Hatutakubali hili la nyongeza ndogo ya mshahara!

Hatutakubali hili la nyongeza ndogo ya mshahara!

Wamemwaga mboga tunamwaga ugali ..na diplomatic way tutaiadabisha CCM na serikali yao,wait and see
 
Nimeitaja miradi hii kwa vile ulisema mtaji ni tatizo, hiyo haitumii mtaji mkubwa sana. Great investment ni investment inayohusisha ardhi, so usione ngumu kutoka nje ya mji na kununua shamba/ardhi. Hapo Kisarawe, bagamoyo, mkuranga, kigamboni yapo mashamba mazuri tu tena kwa bei nzuri tu wala usiogope. Huko shamba utamweka shamba boy ambaye utamlipa kwa commission kwa miradi utayomuwekea, kikubwa unamjengea kibanda na kuingia naye mkataba wa kumlipa kwa % flan ya kile kitachopatikana ktk miradi yako huko shamba. Ardhi hiyo itawatoa hata wajukuu zako.

Kwenye ardhi hiyo ambayo partly itakuwa na mizinga ya nyuki, nusu yake panda miembe ya kisasa ipo SUA (2500@) na AMAGRO (4000@) karibu na Kibasila secondari. Hii miembe ndani ya miaka mi 3 inazaa. Ukiwa na miche yako 200, kila mche ukatoa maembe lets say 200 na kila embe ukauza TZS 300 you can imagine how much utapata kwa mradi huo wa maembe tu, hapo wa nyuki hujauhesabia.

Kumbuka miembe inazaa maembe kadri inavyokuwa na maembe yanapanda bei kila siku na hakuna sustainable supply ya maembe hapo mjini ingawa population inaongezeka kila siku. Watu wanaona shida kusubiria hii miaka mitatu, wanataka kupanda mahindi tu. Take your time visit shamba moja lipo maeneo ya Kerege nafkiri as you go to Bagamoyo. Utajifunza mengi kwa kuskia maneno toka kwenye horsemouth.

Miradi ya karibu na unapoishi ipo mingi ila cna uzoefu nayo sana coz cjaifanyia utafiti wa kutosha, naogopa kukushuri kitu nisichokitafiti vya kutosha. Ila upo mradi mmoja wa Network Marketing unaitwa Forever Living. Hawa wanadistribute vyakula vyenye viini lishe au madawa yanayotokana na Aloe vera/organic products. Note. Network marketing ni moja ya aina za business zinazoongoza kwa kulipa hapa duniani.

Hii biashara ni ya kimtandao, na inamtandao mkubwa sana hapa Duniani. Unaweza ukajiunga nao then nawe ukawa part ya huo mtandao na ukawa unaenda kupata mafunzo yao, unaweza hudhuria seminars zao hapo utaelewa vizuri sana na utajua wap pa kuanzia, na haihitaji mtaji mkubwa kuingia na kutoka kimaisha, unahitaji network nzuri na commitment. Ukihitaj kujua naweza nikakulink na mtu.

Umenifungulia siku! Hapa nilipo kuna mtu ananielezea kuhusu mashamba yanayouzwa bagamoyo 450000 kwa eka. Kama si kesho basi jumapili nitaenda huko angalau nipate hiyo eka moja kwa kuanzia, je inatosha?.
 
Serikali imeshindwa kufanya kazi zake ipasavyo moja wapo ni hili la mishahara kiduchu isiyo endana na gharama harisi za maisha.
 
Watanzania tuna asili ya kulalamika bila juhudi zozote,,ukiangalia vizuri mishahara ni midogo lkn sisi wenyewe tunafanya nini kujiongezea kipato,,,? Siku zote mshahara hautoshi hata ulipwe kias gani,,,,

siyo kulalamika mkuu wangu wafanyakazi wanaitaji japo mwajiri wao(serikali) awalipe kiasi cha kuweza kumudu only basic human need( chakula,malazi,mavazi,maji,afya) hakika kwa sasa kuna wafanyakazi wanakula mlo mmoja tu,ushaidi ninao,maskini taarifa niliyopata muda sio mrefu kuna mwalimu mwendesha bodaboda amekufa kwa ajali ya kugongwa na fuso,wakati akijiongezea kipato.

wafanyakazi hawaitaji mamilion kama ya wabunge,wanchoitaji ni ongezeko la maana tu kuweza kumudu maitaji ya kawaida ya kila siku.
kwa iyo matarijio yetu ni ongezeko lenye tija na wala sio hili la 6%.
 
Umenifungulia siku! Hapa nilipo kuna mtu ananielezea kuhusu mashamba yanayouzwa bagamoyo 450000 kwa eka. Kama si kesho basi jumapili nitaenda huko angalau nipate hiyo eka moja kwa kuanzia, je inatosha?.
Yap! kwa kuwa huna hata moja, hiyo inatosha sana kwa sasa. You will have more than that before this year ends cause naona umedhamiria kweli na upo committed kumake changes in your life. Hiyo ni hatua kubwa sana mana inaonekana wazo la shamba hukuwa nalo kabisa, huo ndio tunauita uthubutu. So chukua hilo then tutajua nini cha kufanya ndan ya hilo shamba as i told you.

Tena kama anaheka zaid ya moja mwambie akupe 2 au 3 then nyingine akudai, utamlipa taratibu ndivyo watu wanavyonunua ardhi. Bagamoyo ardhi inapanda sana. Leo unannua kwa 450,000 hadi mwezi wa 6. watauza 800,000 kwa heka. Watu wengi sana wanaelekea huko. Nadhan unaskia mipango ya serikali ya kuuendeleza mji wa Bagamoyo. Utakuwa mji muhimu sana hapo Tanzania kwa hizi plan ninazozisikia.
 
Yap! kwa kuwa huna hata moja, hiyo inatosha sana kwa sasa. You will have more than that before this year ends cause naona umedhamiria kweli na upo committed kumake changes in your life. Hiyo ni hatua kubwa sana mana inaonekana wazo la shamba hukuwa nalo kabisa, huo ndio tunauita uthubutu. So chukua hilo then tutajua nini cha kufanya ndan ya hilo shamba as i told you.

Salute!
 
tatizo la serikali halisikilizi kilio cha wafanyakazi wake na ndio maana wizi ndani ya halmsahauri na wizara hautapungua, mtu anasimamia mradi wa milion 100 alafu analipwa mshahara wa laki 2 unategemea hiyo kazi ifanyike kwa ufanisi kweli, serikali ichukue hatua ya kuboresha maslai ya watumishi ili hata mtu akichakachua tujue ni mwizi tu na sio kwasababu kipato kimekuwa kidogo
 
tatizo la msongo wa mawazo limekuwa kubwa tz,sababu ya mishahara midogo kupita kiasi wakati maitaji na gharama za maisha kubana.
hii inamaana ya kwamba ata umri wa kuishi wa mtz unapungua sana,kutokana na mawazo kupita kiasi

Umri wa kuishi unapungua kutokana na life style pamoja na tamaa. Adam 'n Eve hawakulipwa mshahara wowote na YHWH lakini waliishi miaka mingi sana, wakila matunda na mizizi wakilala nje coz hawakuwa na maghorofa au ma-sky scraper kama humu tunamoishi leo.
 
Umri wa kuishi unapungua kutokana na life style pamoja na tamaa. Adam 'n Eve hawakulipwa mshahara wowote na YHWH lakini waliishi miaka mingi sana, wakila matunda na mizizi wakilala nje coz hawakuwa na maghorofa au ma-sky scraper kama humu tunamoishi leo.

Ni kweli mkuu life style inachangia,lakini ata ili la msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha sio la kupuuziwa.Enzi za Adam& Eve hakukuwa na system ya mishahara,walikuwa wanatunzwa na sir god moja kwa moja kwa kupew kila ktu,ila wakamuuzi mungu akaamua kuwamaliza.
Adama& Eve ni ni sawa na viongozi wengi wa sasa wanapewa mishahara minono,marupurupu,nyumba,gari lakini bado wanakuwa wezi wakubwa/mafisadi
 
Kila mwaka serikali ya dhaifu inajigamba kuongeza mishahara lkn ongezeko hilo ni 6% na 12%,tumechoka kunyaswa hatutakubali.


ni kweli yametimia kama ilivyotabiriwa ongezeko ni 8.4%,wafanyakazi tuungane kupinga hili
 
Hata kama ungepewa 300% , mshahara huwa hautoshi kamwe. Mtumishi unatakiwa kutumia mshahara wako kuwekeza au kuzalishia pesa.
 
Mokoyo; Hakika ukipata mtaji ni vema kujiajiri, tatizo hawa mafisadi wa bongo wanapeleka hela Uswisi badala ya kuweka benki za ndani na kukopesha kwa riba nafuu!
 
Last edited by a moderator:
hii topic niliiweka hewani tarehe 4april 2013,baada ya kupata taarifa toka vyanzo ndani ya serikali kuwa ongezeko litakuwa 6%--12%,lakini waziri wa kazi alijaribu kudaganya watumishi wa serikali kuwa ongezeko litakuwa 25%,sasa imebainika ongezeko la 2013/2014 ni 8.4%
 
Wafanyakazi tuungane tujitetee wenyewe,hatuna wakututetea we jiulize tu tokea umepata Akili umewai kumuona mbunge akikutetea,ila wafanyabiashara wanatetea sana kuanzia kufutiwa Kodi na fulsa nyingine tuungane
"VV"
 
mlioko serikalini tuisusie serikali tutafute private tukafanye huko tuone serikali itawatumia akina nanai?
 
Back
Top Bottom