Hatutakubali hili la nyongeza ndogo ya mshahara!

Hatutakubali hili la nyongeza ndogo ya mshahara!

Najionea huruma mimi mfanyakazi wa serikali! sijui nini kitatukomboa kipindi hiki. Wakati ule tuliambiwa asiyetaka na akae nyumbani, hata kura yetu haikuwa na thamani! Leo nini kitatukomboa??? Hapa tulipo tuna madeni kila upande, hizo salali silipu zinatia huruma; sasa hii nauli ndo itatumaliza kabisaaaaaaaa. Tukimbilie wapi? mmh

kiongozi,
kitakachotukomboa ni sisi wenyewe kusimama kidete bila woga wala unafiki kulipigania hili.
tusikimbie popote tuwe hapa tulipo ili tupambane nalo. tukikimbia haitasaidia na huko tunakotaka kwenda je ndipo msaada ulipo?
umoja na mshikamamno ndio unaoleta mapinduzi
 
Tatizo wafanyakazi wa nchi hii waoga,Lazima watu wajitolee kuwa kafara kwa ajili ya wengine na maneno YA mbayuwayu!!!!!!!AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZA KWAKO!!! HAKUNA MFANYAKAZI WA TANZANIA MWENYE UWEZO WA KUANDAMANAAA!!!

nakubaliana na wewe asilimia mia. yani watanzania wanajua wanaonewa wanatamani mabadiliko lakini hawana uthubutu wa kufanya mapinduzi yoyote yale. wachache wanaojaribu huvunjwa nguvu na wengi wasioweza kujaribu.
kudai haki ni utamaduni unaohitaji moyo wa dhati kuuishi.
tukibadilika katika hili tutaona matunda yake
 
gharama za vyakula zinapanda kila siku, gharama za ada za shule zinapanda, usafirishaji ndio hivyo tena matibabu ndio usiseme, gharama za maji kwa baadhi ya maeneo ni kubwa mno, mishahara bado duni kwa nini mtanzania huyu asichanganyikiwe na kuwa tayari kufanya lolote.
halafu mnasema eti wanasema nchi haitatawalika.
nyinyi serikali ndio mnafanya nchi haitawaliki.
matokeo ya haya : ujambazi unaongezeka ufisadi na rushwa unakuwa kwa kasi kila mtu anawahi chake mapema. dhuluma na kutokuwapo na haki, vurugu nyingi zinatokea watu hawana cha kupoteza serikali ijitafakari na kuangalia namna ya kuboresha maisha badala ya kuendelea kudidimiza maisha ya wananchi kwa namna moja au nyingine.
 
Kila mwaka serikali ya dhaifu inajigamba kuongeza mishahara lkn ongezeko hilo ni 6% na 12%,tumechoka kunyaswa hatutakubali.

Jamani hivi mshahara kiasi gani ndio unatosha? kwa sababu hata wabunge wetu wanaojilipa vizuri wanatamani kuongezewa tena. Hata wabunge wa nchi jirani ilioko kaskazini (jina kapuni) nao hawajatosheka pamoja na donge nono wanalolipwa.
 
kiongozi,
kitakachotukomboa ni sisi wenyewe kusimama kidete bila woga wala unafiki kulipigania hili.
tusikimbie popote tuwe hapa tulipo ili tupambane nalo. tukikimbia haitasaidia na huko tunakotaka kwenda je ndipo msaada ulipo?
umoja na mshikamamno ndio unaoleta mapinduzi

Sawa Mkuu, Lakini si unakumbuka kipindi kilichopita kabla ya uchaguzi??? Ile hotuba iliyotolewa kwa wale vibibi na vibabu vilivyokuwa vinasinzia? unakumbuka na wale viongozi wa mshikamano wetu walivyoingia mitini? Nahisi mambo yatajirudia na tutabaki kukabwa koo kwa maslahi sifuri.

Hata hivyo najipa moyo, wanasemaga HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA.
 
Najionea huruma mimi mfanyakazi wa serikali! sijui nini kitatukomboa kipindi hiki. Wakati ule tuliambiwa asiyetaka na akae nyumbani, hata kura yetu haikuwa na thamani! Leo nini kitatukomboa??? Hapa tulipo tuna madeni kila upande, hizo salali silipu zinatia huruma; sasa hii nauli ndo itatumaliza kabisaaaaaaaa. Tukimbilie wapi? mmh
Dada Happiness, sisi wafanyakazi wa Serikali hatutakaa tupate maslah ya kukidhi viwango vya maisha. Hili sio tu kwa serikali ya Tanzania, hata wafanyakazi wa nchi nyingine ndivyo ilivyo. Kubwa ni kujiongeza na kuwa businesswoman/man. Ila kwa kuendelea kuajiriwa, hatutaacha kutoa milio, hasa kwa nchi maskin kama yetu.
 
Dada Happiness, sisi wafanyakazi wa Serikali hatutakaa tupate maslah ya kukidhi viwango vya maisha. Hili sio tu kwa serikali ya Tanzania, hata wafanyakazi wa nchi nyingine ndivyo ilivyo. Kubwa ni kujiongeza na kuwa businesswoman/man. Ila kwa kuendelea kuajiriwa, hatutaacha kutou milio, hasa kwa nchi maskin kama yetu.

Kinachouma zaidi ni jinsi wakuu wa serikali wanavyotumbua maisha na wadogo tunavyosota na maisha. Si wafanyakazi wote wa serikali wenye hali mbaya wapo wasiojua tatizo la pesa maofisini mwao na hii ndio inasababisha wafanyakazi wa serikalini wasiwe na mshikamano thabiti.

Kuwa business woman kuasaidia tatizo ni capital na muda wa kufuatilia hiyo biashara. Mikopo imetuzunguka hadi unashindwa uanzie wapi.
 
Nakuelewa ila mark my words, true financial freedom ipo kwenye self employment. Kwa kuendelea kuajiriwa hata ufaidi vipi wakati huu km muajiriwa, ukistaafu tu shida ulizoziahirisha miaka mingi zitakurudia kwa speed ya ajabu.

Ninachowasihi watumishi wenzangu ni kuwa matatizo haya yanayotukabili, yawe ndiyo chachu ya sisi kufikiria kujiajiri. Ukiachana na ajira, muda utakuwa mwingi sana wa wewe kujikita kwenye Shuguli yako. Zipo shughuli nyingi sana zenye faida kubwa tu ambazo wala hazihitaji mitaji ya mabilion.

Kikubwa kinachotakiwa ni Moyo/utayari wa kujiajiri na wala sio mtaji. Mitaji ipo kwenye mabenk ila tu watu wamekosa utayari. Eneo moja ambalo ukikomaa unatoka ni kilimo cha mpunga. Nenda Ifakara au Kyela kafanye utafiti then utanambia.
 
Nenda kajiajiri. Kama hutaki kujiajiri kaa kimya.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nakuelewa ila mark my words, true financial freedom ipo kwenye self employment. Kwa kuendelea kuajiriwa hata ufaidi vipi wakati huu km muajiriwa, ukistaafu tu shida ulizoziahirisha miaka mingi zitakurudia kwa speed ya ajabu.

Ninachowasihi watumishi wenzangu ni kuwa matatizo haya yanayotukabili, yawe ndiyo chachu ya sisi kufikiria kujiajiri. Ukiachana na ajira, muda utakuwa mwingi sana wa wewe kujikita kwenye Shuguli yako. Zipo shughuli nyingi sana zenye faida kubwa tu ambazo wala hazihitaji mitaji ya mabilion.

Kikubwa kinachotakiwa ni Moyo/utayari wa kujiajiri na wala sio mtaji. Mitaji ipo kwenye mabenk ila tu watu wamekosa utayari. Eneo moja ambalo ukikomaa unatoka ni kilimo cha mpunga. Nenda Ifakara au Kyela kafanye utafiti then utanambia.

Asante. Umezalisha kitu kipya akili mwangu. Mungu akubariki
 
Na wewe ungekuwa serikali ungefanya nini? Mna akili ndogo kinyama....kuna mtu hapendi mishahara ipande? Budget yoooote iende kwenye mishahara? Serikali serikali serikali ulivyokuwa mjinga tena utasema mafisadi haya hela walizochukua hao mafedhuli zitatosha kupandisha mishahara ya watumishi wote? Haya rasilimali nyingi Sanaa kuna gesi kuna madini hela yakuchimba ikowapi? Wakitusaidia Wachina ooh serikali inasaidiana na Wachina kutuibia. Cha msingi jitume kiume ufanikiwe na ukiona mlango wa kuchukua kidogo pitia pia na hao wezi tuwa wajibishe kwa Kira 2015
Hoja zenu ni nzuri na za msingi lakini punguzeni ukali wa ,maneno
 
Ushauri wangu ni kwamba sisi kawa wazalendo tutoe ushauri ni erikali inatakiwa kufanya na kipi tumebaini kuwa ni kasoro. Kama tutabaki tunalalamika na kujifari kuwa hata ungekuwa wewe upo serikalini ungefanya hivyohivyo nadhani siyo sahihi. Kwani ukipata wewe uliyoko serkalini na mimi mchemsha nyadogi nitafaidika kwa sababu lazioma utataka kula.
 
Asante. Umezalisha kitu kipya akili mwangu. Mungu akubariki
Pouwa Happiness, I would be happy to hear from you one day kuwa umeachieve ua freedom financially. Check hii Youtube clip ya huyu jamaa, then utanambia why uwe masikini. http://www.youtube.com/watch?NR=1&feature=fvwp&v=dvdkyyM4z48 zipo nyingi sana Youtube zitakupa moyo sana wa kufanya maamuzi. Check pia Youtube clip za Robert Kiyosaki zitakupa mwanga zaid. Mind you! You are responsible for your richness/poorness. Sio mwajiri wala mzazi.
 
Si tumekubali kutawaliwa na serikali ya ccm, hivyo tuendelee kuwa wavumilivu tu!
 
Kinachouma zaidi ni jinsi wakuu wa serikali wanavyotumbua maisha na wadogo tunavyosota na maisha. Si wafanyakazi wote wa serikali wenye hali mbaya wapo wasiojua tatizo la pesa maofisini mwao na hii ndio inasababisha wafanyakazi wa serikalini wasiwe na mshikamano thabiti.

Kuwa business woman kuasaidia tatizo ni capital na muda wa kufuatilia hiyo biashara. Mikopo imetuzunguka hadi unashindwa uanzie wapi.
Happiness nimekumbuka pia, kuna mradi wa ufugaji Nyuki ambao kwa sasa baada ya wachina kujenga kiwanda hapo nyumbani unalipa sana. Ufagaji wa nyuki huitaji kuwanunulia chakula kama kuku, what you need ni kuwa na shamba km heka 2 tena porini, ukaweka hapo kibanda/Mizinga then nyuki kwa muda wao wataingia na kwa muda wao watajilisha. Nyuki Mtu haibi so unahitaj minimum supervision. Wakikubali vizuri, you can earn upto 300m per year. Hivi kwa kuwa mtumishi kweli utapata leo pesa hizi???Hata hicho kiinua mgongo kinachotufanya tusote kitafika hiyo pesa??? Miradi ni mingi sana ambayo for sure inahitaji utayari zaidi kuliko mtaji.
 
Mradi huu unahitaji pori; nitalipata wapi?? itakuwa mbali sana. Kwa kuwa nataka kuanza kujishughulisha, naomba unishauri miradi ambayo nitaifanya eneo/karibu na ninapoishi. Natanguliza shukrani kwako; maana sio siri maisha ya mfanyakazi wa serikali hii yamekuwa balaa
 
asilimia 80% ya wafanyakazi wa serikali wanaenda kazini kama ushahidi tu.
duh! kweli kabisa yaani kuna watumishii wa umma uwa wapo full time jf na fb sijui wanafanya kazi saa ngapi?
 
Mradi huu unahitaji pori; nitalipata wapi?? itakuwa mbali sana. Kwa kuwa nataka kuanza kujishughulisha, naomba unishauri miradi ambayo nitaifanya eneo/karibu na ninapoishi. Natanguliza shukrani kwako; maana sio siri maisha ya mfanyakazi wa serikali hii yamekuwa balaa
Nimeitaja miradi hii kwa vile ulisema mtaji ni tatizo, hiyo haitumii mtaji mkubwa sana. Great investment ni investment inayohusisha ardhi, so usione ngumu kutoka nje ya mji na kununua shamba/ardhi. Hapo Kisarawe, bagamoyo, mkuranga, kigamboni yapo mashamba mazuri tu tena kwa bei nzuri tu wala usiogope. Huko shamba utamweka shamba boy ambaye utamlipa kwa commission kwa miradi utayomuwekea, kikubwa unamjengea kibanda na kuingia naye mkataba wa kumlipa kwa % flan ya kile kitachopatikana ktk miradi yako huko shamba. Ardhi hiyo itawatoa hata wajukuu zako.

Kwenye ardhi hiyo ambayo partly itakuwa na mizinga ya nyuki, nusu yake panda miembe ya kisasa ipo SUA (2500@) na AMAGRO (4000@) karibu na Kibasila secondari. Hii miembe ndani ya miaka mi 3 inazaa. Ukiwa na miche yako 200, kila mche ukatoa maembe lets say 200 na kila embe ukauza TZS 300 you can imagine how much utapata kwa mradi huo wa maembe tu, hapo wa nyuki hujauhesabia.

Kumbuka miembe inazaa maembe kadri inavyokuwa na maembe yanapanda bei kila siku na hakuna sustainable supply ya maembe hapo mjini ingawa population inaongezeka kila siku. Watu wanaona shida kusubiria hii miaka mitatu, wanataka kupanda mahindi tu. Take your time visit shamba moja lipo maeneo ya Kerege nafkiri as you go to Bagamoyo. Utajifunza mengi kwa kuskia maneno toka kwenye horsemouth.

Miradi ya karibu na unapoishi ipo mingi ila cna uzoefu nayo sana coz cjaifanyia utafiti wa kutosha, naogopa kukushuri kitu nisichokitafiti vya kutosha. Ila upo mradi mmoja wa Network Marketing unaitwa Forever Living. Hawa wanadistribute vyakula vyenye viini lishe au madawa yanayotokana na Aloe vera/organic products. Note. Network marketing ni moja ya aina za business zinazoongoza kwa kulipa hapa duniani.

Hii biashara ni ya kimtandao, na inamtandao mkubwa sana hapa Duniani. Unaweza ukajiunga nao then nawe ukawa part ya huo mtandao na ukawa unaenda kupata mafunzo yao, unaweza hudhuria seminars zao hapo utaelewa vizuri sana na utajua wap pa kuanzia, na haihitaji mtaji mkubwa kuingia na kutoka kimaisha, unahitaji network nzuri na commitment. Ukihitaj kujua naweza nikakulink na mtu.
 
Na wewe ungekuwa serikali ungefanya nini? Mna akili ndogo kinyama....kuna mtu hapendi mishahara ipande? Budget yoooote iende kwenye mishahara? Serikali serikali serikali ulivyokuwa mjinga tena utasema mafisadi haya hela walizochukua hao mafedhuli zitatosha kupandisha mishahara ya watumishi wote? Haya rasilimali nyingi Sanaa kuna gesi kuna madini hela yakuchimba ikowapi? Wakitusaidia Wachina ooh serikali inasaidiana na Wachina kutuibia. Cha msingi jitume kiume ufanikiwe na ukiona mlango wa kuchukua kidogo pitia pia na hao wezi tuwa wajibishe kwa Kira 2015

Kama sio bangi itakuwa chang'aa....
 
Watanzania tuna asili ya kulalamika bila juhudi zozote,,ukiangalia vizuri mishahara ni midogo lkn sisi wenyewe tunafanya nini kujiongezea kipato,,,? Siku zote mshahara hautoshi hata ulipwe kias gani,,,,
 
Back
Top Bottom