Hawa ndio wanaweza kuzuia Rushwa Tanzania

Lidafo

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
551
747
Rushwa ni hali ya mtu kutenda au kutokutenda jambo fulani kwa mtu au kikundi cha cha watu kwa nia ya kujipatia faida binafsi, Baada ya kupatiwa au kuahidiwa kupatiwa kiasi fulani cha fedha au vitu vinginevyo, Kinyume cha matakwa au misingi ya kazi.

Kutokana na maana ya rushwa hapo juu utagundua kuwa, Mpokea rushwa aghalabu mtoa rushwa ni mtu mwenye mamlaka fulani, ama katika utumishi wa umma au katika kampuni au taasisi Fulani.

Imezoeleka kwa Tanzania kusemwa kuwa rushwa ni adui wa haki nahii ni kauli inayosemwa na Viongozi wa kisiasa, Watumishi wa umma na kutiliwa nguvu sana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Lengo la uzi huu sio kuchambua utendaji kazi wa TAKUKURU bali ni kutoa mtazamo wangu juu ya ni kina nani hasa wanaweza Kupambana na kuzuia rushwa Tanzania.

Katika kufahamu ni kina nani wanaweza Kuzuia Rushwa Tanzania kwanza nataka tuainishe maeneo ambayo rushwa imekithiri ili nitakapo bainisha wanaoweza kupamabana na rushwa sote twende pamoja.

MAENEO AMBAYO RUSHWA IMEKITHIRI

Maeneo ambayo rushwa imekithiri ni Jeshi la polisi aghalabu na majeshi mengine, vyuoni hasa rushwa ya ngono, Wizara zote za Tanzania, Hospitalini, mahakamani, Taasisi za Serikali na zisizo kuwa za serikali, Serikali za mitaa, Vyama vya Siasa n.k Ni ngumu kutaja taasisi zote za serikali ila tuelewe kuwa popote penye Taasisi ya serikali ama isiyo ya serikali kuna harufu ya rushwa.

KINA NANI WANATUHUMIWA KUHUSIKA NA RUSHWA?

Hapa utaona watanzania wengi tunapigia kelele TAKUKURU na Watumishi wote walio katika nafasi nilizozitaja hapo juu mfano maaskari, Madaktari, Mahakimu, Walimu, wenyeviti serikali za mitaa, makatibu n.k
Swali la kujiuliza ni, je, ni kweli askari wa kawaida anaweza zuia rushwa?

Ni kweli katibu serikali za mitaa anaweza zuia rushwa ni kweli TAKUKURU wanaweza zuia rushwa? Kama jibu ni Hapana Kwanini wanabebeshwa majukumu hayo na lawama? Kama jibu ni ndiyo mbona rushwa ipo na ndo kwanza inazidi?

Binafsi siamini kwamba tunaweza zuia rushwa kwa kutegemea wala rushwa kuzuia rushwa bali rushwa huzuiwa na watu wenye nguvu kubwa ya kimamlaka katika serikali tena wenye nia ya dhati ya kutaka kupambana na kukomesha rushwa.

HAWA NDIO WENYE UWEZO WA KUPAMBANA NA RUSHWA TANZANIA

RAIS WA NCHI
Rais ndio mwenye nguvu kubwa katika serikali kuu. Kwa nchi kama Tanzania ambapo Rais amepewa mamlaka ya kuteua Viongozi wa kubwa kabisa katika dola kama mkuu wa majeshi ya ulizi, Jeshi la Polisi jaji mkuu, mkurugenzi usalama wa taifa, TAKUKURU, Bandari, Mawaziri n.k
Kwa mamlaka haya ni wazi kuwa kwa kuteua na kupendekeza wakuu katika taasisi mbalimbali Rais mwenye nia ya dhati ya kupambana na rushwa ataweza kuteua watu wenye kufanana nae ambao watakuwa na nia kama yake ili waweze kumsaidia kukomesha rushwa.

MAKAMO WA RAIS
Huyu ni kiongozi namba mbili mwenye uwezo wa kukomesha rushwa Tanzania kwani kwa muundo wa majukumu yake ya kazi ataweza kumshauri Rais na pia kuwawajibisha wote wenye nia tofauti na misingi ya serikali hasa katika kukabiliana na rushwa.

WAZIRI MKUU
Huyu ndiye injini ya Kupambana na rushwa kwani Wizara zote zipo chini yake na tukumbuke kila wizara imechafuka rushwa hivyo ikiwa Waziri mkuu atasimama kisawasawa ataweza kudhibiti mawaziri wake na kusafisha uchafu wote wenye kuendeleza rushwa kwenye wizara mbalimbali na hivyo kuacha wizara zikiwa safi.

SPIKA WA BUNGE NA BUNGE KWA UJUMLA
Spika ndio kiongozi wa bunge na moja kati ya kazi za bunge ni kuwasilisha mawazo na matatizo ya wanachi katika serikali kuu na moja ya tatizo sugu ni rushwa ikiwa spika ataamua kusimama kisawasawa kupamabana na rushwa basi wataweza kuiwajibisha serikali na kuitaka kufagia kila mla rushwa.

JAJI MKUU
Kwakuwa suala la rushwa ni suala ambalo litahitajiaka Kwenda kuthibitika na kutolewa hukumu mahakamani jaji mkuu hapa atahitajiaka kuwa imara na mwenye weledi mkubwa katika kusimamia shughuli mbalimbali za kimahakama ili haki itendeke.

Ni hitimishe kwa kusema kwamba Muunganiko wa Rais, Makamo wake, Waziri Mkuu, Spika wa bunge na Jaji mkuu huu ndio muunganiko wenye uwezo mkubwa wa kuzuia rushwa usio shindwa ila kwa sharti tuu wote wawe na nia ya dhati ya kupambana na rushwa.

Embu fikiri afisa anaeyefanya kazi TAKUKURU amegundua kuna harufu ya rushwa Wizara fulani alafu anapeleka taarifa kwa wakubwa zake anaambiwa hilo suala ni la wakubwa aking’ang’ania kutafiti anaishia kuamishwa kituo cha kazi. Mtu huyu atapoteza shauku yake na ataishia naye kuwa mla rushwa

Mwisho niseme kuwa kuendelea kuona tatizo linamea kila siku na kukosa ufumbuzi ni Ushahidi wa wazi kuwa kuna shida kubwa katika mifumo Ya nchi yetu hivyo ni wakati sasa wa Rais kuamua kwa dhati kusafisha kila aina ya waovu na wabaya wasio na nia nzuri kwa taifa hili ili kuweka mambo sawa vinginevyo Tanzania itakuwa ya watanzania wengi inayofaidiwa na watanzania wachache.
 
Rushwa ni sehemu ya maisha ya mswahili. Trafic asipotumia rushwa hakuna gari itatembea barabarani.
Tra wasipochukua hakuna duka litafunguliwa
 
Jaji atakufunga Kwa kula rushwa na haliyakua kala rushwa Ili ufungwe Kwa kisingiziwa umekula rushwa🤣🤣👆🏿
 
Rushwa ni sehemu ya maisha ya mswahili. Trafic asipotumia rushwa hakuna gari itatembea barabarani.
Tra wasipochukua hakuna duka litafunguliwa
Kwanini asiruhusu bila kula rushwa? Hii inamaanisha kuwa rushwa ni tabia iliyojijenga na ni tabia sugu hivyo basi kuna umuhimu wa kurekebisha mifumo yetu ili kuiua tabia hiyo.
 
Kwanini asiruhusu bila kula rushwa?
Hii inamaanisha kuwa rushwa ni tabia iliyojijenga na ni tabia sugu hivyo basi kuna umuhimu wa kurekebisha mifumo yetu ili kuiua tabia hiyo
Vipato vyao havitoshi vimepelekea tabia
 
Jaji atakufunga Kwa kula rushwa na haliyakua kala rushwa Ili ufungwe Kwa kisingiziwa umekula rushwa🤣🤣👆🏿
Ndio maana nikasema jaji mkuu anapaswa kuwa na nia ya dhati ya kutokomeza rushwa il kufunga mianya yote ya rushwa.
 
Vipato vyao havitoshi vimepelekea tabia
Vipato ni sababu moja wapo lakini ukiangalia kuna watumishi wa serikali wanapokea mpaka milioni 7 na posho juu ila bado wanakula rushwa hapo napo vipi?
 
Uzalendo wa kweli na tena baada ya kuondoshwa kikamilifu adui ujinga ndipo tu adui rushwa ataweza punguzwa kwa kiasi kikubwa, kwani kuondoshwa kabisa ni ngumu, hao ulio wataja pekee yao hawawezi kwani wenyewe ni wasimamizi tu wa mifumo na mifumo hiyo inaundwa na watu, watu ndio wala rushwa na ndio wasimamizi wa mifumo 🤔.
 
Rushwa ni tabia binafsi ya mtu kutokuwa na utashi wa kufuata utaratibu.

Familia, dini na shule ni taasisi za msingi katika kujenga kizazi kinachoheshimu na kufuata utaratibu.

Uliowaelezea hapa ni kweli wanaweza kupambana na rushwa iwapo taasisi za msingi zitatimiza wajibu wake bila tashwishi.
 
Wazalendo pekee waliobaki; madaktari wa falsafa Prof. Kabudi na Dr. Bashiru huwezi kuwaacha listi ikakamilika. Watu waliopinga rushwa hata ukiwatazama usoni unaona hivyo! Ha ha ha!
 
Back
Top Bottom