Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Akilihuru

JF-Expert Member
May 20, 2022
1,444
2,833
Za asubuhi wakuu, leo nakuja na makala ya watu maarufu duniani, ambao wameacha alama kubwa katika tasnia zao na mpaka leo hakuna alietokea kuziba mapengo yao.

1) Mohammedi Ali
Huyu ni bingwa, mbabe na mtemi wa masumbwi ulimwenguni kote. Mohammed Ali ambae alizaliwa 17 January 1942, huko Louisville, Kentucky Marekani na kufariki 3 June 2016, huko Scottsdale, Arizona Marekani. Alikuwa ni bondia wa pekee kuufanya mchezo huo uwe na wapenzi na waangaliaji wengi ulimwenguni.

Licha ya kwamba mchezo huo ulikuwepo maelfu ya miaka kabla ya ujio wake Ali, lkn ni yeye ndio aliefanya watu waanze kuupenda zaidi mchezo huo na kuchukua nafasi ya pili kwa kupendwa duniani baada ya mchezo wa mpira wa miguu. Ali ambae alikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki ulingo, kukwepa ngumi, na mwepesi wa kupiga ngumi za haraka haraka. Lakini pia alikuwa na mbinu nyingi za kuweza kumchosha na kummaliza kbs mpinzani wake wakati wowote alioutaka yeye ulingoni.

Ali alikuwa na uwezo wa kumsogezea mpinzani sura, lkn utashangaa hadi round nzima inaisha bila mpinzan wake kufanikiwa kumpiga ngumi hata 1 tu usoni (kama tuonavyo pichani) sometimes unakuta mpinzani wake anarusha ngumi (kota) na kuanguka mwenyewe, huku Ali akimtizama kwa dharau πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£

Pamoja na yote lkn kama ilivyo michezo mingine na yey kuna muda alikuwa anapoteza baadhi ya mapambano pia, aidha kwa kutokana na mchoko wa mazoezi makali anayokuwa amefanya kabla ya pambano nk. Toka Ali alipostaafu ngumi mpaka kifo chake, hakuna bondia ambae ashawahi kufikia rekodi ya upiganaji wake na vituko vyake awapo ulingoni na nje ya ulingo.

Mabondia wengi kama kina Mike Tyson, Evander, Lenox Lewis na wengineo walikuwa wanakwenda kumuona na kupata mbinu mbali mbali za kupigana ulingoni kupitia mfalme huyo wa ngumi ulimwenguni. Huyu ndio Mohammed Ali alieacha alama kubwa ktk mchezo huo maarufu wa ngumi duniani. Hakuna na hatotokea Mohammed Ali mungine, Never.
Mungu ailaze roho ya huyu Legend mahali pema peponi.

hi-res-a97e1973028243210735b20be544f484_crop_exact.jpg


2) Bob Marley
Bob Marley alizaliwa 6 Feb 1945, huko Nine Mile, Jamaica, na kufariki 11 May 1981, huko Florida Marekani.

Alipozaliwa aliukuta mzikiwa reggae ukiwa ulimwenguni miaka na miaka. Lkn kwa kipaji chake na uwezo wake akaanza kuleta mabadiliko makubwa katika mziki huo, hadi kufikia hatua ya kusikilizwa na viongozi wakubwa wa nchi mbali mbali. Japo kulikuwa na waimbaji wengine wakubwa kama kina Peter Tosh, Burn Spear nk, lkn ni yeye Bob Marley ndio aliefanya reggae ipendwe na walio wengi. Hadi anakufa Bob Marley aliacha muziki huo ukiwa na mamilioni ya wasikilizaji ulimwenguni.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

348431656.jpg


3) Bruce Lee
Bruce Lee alizaliwa 27 Nov 1940, huko San Francisco, California Marekani na kufariki 20 July 1973 huko Kow loon Tong, Hong Kong.

Bruce alizaliwa na kuukuta mchezo wa kung fu au karate ulimwenguni. Lakini kwa kipaji alichozaliwa nacho, alianza kuleta mabadiliko makubwa kwenye mchezo huo hadi kushawishi mamilioni ya watu ulimwenguni kuupenda na kuanza kuufuatilia mchezo huu. Bruce alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na hisia za adui na kujua ni wapi atapopiga lazima adui atakaa tu hata awe na mwili kama jumba.

Ikafika kipindi watu wakamshauri ajiunge kwenye tasnia ya uigizaji ili kuwavutia watu zaidi kuupenda mchezo huo, lkn pia kujifunza baadhi ya mbinu za upambanaji kupitia movie zake. Mpaka toka Bruce afariki mpaka leo bado anapewa heshima kubwa na magwiji wa mchezo huo wakiwemo wacheza sinema kama vile Jackie Chan, Jet Lee nk. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Bruce Lee.jpg


Wanaofuatia ni πŸ‘‡
4) Michael Jackson king wa Pop na mitelezo.

5) 2pac Shakur king wa Hip hop aliekuwa haiogopi serikali ktk kuwatetea wamarekani weusi wenzake na jamii nyingine zilizobaguliwa nchini Marekani, pia alipambana sana na polisi kuhusu unyanyasaji wowote uliofanywa na jeshi hilo kwa vijana mbali mbali hadi alipouwawa. Aliwahi kuwa na kesi ya kuwashambulia polisi wawili na bunduki, baada ya 2pac kupita sehem na gari aliwakuta polisi wakiwa wamemfunga pingu mtu mweusi huku wanampiga, kitendo kile kilimuuzi 2pac ndipo alipoamua kutoa bastola yake na kuwashambulia polisi, japo baadae polisi wale waliwahishwa hospital na kupona.
Katika kesi ile 2pac hakuhukumiwa baada ya kuonekana kuwa wale polisi walikuwa na makosa ya kiutendaji kwa mtuhumiwa waliekuwa wamemkamata.
Mungu awalaze roho zao mahali pema peponi.

6) Michael Jordan
Mzee wa kudumbukiza kikapuni. Huyu alikuwa na uwezo wa kuruka juu zaidi na kuonekana kama ameganda kwa sekunde kadhaa hewani kabla ya kutia mpira kapuni na kushuka chini. Toka astaafu bado hajapatikana Jordan mungine, japo bwana mdogo hayati Kobe Bryant alijitahidi kwa namna fulan, lkn bado hakufikia kule alipofikia mzee wa kazi.

Michael-Jordan.jpg


Hawa ni baadhi ya watu ambae mpaka leo viatu vyao viko wazi, havijapata wa kuvivaa vikawatosha.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nilikuwa nazungumzia tasnia ya music mkuu. Yuda naona ni upande wa watafuta pepo na kwenda mbinguni.
Ingawa uzi wako umechanganya musicians na wasio musicians, binafsi charity start at home,Said Mabera Ile solo yake inayakabana koo na piano, sitegemei nchi hii itampata mbadala wake ohoooo Shabaan Dede.....Fatumaaaaaaaa nasafiri mamaaaa, naona niishei hapa maana nimeshaanza kuwa emotional hapa
 
Hapo bila ya kuwepo Mike Tyson huu uzi utakuwa hauleti maana iliyokusududiwa...
Michael Tyson anaheshima yake ktk ngumi, lkn hawezi kufikia viwango vya Mohammed Ali mkuu. Ikumbukwe hata Tyson mwenyew ana mengi aliyojifunza kutoka kwa mtemi huyo wa ngumi ulimwenguni.
Sasa nikimuweka na Tyson itakuwa tasnia moja ina king wawili kitu ambacho kitasnia hakiwezekani mkuu.
 

Attachments

  • images (15).jpeg
    images (15).jpeg
    25.7 KB · Views: 48
Ingawa uzi wako umechanganya musicians na wasio musicians, binafsi charity start at home,Said Mabera Ile solo yake inayakabana koo na piano, sitegemei nchi hii itampata mbadala wake ohoooo Shabaan Dede.....Fatumaaaaaaaa nasafiri mamaaaa, naona niishei hapa maana nimeshaanza kuwa emotional hapa
Naongezea Diblo Dibala, Dally Kimoko, bila kumsahau Francoo wa Mario
 
Ingawa uzi wako umechanganya musicians na wasio musicians, binafsi charity start at home,Said Mabera Ile solo yake inayakabana koo na piano, sitegemei nchi hii itampata mbadala wake ohoooo Shabaan Dede.....Fatumaaaaaaaa nasafiri mamaaaa, naona niishei hapa maana nimeshaanza kuwa emotional hapa
Kwa upande wa nyumban kimziki hakuna na wala hatokuwepo mwanamziki mwenye uwezo wa kuimba na kutunga nyimbo zenye visa mbali mbali vya kweli na vile vya kufunza jamii kama Marijani mwana wa Rajabu.

Huyu waliomwita jabali la muziki Tanzania toka miaka hiyo hadi kufa kwake hawakukosea aisee. Mpaka serikali ilitambua mchango wake na baadhi ya nyimbo zake zikatumika shuleni na ktk mitihani mbali mbali ya kitaifa. Pia mwaka 2015 kama sijasahau alipewa tuzo na raisi J. Kikwete.

Lkn pia kuna wasanii wengine nao wanaheshimika kwa uimbaji na utungaji wao kama vile Mbaraka Mwinshehe, Bitchuka, Gurumo, Dede, Chidumule nk.

Ila kwa kuwa king wa tasnia huwa ni mmoja basi Marijani Rajabu ashakaba namba mda mrefu. RIP kwa wasanii wetu wote waliotangulia mbele ya haki.
 
Back
Top Bottom