Hawa panya wa kisasa mbona balaa

Hawa panya wa kisasa mbona balaa

Umuofia kwenu, kwa takribani miezi minne sasa nilishuhudia mbegu mpya kabisa ya panya nyumbani kwangu.

Panya hao wana muonekano tofauti na hawa wetu na cha ajabu kabisa wanawawinda panya wale wa asili na kuwaua kabisa.

Mdomo wao ni mrefu kama nguruwe hivi, na ajabu yao pia hawa panya hata paka hawali, ukiwategea sumu hawali, Wana mwili ambao una mijongeo ya ajabu ,nasemea hili kwa sababu panya hawa hata pawe na tundu dogo kiasi gani atajiminya

Na kupita kabisa, mbaya kuliko wanazaliana kama utitiri yani

Nimetumia Indocid yani naona kama ilikua cow bell kwao, nikatumia masumu ya mitaani mpaka madukani bila bila.

Nikajitahidi kuzidisha usafi na kutokuacha uchafu kwa namna yoyote hapo wakaanza kula gypsum sasa.

Wakuu kama kuna mtu anafahamu ile gundi maalum ipo kwenye tube kama ya baiskeli naomba aniambie

Ntaipata wapi mana najua ile kidogo ni suluhisho nje ya hapo sijui na panya hawa sijafanikiwa kupata picha ila usiombee🥹🥹🥹
Kweli hata mimi nilishamuua mmoja ofisini, nikashangaa alivyo. Mdomo wake mrefu na meno makali na magumu. Ukimpelekea mguu anakuuma na atajutiboa. Huyu anashambulia pale anaposhambuliwa
 
Hawa panya wa kawaida
Wapo vijiji
Sisi kwetu tunawaita panya msusu

Akiingia kwenye begi la nguo anaweza toboa na kichana chana zote

Ni waharibifu tu

Ukimuua mmoja usimtupe wenzake wakiona mzoga watahama wenyewe
 
Umuofia kwenu, kwa takribani miezi minne sasa nilishuhudia mbegu mpya kabisa ya panya nyumbani kwangu.

Panya hao wana muonekano tofauti na hawa wetu na cha ajabu kabisa wanawawinda panya wale wa asili na kuwaua kabisa.

Mdomo wao ni mrefu kama nguruwe hivi, na ajabu yao pia hawa panya hata paka hawali, ukiwategea sumu hawali, Wana mwili ambao una mijongeo ya ajabu ,nasemea hili kwa sababu panya hawa hata pawe na tundu dogo kiasi gani atajiminya

Na kupita kabisa, mbaya kuliko wanazaliana kama utitiri yani

Nimetumia Indocid yani naona kama ilikua cow bell kwao, nikatumia masumu ya mitaani mpaka madukani bila bila.

Nikajitahidi kuzidisha usafi na kutokuacha uchafu kwa namna yoyote hapo wakaanza kula gypsum sasa.

Wakuu kama kuna mtu anafahamu ile gundi maalum ipo kwenye tube kama ya baiskeli naomba aniambie

Ntaipata wapi mana najua ile kidogo ni suluhisho nje ya hapo sijui na panya hawa sijafanikiwa kupata picha ila usiombee🥹🥹🥹
Dah hawa panya ni hatari sana,hapa kwangu Kuna panya wawili wasumbufu balaa.....
Mitego yote wanakwepa nakimbizana nao kama tunacheza kidali pooo..
Wanachokera zaidi mara wanawasha redio,tv na ukiweka simu kwenye chaji utawakuta wanacheza games!!!
 
Upo sahihi hawa panya wakifika nyumbani kwako tu basi panya wa asili wanapotea tena hao panya hata paka nanashindwa kuwala akiwala anaweza hata kutapika hivyo paka wana waacha tu bila ya kuwa fanya chakula..kitu cha kushangaza viongozi wa nchi na vyombo usika vipo kimya kuhusu aina hii mpya ya panya .....nchi imejaa viongozi wapumbavu sana hii ...tena hawa panya sijui waliletwa na akina mwamposa ili kuvutia utapeli wao makanisani maana kwa mara ya kwanza niliwaona kwenye tv vipindi vya dini waumini wakisema ni mambo ya kichawi baada ya kutumia maji ya upako na mafuta ya upako ...nina mashaka makubwa kama siyo viongozi wa dini ya kikristo ndiyo wameingiza aina hii ya panya nchini
Hadi panya serikali ?
 
Kiruka njia, waharibifu hatari...kila kitu wanakula.
Tafuta mtego wa kuwabana. Yale magundi sikuhizi hayana nguvu yyt, akinasa anajinasua
 
Back
Top Bottom