Kafiti
JF-Expert Member
- Mar 27, 2011
- 537
- 220
Habari wanajamvi,
Nimetimba tena kwenye jukwaa letu pendwa nikihitaji ufafanuzi wa maneno haya, naona tumekuwa tukiyatumia sana kimatamshi ila yamekuwa yakinitatiza kimaandishi.
Kuna neno huwa tunalitamka kuafiki kuwa kilichozungumzwa ni sahihi, watu husema "Ewalaa" Je hivi ndivyo liwavyoandikwa au huwa linaandikwaje. Ni Ewala, Hewala, Ewalaa, Hewalaa au yote siyo sahihi.
Pili kuna hili neno "Hawala" mtaani huwa tunalitumia kumwakilisha mtu mwenye mahusiano ya kimapenzi na mtu fulani yasiyo rasmi. Sasa je hili neno ni tungo tata au ni neno la kawaida. Na mtu anaposema "Hawala ya fedha" anamaanisha nini.
Nawasilisha.