Hawa ndiyo wabunge wa viti Maalum CHADEMA, CCM na CUF

Msekwa alikuwa na mkewe bungeni; Sitta alikuwa na mkewe bungeni; Malecela alikuwa bungeni na mkewe.............list goes on!!! Hakuna kigeni TZ hii...........!!

kwa sasa tumefikia kujilinganisha na ccm? .....nilifikiri tulitaka kuonyesha kuwa ccm haina maana!
 
Nimepata tamko hili toka Chadema:
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

UPOTOSHAJI KUHUSU VITI MAALUMU
Katika toleo lao la leo, magazeti ya Mtanzania na HabariLeo yamechapisha kile
walichokiita orodha ya viti ya wabunge wa viti maalumu kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo. Tunapenda kuwataarifu wanachama wetu na wananchi kwa
ujumla kuwa orodha iliyochapishwa na magazeti haya ni ya UONGO na imetolewa kwa
lengo la propaganda za kuyumbisha kampeni zetu katika dakika hizi za lalasalama.
Jambo moja la kuthibitisha uongo wa taarifa hizi ni ukweli kwamba orodha ya
majina iliyotolewa na magazeti haya mawili inatofautiana, pamoja na kwamba
magazeti haya yanadai kuwa wamepata kutoka kwa vyanzo vya habari vinavyofanana.


Tunawataarifu wanachama wetu na umma kwa ujumla kuwa, kwa mujibu wa makubaliano
kati ya chama chetu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, orodha yetu ya wabunge wa viti
maalumu ni siri na itajulikana baada ya uchaguzi mkuu kufanyika na si
vinginevyo.

2010 Hatudanganyiki


Hamad Rashid
Naibu Katibu Mkuu
 
ila sio siri hata kama hatupendi, hali kama ndio hii kazi ipo. kwa nini hao wanafamilia wasitafute kazi nyingine za kufanya kuijenga tanzania na kuonyesha uzalendo wao. kwani lazima wote waende bungeni? pamoja na kwamba slaa anayo kura yangu, haya mambo msijekuwa mnaturudisha kulekule tunakokukimbia .
 
Lawama hizo zimejidhihirisha kwani katika orodha hiyo, mbali na watoto na ndugu wa vigogo wa chama hicho, pia wabunge wote wa viti maalumu wa Chadema waliomaliza muda wao, wakiwamo wanaogombea katika majimbo ya uchaguzi, wamerudishwa katika orodha hiyo na kupewa nafasi za juu.

Wabunge waliomaliza muda wao walioko katika orodha hiyo ni Lucy Owenya ambaye ni mtoto wa mgombea ubunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo; na ni wa kwanza, jambo linalomhakikishia ubunge ikiwa uteuzi utafanyika kwa kufuata wa kwanza mpaka wa mwisho.

Wengine ni Mhonga Ruhwanya (namba 3), Halima Mdee (5), Grace Kiwelu (9) ambaye ni mkwewe Ndesamburo, Anna Komu (13) na Susan Lyimo (10).


Pia yumo Rose Kamil Sukum (19) ambaye ni mke wa mgombea urais wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa. Aidha, kwa mfumo huo wa Chadema, wagombea ubunge ambao wamo miongoni mwa majina hayo, watajihakikishia ‘ulaji’ bungeni endapo watashindwa katika majimbo hayo.

Wagombea hao wa majimbo walioko katika orodha hiyo ni Mdee wa Kawe, Leticia Nyerere (16), Kwimba; Regia Mtema (11), Kilombero na Sukum, Hanang. Wengine ni Christina Lissu Mughiwa (20) na Paulina Slaa Narcis (84).

Orodha hiyo pia imewataja Easther Matiko(2), Anna Mallac (4), Paulina Gekul (6), Conjesta Rwamlaza (7), Susan Kiwanga (8), Christowaja Mtinda (12), Mwanamrisho Abama (14), Joyce Mukya (15), Naomi Kaihula (17), Chiku Abwao (18), Raya Hamisi (21), Philipa Mturano (22) na Mariam Msabaha (23).

Wengine ni Rachel Mashishanga (24), Sabrina Sungura (25), Rebecca Mngodo (26), Cecilia Pareso (27), Subira Waziri (28), Leticia Musore (29), Helen Kayanza (30), Rosana Chapita (31), Mona Bitakwate (32), Evarim Mpangama (33), Asha Kayumba (34), Hija Wazee (35), Mary Martin (36), Sophia Mwakagenda (37), Bupe Kyambika (38), Magreth Mangowi (39), Esther Daffi (40), Jane Pesha (41), Aikande Kwayu (42) na Helga Mchomvu (43).

Pia orodha hiyo iliwataja walioteuliwa kuwa ni Rebecca Magwisha (44), Neema Msuya (45), Anastazia Manyanda (46), Selina Nguma (47), Bertha Matanwa (48), Christina Ngola (49), Lydia Mwaipaja (50), Zaituni Lubinza (51), Adelastela Kilindi (52), Hawa Mwaifunga (53), Loyce Iboma (54) na Rita Kanoro (55).

HabariLeo | Siri ya wabunge viti maalumu Chadema yavuja

Vipi unataka kuzima moshi kwa jirani yako wakati kwako kunawaka moto? toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndo uone kibanzi kwenye jicho la mwenzio.. niendelee?
 
Zubeda;
Nakushauri siku nyingine tafuta ukweli ndani ya chama chako kabla hujaleta habari kama hii ndani ya JF;hawa chini wafuatao ndiyo baadhi ya walioshinda ktk viti maalum ndani ya CCM

Je Zubeda unajua akina mama hawa ama wazazi wao au waume zao walikuwa au ni akina nani ndani ya CCM?Walioshinda viti maalum CCM ni:

Tina Andrew Chenge -Shinyanga

Namelok Edward Moringe Sokoine-Manyara

Salma Musa Bilal-ZNZ

Anna Margreth Abdallah Msekwa -NGO

Magretth Samwel Sitta-Tabora

Rosemary Kasimbi Kigirini-Mara

Janeth Maurice Masaburi-Dar

Rukia Masasi-Iringa

Zarina Shamte Madabida-Dar

Mboni Mohamed Mhita-youth

Asha Bakari Makame-ZNZ

Rosemary Mwanjelwa- MBY

Aziza unawajua akina mama hao niliowataja juu ndugu zao ndani ya CCM;madudu ya kuwapa vyeo ndugu zao yanaongozwa na CCM na ushahidi ni huo hapo juu ambapo karibu vigogo wote wa CCM wana ndugu zao kwenye viti maalum!

Rosemary Mwanjelwa ni nyapu wa JK
 
Kikwete, mgombea binafsi kwa staili ya BMW
ban.blank.jpg


Sarwed Dawalo​

amka2.gif
NYAKATI zimepita na majira ya uchaguzi kwa mara nyingine yamewadia hapa nchini. Uchaguzi Mkuu wa safari hii utakuwa wanne tangu siasa za vyama vingi zirejeshwe mwaka 1992.
Kwa wanasiasa, wagombea na wapiga debe, ni wakati wa vituko na kuropoka hovyo kwenye majukwaa. Na kwa wananchi wapiga kura, huu ni wakati wa kusikiliza ndoto na kughilibiwa kwa uongo usiokuwa na mashiko; kwa wenye akili kuchambua, kutafakari na mwishowe kujikusanya kifikra kwa kuchukua maamuzi yanayokidhi utashi binafsi.
Kampeni hizi zimekuwa zikiendelea kwa takriban miezi miwili sasa. Katika hali ya kawaida si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kukumbuka kila kilichoahidiwa na wagombea tofauti.
Hata hivyo, itoshe tu kusema kuwa yale yote waliosikiliza, kuona na hata kusoma magazetini hadi sasa yameshawasaidia kuunda uamuzi mioyoni mwao, sera au ahadi ipi imewakuna na mwelekeo upi maamuzi yao yatachukua.
Ni vyema tukatambua kuwa uchaguzi mkuu au mwingine wowote ni hatua ndogo katika ujenzi na kuimarisha demokrasi katika nchi. Kwa kuwa uchaguzi hutokea mara moja katika kila miaka mitano, ni vigumu kusema demokrasia ni uchaguzi pekee.
Katika hali ya kawaida na kwa wakati wote, ujenzi wa demokrasia kwenye jamii lazima ijumuishe ufahamu, uelewa, mwamko, ushiriki, ukereketwa nk. raia katika kila uamuzi ama wa pamoja au binafsi katika mambo yahusuyo maisha kwa ujumla, mtaa hadi taifa. Katika hali hiyo, demokrasia inageuka kuwa ni uhai wa kila siku wa taifa lililonawiri.
Wakati kampeni za kila chama ziko kwenye kasi ya juu, tumeweza kuona namna chama tawala, Chama Cha Mapinduzi kilivyojikita katika harakati hizo na staili ambayo wamechagua kufuata katika uchaguzi huu.
Kwa mara ya kwanza tumeona mgombea wa CCM ambaye anatetea kiti chake akipita huku na huko ‘akijinadi’ mwenyewe kama ‘mtoto mkiwa’. Jambo la kustaajabisha, wazee na viongozi wengine wastaafu wa Serikali zilizopita ambao wanavikwa heshima kubwa na Watanzania hawashiriki kampeni hizi za CCM. Mojawapo linawezekana, ama wamewekwa kando kwa makusudi au wamejiweka pembeni wenyewe.
Marais wastaafu Mwinyi na Mkapa hawapo pichani, makamu wenyeviti wa CCM, Karume na Msekwa halikadhalika. Mawaziri Wakuu wastaafu Warioba, Msuya, Sumaye na Salim gizani. Makamba, Kingunge na wengi wengineo hawajaonekana hata mara moja kwenye majukwaa ya CCM.
Amebakia hapa Dar es Salaam Abdulrahman Kinana akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM (wengi wametilia shaka kama kamati hiyo ipo kweli) kujibu hoja kwa waandishi wa habari kila inapotokea Dakta Slaa (mgombea wa CHADEMA) amerusha kombora.
Kwa ufupi, CCM safari hii imeacha kuiongoza kampeni na badala yake wamekuwa wakijibu mapigo ya Dk. Slaa tu.
Wamekuwa wakitumia muda mwingi kujitetea au kumkashifu Dakta Slaa na viongozi wengine wa upinzani. Kwa chama kilicho kubuhu kama CCM hatua hii ni ya kushangaza mno na ni ishara ya kupoteza umakini hususan kwenye ngazi ya juu ya uongozi wake.
Kwa mara ya kwanza, mgombea urais Jakaya Kikwete ameamua kuchukua hatamu za kampeni yake na kuongoza mwenyewe takriban kila idara. Tathmini nyepesi tu inaonyesha kuwa katika uchaguzi huu wa 2010, CCM imekosa mkakati madhubuti wa kushinda. Badala yake Kikwete amekuwa akipita kote na kumwaga ahadi za ajabu ajabu na ambazo uwezekano wa kuzitekeleza haupo.
Ni dhahiri kuwa hata kama nchi hii ingekuwa na utajiri wa nchi kama Marekani bado ahadi za Kikwete zingekuwa ngumu kutekelezeka. Hata hivyo, ukweli huu haujamzuia Kikwete kuendelea na ahadi zake. “Nitajenga hiki, nitafuta deni lile, nitakamilisha yale, nitawaleteeni hili nk. nk.” Kama vile kateremka leo kutoka sayari nyingine.
Kwa maono mengine, kwenye uchaguzi wa 2010 kwa kiti cha urais, CCM imesimamisha ‘mgombea binafsi’. Dalili zote zinaonyesha kuwa katika kinyang’anyiro cha urais CCM kama chama hakishiriki, ila Kikwete kama mwanachama wa CCM anagombea urais akiwa kama ‘Private Candidate’.
Kwa kuthibitisha upweke wake, Kikwete amewakabidhi kazi hiyo familia yake. Mama Salma Kikwete, mkewe, hajapumzika karibuni miezi miwili sasa. Wanawe nao akina Ridhwan wanazurura nchi nzima kumfanyia kampeni mkuu wao wa kaya.
Staili hii imekuja kujulikana kama ‘BMW’ au Baba, Mama na Watoto. Mikiki ya aina hii huioni kwenye ngazi ya chama. Ni kama vile viongozi wengine wa CCM wametulia huku wakisema ‘tuone litafika wapi’ nae Kikwete akisema ‘nitawaonyesha kuwa ninaweza na sitowahitaji’.
Ukiondoa mkakati huu wa mgombea binafsi wa CCM wenye mtazamo wa kifamilia pamoja na ahadi zisizo na mwisho, mbinu ingine ni kuongeza mabango yenye picha ya Kikwete nchi nzima. Watanzania wana ufahamu wa kuweza kumtambua Kikwete kama wakikutana naye hata usiku.
Mabango haya na hasa wingi wake unawafanya Watanzania wajinga na wasahaulifu wakubwa kiasi cha kushindwa kumtambua Rais aliewatawala kwa miaka mitano iliyopita. Aidha mabilioni yaliyotumika kuweka mabango hayo na waliofaidika na fedha hizo inawaachia maswali mengi wananchi wetu.
Hivi Kikwete (na si CCM) anaamini kweli kuwa wingi wa mabango ni hakika ya ushindi? Wanasaikolojia wamethibitisha kuwa kitu chochote ambacho umekizoea machoni kupita kiasi unakichoka na pengine hata kukichukia.
CCM ya sasa imeonyesha udhaifu wa hali ya juu kiasi kuwa hata viongozi wastaafu kadhaa wamekuwa wakilalamika hadharani kuhusu jambo hili.
Chama hiki kwa sasa kinajiendesha kimazoea na hadaa. Hadaa hii ni kwa wananchi wa kawaida wanaovaa mashati ya kijani na kucheza rhumba la TOT, huku wakiaminishwa kuwa wameegemea mbuyu hali kuwa ni kuti kavu ambalo litaanguka wakati wowote.
CCM imeingia kwenye uchaguzi huku ikinadi Ilani na sera zake, wakati kila mmoja akiionea haya katiba inayotamka kuwa Sera ya CCM ni ‘Ujamaa na Kujitegemea’. Mkengeuko mkubwa!!!
Kwa wale wachunguzi wa mambo, mashaka makubwa yamejidhihirisha kuhusiana na ufadhili wa CCM kwenye uchaguzi huu. Nikitafsiri methali ya Kiingereza ‘they are spending money like they have no hands’ yaani ‘wanamwaga fedha utafikiri hawana mikono ya kuzishika hizo fedha’.
Sasa haya ndiyo mambo yaliyo dhahiri. Ukweli kuhusu nani kapenyeza nini CCM kitajulikana muda si mrefu tangu sasa.
Matumizi mabaya ya mali za umma anayofanya Salma pamoja na kujivika uongozi wa CCM nayo pia yatakuwa bayana.
Inasemekana Salma siku hizi ana uwezo hata wa kuita viongozi wa kitaifa na wakaitika. Wanahistoria, mtujuvye ufalme huwa unaanza vipi na nini viashiria vyake?
Miezi michache iliyopita, serikali ya CCM iliweza kushinda kesi mahakamani dhidi ya mwanaharakati Christopher Mtikila, ambaye alikuwa akipigania kubadilishwa kwa sheria ili iruhusu ‘mgombea binafsi’ kwenye chaguzi zetu. Siku zote CCM wamekuwa na msimamo wa wazi kuhusu jambo hili, wanaliogopa na kulipinga kwa nguvu zote.
Kinyume chake, CCM katika uchaguzi huu imeamua kusimamisha mwanachama wake, Jakaya Kikwete, kama ‘mgombea binafsi’. Wapiga kura wamechanganyikiwa, ikitokea Kikwete kaibuka mshindi, Tanzania itatawaliwa na nani? Chama kwa maana ya CCM au mtu binafsi kwa maana ya Kikwete na familia?


h.sep3.gif

sdawalo@yahoo.com


https://www.jamiiforums.com/uchaguz...ikwete-mgombea-binafsi-kwa-staili-ya-bmw.html

Kikwete, mgombea binafsi kwa staili ya BMW
 
Nimepata tamko hili toka Chadema:

Mwanakijiji babu--we both now the truths. Hilo tamko la chama ni kutuzingua. Kila mtu anajua jinsi watu walivyopasua vichwa kuwachagua hao wagombea. As the matter of fact sitakuwa surprised kama WanaChadema non-wachaga ndio wameilikisha hii story.

Bottom line its the truth, kama mnabisha. Tusubiri hayo majina yakiekwa hadharani. Its the matter of time.
 
Nimepata tamko hili toka Chadema:

Mwanakijiji babu--we both now the truth. Hilo tamko la chama ni kutuzingua. Kila mtu anajua jinsi watu walivyopasua vichwa kuwachagua hao wagombea. As the matter of fact sitakuwa surprised kama WanaChadema non-wachaga ndio wameilikisha hii story.

Bottom line its the truth, kama mnabisha. Tusubiri hayo majina yakiekwa hadharani. Its the matter of time.
 
Mwanakijiji babu--we both now the truth. Hilo tamko la chama ni kutuzingua. Kila mtu anajua jinsi watu walivyopasua vichwa kuwachagua hao wagombea. As the matter of fact sitakuwa surprised kama WanaChadema non-wachaga ndio wameilikisha hii story.

Bottom line its the truth, kama mnabisha. Tusubiri hayo majina yakiekwa hadharani. Its the matter of time.

wewe selemani hujaacha upuuzi wako huu, non-wachaga ndio kina nani?
 
wamesahau wafoji vyeti wa bot

Kwa hiyo ninyi mnashabikia kuondoa uozo wa CCM ili uje katika sura mpya au? No wonder wengine we only see a giant sign on ur cause saying....ITS OUR TURN TO EAT....

Kitendo cha kuhalalisha mapungufu yenu eti kwa kuwa na wengine nao wanamapungufu kama yenu kinanikumbusha statement ya ROSTAM kuwa Tanzania hatuna tatizo la ufisadi ukilinganisha na wenzetu wa Kenya ama DRC.....
 
Msekwa alikuwa na mkewe bungeni; Sitta alikuwa na mkewe bungeni; Malecela alikuwa bungeni na mkewe.............list goes on!!! Hakuna kigeni TZ hii...........!!

Mr. Zero,

Hao wote unaowasema walichaguliwa na wananchi na hawakuteuliwa na viongozi. Lakini pia tumekuwa tukiilaumu CCM hapa kwa mambo hayo hayo, leo hii CCM ndio kipimo cha mabadiliko yanayoletwa na CHADEMA?

Wangeruhusu wanawake wachague watu wanaotaka wawe wawakilishi wao bungeni na sio mijianaume ndio inawachagulia wanawake wawakilishi wao.
 
Kaka...umafia wanajua wengi tena wengine ni wazoefu na wamejaaliwa nyenzo na dhamira kali....Hii dharuba inaelekea ni kali, zinakuja nyengine nyingi....

hakuna dharuba yoyote ile ... ccm mtalia mwaka huu (labda mtumie ubabe kama Kibaki na Mugabe).
 
Tupe na orodha ya watoto wa vigogo wa CCM walorisishwa nafasi na ulaji katika chama hicho. Hii itatupa nafsi nzuri ya kufanya comparison.

Ridhiwani JK na yule mdogo wake teja pamoja na mama yao Salma, January Makamba na nduguye Mwamvita, Husein Mwinyi, Mtoto wa Kigoma Malima, Mke wa spika Sitta, Dada yake Abdalla Kigoda, mke wa William Shelukindo, aliyezaa na Kitwana Kondo. orodha ni ndefu mno...
 
Back
Top Bottom