Hatutakubali hili la nyongeza ndogo ya mshahara!

moesy

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
3,555
Reaction score
3,539
wafanyakazi wamevumilia vya kutosha,hizi ambali za kuongeza mshahara kati 6% to 11% Kama zitakuwa ni za kweli wakatiwa kutangazwa kwa bajeti 2013/2014,kamwe wafanyakazi hatutavumilia upuuzi huu wa miaka nendarudi,hivyo tunangoja tusikie hilo ongezeko litakuwaje kupitia waziri wa kazi.

Na serikali ikae ikijua jinsi gharama za maisha zilivopanda maradufu likiwemo hili la nauli mpya,ni muda wa wafanyakazi kuungana na kudai haki za msingi ikiwemo ongezeko la mshahara unaokidhi maitaji ya kila siku ya binadamu
 
Kila mwaka serikali ya dhaifu inajigamba kuongeza mishahara lkn ongezeko hilo ni 6% na 12%,tumechoka kunyaswa hatutakubali.
 
nauli zimepanda kwa asilimia 20-24 ila mshahara asilimia 6! Tutakufa mbona. Hapo bado mafuta, mahindi, maharage, kodi za nyumba, mboga za majani!
 
Pleni sana watumishi wa Serikali hii ambayo siku zote imekuwa upande wa wafanyabiashara na kuwaacha wafanyakazi na wasio na kazi bila mtetezi.
 
Najionea huruma mimi mfanyakazi wa serikali! sijui nini kitatukomboa kipindi hiki. Wakati ule tuliambiwa asiyetaka na akae nyumbani, hata kura yetu haikuwa na thamani! Leo nini kitatukomboa??? Hapa tulipo tuna madeni kila upande, hizo salali silipu zinatia huruma; sasa hii nauli ndo itatumaliza kabisaaaaaaaa. Tukimbilie wapi? mmh
 
tatizo la msongo wa mawazo limekuwa kubwa tz,sababu ya mishahara midogo kupita kiasi wakati maitaji na gharama za maisha kubana.
hii inamaana ya kwamba ata umri wa kuishi wa mtz unapungua sana,kutokana na mawazo kupita kiasi
 
Na wewe ungekuwa serikali ungefanya nini? Mna akili ndogo kinyama....kuna mtu hapendi mishahara ipande? Budget yoooote iende kwenye mishahara? Serikali serikali serikali ulivyokuwa mjinga tena utasema mafisadi haya hela walizochukua hao mafedhuli zitatosha kupandisha mishahara ya watumishi wote? Haya rasilimali nyingi Sanaa kuna gesi kuna madini hela yakuchimba ikowapi? Wakitusaidia Wachina ooh serikali inasaidiana na Wachina kutuibia. Cha msingi jitume kiume ufanikiwe na ukiona mlango wa kuchukua kidogo pitia pia na hao wezi tuwa wajibishe kwa Kira 2015
 
Yaani wewe ndio unaakili ndogo kama tigo,umeshindwa atakuelewa kinachozugumziwa apa,akili kama mt,,,ko,tulia uzae bwana mdogo bado una akili za kitoto.
 
si mlishaambiwa asiyetaka achape lapa? Na bado ndo maisha bora hayo
 
TUCTA jamani isimamie maslahi ya wafanyakazi wanakamuliwa mno. Ebu angalia unakatwa PAYE na bado kila bidhaa na huduma unayopata unalipia tena kodi. Mbona wanajeshi wao wamepunguziwa makali kwa si wafanyakazi kama wengine. Tuamke jamani tunanyonywa na mafisadi wa Richmond, Dowans, EPA n.k.
 
Sijakuelea MOES unasema HATUTAKUBALI wewe na akina nani? halafu ewe ni manafunzi au mfanyakazi?
 
Ahsante kwa maswali mazuri,
QN1 Hatutakubali mimi na pamoja na wafanyakazi wenzagu waliobuni njia kambabe,ya akili ya khali ya juu ,very diplomatic way kukabiliana na suala hili,subiri yako macho.
qn2 Nimeshalijibu kwenye swali la kwanza apo juu,
 
na wewe ungekuwa serikali ungefanya nini? Mna akili ndogo kinyama....kuna mtu hapendi mishahara ipande? Budget yoooote iende kwenye mishahara? Serikali serikali serikali ulivyokuwa mjinga tena utasema mafisadi haya hela walizochukua hao mafedhuli zitatosha kupandisha mishahara ya watumishi wote? Haya rasilimali nyingi sanaa kuna gesi kuna madini hela yakuchimba ikowapi? Wakitusaidia wachina ooh serikali inasaidiana na wachina kutuibia. Cha msingi jitume kiume ufanikiwe na ukiona mlango wa kuchukua kidogo pitia pia na hao wezi tuwa wajibishe kwa kira 2015
binamu wa naapee huyoo
 
mimi nataka upunguzwe ili wafanyakazi wakitanzania wawe na akili ya kufaham kwamba serikali ni yao, wao ndio wamiliki na sio serikali ndio inayowamiliki.
 
wafanyakazi wamevumilia vya kutosha,hizi ambali za kuongeza mshahara kati 6% to 11% Kama zitakuwa ni za kweli wakatiwa kutangazwa kwa bajeti 2013/2014,kamwe wafanyakazi hatutavumilia upuuzi huu wa miaka nendarudi,hivyo tunangoja tusikie hilo ongezeko litakuwaje kupitia waziri wa kazi.

Na serikali ikae ikijua jinsi gharama za maisha zilivopanda maradufu likiwemo hili la nauli mpya,ni muda wa wafanyakazi kuungana na kudai haki za msingi ikiwemo ongezeko la mshahara unaokidhi maitaji ya kila siku ya binadamu

Tatizo wafanyakazi wa nchi hii waoga,Lazima watu wajitolee kuwa kafara kwa ajili ya wengine na maneno YA mbayuwayu!!!!!!!AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO!!! HAKUNA MFANYAKAZI WA TANZANIA MWENYE UWEZO WA KUANDAMANAAA!!!
 
Wamefanikiwa kutugawa sana watumish wa umma.Kuna tabaka la wenye nacho na wasionacho.Wengi wenye vididrii wana kimshahara ahueni na ndio wenye fursa za kupata posho nyingi na marupurupu mengine.Wengi ni watawala na waliobaki ni waoga sana hawana huo ujasiri!Ugumu wa hawa wa chini ambao ndio wanafanya kazi sana na maslahi yao ni madogo sana ni kuwa hawawezi kugoma wakiwa chini ya wasimamizi waoga kwa hofu ya kusalitiwa.Naona nguvu ya kura isipofanikiwa hatuna jinsi!Kwani hoja pia si kupanda mishahara tu,bali ni kuimarisha uchumi ili wasipandishe ovyo
ovyo bei za vitu.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
umeongea ukweli mkuu.
 
mbeya ingechukuliwa na malawi sasahivi, ningehamia mbea ambayo ni sehemu ya malawi. Nimechoka.
 
Back
Top Bottom