Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala wa Bora Bi. Sophia Simba ameliambia Bunge leo kuwa serikali haijashindwa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa Saileth Vithlani ambaye anadaiwa kupokea rushwa ya Shs. Bilioni 12 katika ununuzi wa Rada. Bi. Ghasia amesema kuwa serikali haitosita kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwani uchunguzi bado "unaendelea".
Vile vile Bi. Ghasia ameliambia Bunge kuwa TAKUKURU haifanyi kazi kwa upendeleo au woga wa wala rushwa wa kubwa. Alisema hivyo kufuatia madai kuwa serikali inafanya haraka sana kuwafikisha mahakamani wala rushwa wadogo wadogo lakini wale wakubwa inaonekana kusua sua au kuwaogopa. Alisema kuwa Sheria mpya ya Rushwa ya 2007 haitenganishi wala rushwa wadogo wadogo au wakubwa.
Bi. Ghasia aliyasema hayo na mengine katika majibu yake ya hoja za Wabunge waliochangia mjadala wa bajeti wa Wizara yake hapo jana .