Hatujui kesho yetu

Hatujui kesho yetu

Bonjour

Jamani haya maisha , tuache kudharau watu ambao tunawajua na tusio wajua

Kuna jamaa yangu mmoja, nili meet nae almost 5 years ago alikuwa boda boda, alikuwa ana park kimara pake stend ya kuelekea Bonyokwa, nakumbuka alikuwa amechoka na kama kapoteza future , ila Leo tumekutana tena hapa Kambi ya jeshi Twalipo.. ni officer wa jeshi jwtz , ana nyota tatu (3)

Ana mdogo wake pia , ni soldier komando , last time nili meet nae, alikuwa school driving..

Aisee ime nipa hope sana

Kuhusu alifikaje , kasema ataniambia ..

Tuache kuwachukulia watu poa .
Haipaswi kumdharau Binadamu yeyote, awe fukara, mlemavu, Tajiri n.k

Tuheshimiane tu.
 
Usidharau mtu na wale usihofie kuhusu siku zijazo ,lolote linaweza kutokea.

Usiwe na wasi kuhusu kesho yao ila pambana kupata chochote kuendesha maisha yako ya baadae... Mwezi wa nane nilikuwa Dar nimekaa hapo miaka kibao ila mwezi wa tisa nimepata kazi sehemu nyingine na naishi mkoani sasa.

Nilikuwa na mipango kibao haswa huu mwezi wa 12 ila sipo tena nipo sehemu nyingine...Sisi wanadamu hatujui chochote kuhusu kesho yetu.
Kabisa mkuu.
Me mwez wa 7 nilipanga nitoke home nikapange ilikuwa Arusha imefika mwez wa 7 nimeanza kukaa geto Tabora☺️
 
Lengo lake zuri sana nimelielewa la kutumotivate lakini mfano wake wa mchongo.....
Sio mfano Mzee .

It's really.. nimeona stars kwenye mabega..

Sasa mm sijui, mchakato wa kupata hiko cheo inachukua muda.

Ninachojua ukiwa na Elimu kubwa ndio unapata promotion ya vyeo

Na jamaa na meet, alikuwa kashamaliza chuo, miaka kadhaa nyuma

Ni big brother kabisa kwangu..
 
before alikuwa mlinzi wa getini .. now ni Afisa habari Wizara ya kilimo
Hawa ni wengi sana hata Sugu alikua Mlinzi wa getini baadhi ya wachungaji ukimtoa Mwmposa wakisimulia simulizi zao watakwambia waliwahi kua walinzi magetini
 
Kaka, mm ni bachelor Holder, ila kazi ninayo fanya ,acha tu

Ila naamini Kuna siku nitakuwa mkubwa
HAlafu balaa ni kwamba kuna wadau wanasoma comment yako wanaweza kukuvusha Ila sasa wanakuacha uendelee kuwa mtumwa, you're a slave you keep on obeying your master na unalipwa ujira kidogo Pole sana mtumwa.

Sasa kuna watumwa wengi sana wenye maelezo kama yako huku wakiwa wamebebeshwa vyeti vinaitwa degree wengi hujisemea Mimi ni degree holder Ila kazi ninayoifanya acha tu yaan nilijua nikisoma nitapata kujikomboa Ila nimebaki kuwa mtumwa.

Pole tena mtumwa wewe ni mtumwa umepigwa minyororo na hata ukipata decent job utumwa wako hautoishia hapo wewe ni mtumwa mpaka unaingia kaburini, pole sana mtumwa

Nitaandika shairi lako mtumwa...
Pole sana mtumwa
 
Don’t worry bro,,,the best issue ni kutokata tamaa kamwe regardless of what they say,,,coz no one can live your life on your behalf. Keep on moving little by little you will reach your destiny.
Mtumwa mmoja anamfariji mtumwa mwingine, nice and sweet

Pole sana mtumwa
 
Huku kitaa kuna jamaa alikuwa anaokota makopo ni kichaa kabisa amevurugika juzi juzi tulimuona yuko kwenye msafara wa kiongozi fulani kavaa kaunda suti😁
 
Huku kitaa kuna jamaa alikuwa anaokota makopo ni kichaa kabisa amevurugika juzi juzi tulimuona yuko kwenye msafara wa kiongozi fulani kavaa kaunda suti😁
Hiyo haipo siku hizi hawafanyi hivyo.
 
Et mtu umheshimu kisa ana mafanikio ko asipokuwa na mafanikio unayotaka basi hastahili heshima , mtoa mada ni ndezi Sana , na ndo chanzo cha kutengeneza machawa , hii nchi vijana wamekuwa machawa na walamba miguu ya watu
Tuende poke, kwa upwndo, kwa kujengana, kwa kuelewa kuwa kuna wengi wanajifunza mambo, wanajifunza maisha.

Kitu kimoja nilichojifunza JF ni kwamba, hapa kuna watu wa kila aina, kila rila, kila uzoefu.

Kwa hivyo, unaweza kukuta watu wawili tofauti sana wanajibizana, na wasipojua kupeana nafasi ya kujibizana vizuri, kitakachofuata ni matusi.

Mtoa mada ya msingi sijui umri wala elimu rasni yake, wala upeo wake, ika nimependa sana alivyoandika.

Kitu kikubwa anafundisha au kukumbusha jamii ni kuheshimiana, kutochukuliana poa tu.

Hili ni somo zuri sana ambalo wengi tunaweza kulitumia, hata mimi.

Kitu kingine anachotufundisha ni juwa maendeleo yanahitajika, yanatuheshimisha, ni jambo ambalo linatupasa wote tulilenge.

Hapo sina cha kumpinga. Yumkini ukiwa na rafiki ambaye hana maendeleo, halafu ukakutana naye baada ya miaka michache ana maendeleo, hayo maendeleo aliyoyapata ni kitu kizuri, ni kitu cha kupigiwa mfano, si kitu cha kubezwa. Hapo sijampinga hata tone. Mimi pia hupenda kujifunza kwa watu, sio tu walioendelea zaidi yangu, bali hata wale waliojiendel3za kutoka walipokuwa mara ya mwisho mpaka walipo sasa ambao hawajaendelea kama mimi labda. Kitu muhimu ni kujua wamepigaje hatua. Maana dunia inabadilika kila simu, na pengine hata mimi ninayeweza kujiona niko zaidi yao, nikawa sijajua kupiga hatua kwa haraka na ufanisi zaixi katika dunia ya leo, nikajifun,a kitu kutoka kwao. Hapo sina tatizo.

Kwa hivyo, kimsingi, mtoa mada namuelewa sana na mambo aliyoandika ni ya msingi sana.

Nilitaka kukumbushia tu point moja ya msingi kwamba, watu wote wanastahili heshima. Waliofanikiwa na wasiofanikiwa.

Kwa sababu, kwanza, si watu wote wanaostahili heshima wanafanikiwa.

Watu wengine huwa wanaacha mambo yanayoweza kuwapa heshima katika jamii fulani - hususan kupata pesa na positions za uongozi- kwa sababu zenye kuweza kuwapa heshima ya juu zaixi ya habari za pesa na uongozi.

Kwa hivyo, unapokutana na, kwa mfano, mtu ambaye alipata nafasi ya kuibia wananchi na kuwa tajiri mkubwa sana, lakini hakufanya hivyo, akijua kuwa cheo ni dhamana, akafanya kazi kwa uadikifu, akastaafu vizuri bila kupita njia za rushwa, kwa mtazamo fulani akawa masikini, huyu ni mtu wa kuheshimiwa, si mtu wa kubezwa kwa sababu hakuiba mali za umma kama jamii yetu ilivyotarajia.

Kwa hiyo, heshima ipimwe kwa mambo mengi yenye kina, kuzidi mafanikio ya juu juu tu ya nani ana kazi gani, ana hela ngapi.

Tuangalie mchango mkubwa zaidi kwa jamii.
 
Unaheshimu mtu au unaheshimu mafanikio aliyoyapata mtu, na heshima kwa mtu inakuja kutokana na mafanikio yake tu?

Ungemkuta kachoka zaidi ya alivyokuwa miaka mitano iliyopita ingekuwa sawa kumchukulia poa tu?

Tuwaheshimu watu kwa sababu kesho wanaweza kupata mafanikio zaidi na hatujui nani atapata mafanikio zaidi?

Au tuwaheshimu watu tu, kwa sababu kuwaheshimu watu ni jambo jema, bila kujali kama watu hawa tunaowaheshimu watapata mafanikio au hawatapata?
Supported
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom