valid statement
JF-Expert Member
- Sep 18, 2011
- 2,851
- 868
Habari zenu wana MMU, Siku hizi kumekuwa na msemo kwa wasichana wengi kuwa hawezi olewa na mtu ambaye hana MSIMAMO WA MAISHA.
Hii imekuwa kama kaugonjwa kapya ka wasichana kukimbilia wanaume wenye kipato cha juu, na huwabwaga maboifrend au wachumba zao wenye kipato dhaifu kwa kusema HAWANA MSIMAMO WA MAISHA.
Nimeona wanaume wengi wakimwaga na kisingizio ni msimamo wa maisha.
Ukiwauliza wasichana msimamo wa maisha wanao usema ni upi? Watakwambia, nataka mwanaume wa kunioa awe na KAZI NZURI, awe na NYUMBA na awe na GARI.
Hivi kama huna KAZI NZURI, GARI na NYUMBA tunasema huna msimamo wa maisha?
Wasichana wengi sana wamekuwa hawana mapenzi ya kweli bali wanatafuta maslahi. Ukiwauliza mwanaume wa kukuoa unataka awe na SIFA zipi, ntaanza na kukwambia, awe na msimamo wa maisha, na anipende na kunijali.
Leo unakuwa na mwalimu, unaona hana msimamo wa maisha kwa sababu umetongozwa na daktari, na daktari nae unamwacha ukikutana na mhasibu. Jipangeni sawa sawa, msitukatae eti sababu umepata mwenye gari, nyumba na kipato cha juu. Nimewasilisha....!!