mtu ambaye hana MSIMAMO WA MAISHA.
Hii imekuwa kama kaugonjwa kapya ka wasichana kukimbilia wanaume wenye kipato cha juu, na huwabwaga maboifrend au wachumba zao wenye kipato dhaifu kwa kusema HAWANA MSIMAMO WA MAISHA.
Nimeona wanaume wengi wakimwaga na kisingizio ni msimamo wa maisha.
Ukiwauliza wasichana msimamo wa maisha wanao usema ni upi? Watakwambia, nataka mwanaume wa kunioa awe na KAZI NZURI, awe na NYUMBA na awe na GARI.
Hivi kama huna KAZI NZURI, GARI na NYUMBA tunasema huna msimamo wa maisha?
Wasichana wengi sana wamekuwa hawana mapenzi ya kweli bali wanatafuta maslahi. Ukiwauliza mwanaume wa kukuoa unataka awe na SIFA zipi, ntaanza na kukwambia, awe na msimamo wa maisha, na anipende na kunijali.
Leo unakuwa na mwalimu, unaona hana msimamo wa maisha kwa sababu umetongozwa na daktari, na daktari nae unamwacha ukikutana na mhasibu. Jipangeni sawa sawa, msitukatae eti sababu umepata mwenye gari, nyumba na kipato cha juu. Nimewasilisha....!!
 
Umenigusa mkuu 100% yalitokea kwangu ingawa sasa afadhali nina Kamsimamo
yaani si msimamo kamili ni KAMSIMAMO............ Naapa yaani ni hivyo hivyo
imeniathiri mpaka sitamani tena kuoa!
 
Pole mdau,,,ni mambo tu kwenye maisha
Umenigusa mkuu 100% yalitokea kwangu ingawa sasa afadhali nina Kamsimamo
yaani si msimamo kamili ni KAMSIMAMO............ Naapa yaani ni hivyo hivyo
imeniathiri mpaka sitamani tena kuoa!
 
na sisi tukitaka kuoa basi tutafute mwanamke mwenye msimamo wa maisha!
 
Habari zenu wana MMU, Siku hizi kumekuwa na msemo kwa wasichana wengi kuwa hawezi olewa na mtu ambaye hana MSIMAMO WA MAISHA.
Hii imekuwa kama kaugonjwa kapya ka wasichana kukimbilia wanaume wenye kipato cha juu, na huwabwaga maboifrend au wachumba zao wenye kipato dhaifu kwa kusema HAWANA MSIMAMO WA MAISHA.
Nimeona wanaume wengi wakimwaga na kisingizio ni msimamo wa maisha.
Ukiwauliza wasichana msimamo wa maisha wanao usema ni upi? Watakwambia, nataka mwanaume wa kunioa awe na KAZI NZURI, awe na NYUMBA na awe na GARI.
Hivi kama huna KAZI NZURI, GARI na NYUMBA tunasema huna msimamo wa maisha?
Wasichana wengi sana wamekuwa hawana mapenzi ya kweli bali wanatafuta maslahi. Ukiwauliza mwanaume wa kukuoa unataka awe na SIFA zipi, ntaanza na kukwambia, awe na msimamo wa maisha, na anipende na kunijali.
Leo unakuwa na mwalimu, unaona hana msimamo wa maisha kwa sababu umetongozwa na daktari, na daktari nae unamwacha ukikutana na mhasibu. Jipangeni sawa sawa, msitukatae eti sababu umepata mwenye gari, nyumba na kipato cha juu. Nimewasilisha....!!

"Valid statement" kweli statement zako ziko valid.. basi kama yamekukuta hayo na yako valid kwako, pole!!.. kuachwa kunauma..!!.. nenda mikumi.. wao hawajali cha daktari wala mwalimu.. unajichotea tu.. tena ukisema wewe dereva basi utajaza fuso...
 
"Valid statement" kweli statement zako ziko valid.. basi kama yamekukuta hayo yako valid kwako pole.. kuachwa kunauma..!!.. nenda mikumi.. wao hawajali cha daktari wala mwalimu.. unajichotea tu.. tena ukisema wewe dereva basi utajaza fuso...
Fafanua Mkuu, mi sijaelewa.
 
Mwanamke akikupenda ni balaa
Hata ukimwambia una mtu atasubiri hadi kipyenga cha mwisho, na akidhibitisha atalia na siku inayo fuata atasahau pamoja na kuwa amesubiri miaka

Nirahisi kumpiga kibuti mwanamke uliyempenda kwanza kuliko mwanamke aliye kupenda kwanza​

Last edited by tabutupu; Today at 09:57.

HII THREAD MLIVOICHANGIA WANAUME NASHINDWA KUWAELEWA MNATAKA NINI? MKIPENDWA MAKELELE WATU WAKICHUNGULIA WALET MAYOWE VP?
USHAMBA TU WA MAPENZI UNAWASUMBUA
 
Be gentle Love... Sio wanaume woote....
 
Msimamo wa maisha au mwelekeo wa maisha?

MSIMAMO Wa Maisha, eti uwe na gari, nyumba na kazi nzuri... Msimamo gani hapo zaidi ya kutafuta tu maisha mazuri kwa kutembelea nyota kama MAMAJUSI!
Utadhani ana garantii kuwa huyo mwanaume hatafanikiwa bana...girls bana aaarrhhggh
 
Kama huna msimamo ya nini kuendelea nae? Chapa lapa utakutana asiye na msimamo mwenzio mtaishi. acheni kulalamika nyie wanaume.
 
Back
Top Bottom