Hatujashindwa kumfikisha mahakamani Vithlani-Ghasia

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala wa Bora Bi. Sophia Simba ameliambia Bunge leo kuwa serikali haijashindwa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa Saileth Vithlani ambaye anadaiwa kupokea rushwa ya Shs. Bilioni 12 katika ununuzi wa Rada. Bi. Ghasia amesema kuwa serikali haitosita kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwani uchunguzi bado "unaendelea".

Vile vile Bi. Ghasia ameliambia Bunge kuwa TAKUKURU haifanyi kazi kwa upendeleo au woga wa wala rushwa wa kubwa. Alisema hivyo kufuatia madai kuwa serikali inafanya haraka sana kuwafikisha mahakamani wala rushwa wadogo wadogo lakini wale wakubwa inaonekana kusua sua au kuwaogopa. Alisema kuwa Sheria mpya ya Rushwa ya 2007 haitenganishi wala rushwa wadogo wadogo au wakubwa.

Bi. Ghasia aliyasema hayo na mengine katika majibu yake ya hoja za Wabunge waliochangia mjadala wa bajeti wa Wizara yake hapo jana .
 
One more inefficient public figure....

Ili nchi yetu ipate kuendelea inapaswa ku-get rid of viongozi wa design hizi.

Viongozi wetu siku hizi wakiulizwa maswali nyeti woote wanatupatia jibu la aina moja... "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA". Sasa nazidi amini kwamba nchi yetu iko usingizini na itaendelea kuwa usingizini wakati nchi nyingine (kama Mauritius) zikiwa zinachapa kazi kujiongeza maendeleo. We need Mwalimu afufuke aje kuwachapa viboko watu wa dizaini hizi. Tumechoka sasa!!!
 
Hii mbona haijatulia?

Vithlani hajapokea rushwa bali amesaidia kufanikishwa kwa ununuzi wa "radar" na yeye akapata mshiko wake.

Sasa inakuwaje tena anaonekana amepokea rushwa?
 
RICH.....! NAOMBA NITOE MFANO TOFAUTI KIDOGO.....!
'siku moja wanafunzi wake YESU walimuona mtu akitoa pepo KWA JINA LA YESU! wakamkataza kwa maana haambatani nao, wakamwendea YESU naye akawaambia........ mwacheni kwa maana ....... asiye kinyume chetu yu upande wetu...! (wapo wengine niliopewa wasio wa nyumba hii)'
ASANTE.....! SASA SWALI LAJA UPO UPANDE WA MAFISADI AU WAZALENDO......? (ni swali tu)
 
One more inefficient public figure....

Ili nchi yetu ipate kuendelea inapaswa ku-get rid of viongozi wa design hizi.

Viongozi wetu siku hizi wakiulizwa maswali nyeti woote wanatupatia jibu la aina moja... "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA". Sasa nazidi amini kwamba nchi yetu iko usingizini na itaendelea kuwa usingizini wakati nchi nyingine (kama Mauritius) zikiwa zinachapa kazi kujiongeza maendeleo. We need Mwalimu afufuke aje kuwachapa viboko watu wa dizaini hizi. Tumechoka sasa!!!
UNDERTAKER WA JF punguza nzuka......! hata sisi tulio hai twaweza....! tuimbe nyimbo zetu za kizalendo huku twasonga mbele katika mapambano
 
Aliyetoa majibu hayo ni Sphia Simba. For more information, amesema kuwa uchunguzi huo unasimamiwa na Takukuru na karibu utakamilika na jalada lake kufikishwa kwa DPP. Amesema haikuwezekana kutangaza kuwa Takukuru inalichunguza suala hilo kutokana na matakwa ya sheria mopya ya Takukuru ambayo inazuia kutaja majina ya watu wanaochunguzwa au kusema uchunguzi unaoendelea.
Kuhusu mapendekezo ya Zitto kuhusu UWT, Sphia Simba alisema serikali imeyachukua mapendekezo yote aliyoyatoa na itayafanyia kazi. Eneo kubwa ni kuiangalia sheria na sera ya UWT kwa lengo ya kuziboresha ili kuifanya taasisi hiyo ifanye kzi kwa ufanisi.
 
UCHUNGUZI UTAKAMILIKA KABLA YA BUNGE AMA BAADA YA BUNGE?
NA kama ni baada ya BUNGE...Then wabunge vunjeni SIRIKALI.
 
Hakutaja tarehe specific kama ni kabla au baada ya bunge, amesema HIVI KARIBUNI.
 
RICH.....! NAOMBA NITOE MFANO TOFAUTI KIDOGO.....!
'siku moja wanafunzi wake YESU walimuona mtu akitoa pepo KWA JINA LA YESU! wakamkataza kwa maana haambatani nao, wakamwendea YESU naye akawaambia........ mwacheni kwa maana ....... asiye kinyume chetu yu upande wetu...! (wapo wengine niliopewa wasio wa nyumba hii)'
ASANTE.....! SASA SWALI LAJA UPO UPANDE WA MAFISADI AU WAZALENDO......? (ni swali tu)

Hapana labda sijaeleweka.

Kwanza napenda uelewe kwamba mimi ni mmoja wa wapenzi wa mabadiliko makubwa katika Tanzania na hapa JF ndio mahala pa kuelezea hoja za mabadiliko hayo.

Kwa hio mimi siko upande wa wazalendo tena wale "fundamentalist" ambao tungependa kuona hoja kama za mheshimiwa Ghasia ni pumba tupu.

Nafahamu Vithlani ana pasi mbili za kusafiria na kwa sasa hayupo Tanzania.

Lakini nilidhani kwamba kwa kusema Vithlani amepokea rushwa badala ya kwamba yeye ni facilitator wa ufisadi mzima (kwa mujibu wa Mheshimiwa Ghasia) hapo kidogo pana utata.

Vithlani ni mhujumu, mtengenezaji na mgawaji rushwa na wale waliofanikisha suala hilo zima la RADAR ni wale wapokeaji wa 10% na rushwa zingine.

Kwa hio nafikiri tuangalie pia wale watu ambao wana pasi zaidi ya moja za kusafiria kwamba matatizo wanayosababisha Tanzania ni makubwa na hawawezi kuwekwa chini ya sheria.

Ukumbuke Vithlani yupo nje ya Tanzania na kibali cha kumkamata kinahitajika na suala la radar limehusisha mtandao mkubwa sana.
 
Aliyetoa majibu hayo ni Sphia Simba. For more information, amesema kuwa uchunguzi huo unasimamiwa na Takukuru na karibu utakamilika na jalada lake kufikishwa kwa DPP. Amesema haikuwezekana kutangaza kuwa Takukuru inalichunguza suala hilo kutokana na matakwa ya sheria mopya ya Takukuru ambayo inazuia kutaja majina ya watu wanaochunguzwa au kusema uchunguzi unaoendelea.
Kuhusu mapendekezo ya Zitto kuhusu UWT, Sphia Simba alisema serikali imeyachukua mapendekezo yote aliyoyatoa na itayafanyia kazi. Eneo kubwa ni kuiangalia sheria na sera ya UWT kwa lengo ya kuziboresha ili kuifanya taasisi hiyo ifanye kzi kwa ufanisi.

asante sana.... hilo la usalama wa Taifa nimelipenda.
 
Mama huyu naye.

SFO imethibitisha kuwa jamaa alipewa hongo: yeye mwenyewe alikiri mbele ya SFO. Kikwete alishalia faulo kuwa BAE "walituonea." Ni zaidi ya mwaka tangu taarifa hizo ziwekwe wazi na account ambayo ilipokea hongo hiyo inajulikana. Iweje Ghasia huyu aendelee kutudanganya kuwa serikali inafanya uchunguzi; inaweza kufanya uchunguzi wa maana zaidi ya ule wa SFO?
 
Mbona wasimfikishe sasa mahakamani kama hawajashindwa? hizi ndio siasa za majungu, kila kukiwa na jambo serikali au waziri wanasema wanalifanyia kazi hadi lini maneno yasiyo na mfupa yataendelea hivi. Baraza letu la mawaziri limejaa porojo sana na amana waliyopewa ya kulinda mali ya wananchi na mali ya taifa sidhani kama wanayotena!!!
 
Bwana n'logo nimekuwa nafwatilia posht shako...... mbona una kishirani shana na UWT???????? Walikupota nke nini??????????????????????

ingekuwa mke ningewaachia, kina dada wanatuzidi wanaume 6 to 1 (I have no idea whose statistics is that)...naweza kupata mwingine hata kwa kupiga 900 number... (not that I have done that before..) hapana wameacha nchi yangu iporwe! and that my friend is serious kwani ninayo nchi moja tu.
 
Hakuna mtu mwenye pesa ameshawahi kufungwa Tanzania!! hizo ni hadithi

I guess you are right.

Tanzamia hakuna sheria ila kwa walala hoi tu. Ukishika bastola ukainyoosha kumlenga mtu na kuifyatua ukamuua mtu yule uliyemlenga halafu ukashikwa red-handed kwenye crime scene, pesa yako itafanya kesi dhidi yako iwe ya kuua bila kukusidia.
 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala wa Bora Bi. Sophia Simba ameliambia Bunge leo kuwa serikali haijashindwa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa Saileth Vithlani ambaye anadaiwa kupokea rushwa ya Shs. Bilioni 12 katika ununuzi wa Rada. Bi. Ghasia amesema kuwa serikali haitosita kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwani uchunguzi bado "unaendelea".

Vile vile Bi. Ghasia ameliambia Bunge kuwa TAKUKURU haifanyi kazi kwa upendeleo au woga wa wala rushwa wa kubwa. Alisema hivyo kufuatia madai kuwa serikali inafanya haraka sana kuwafikisha mahakamani wala rushwa wadogo wadogo lakini wale wakubwa inaonekana kusua sua au kuwaogopa. Alisema kuwa Sheria mpya ya Rushwa ya 2007 haitenganishi wala rushwa wadogo wadogo au wakubwa.

Bi. Ghasia aliyasema hayo na mengine katika majibu yake ya hoja za Wabunge waliochangia mjadala wa bajeti wa Wizara yake hapo jana .

Huu ni uongo unatumiwa kila siku. Sasa hivi hatujawa wajinga wa kudanganywa kiasi hiki. Kama RA wanamuogopa, Vithlani ndio hawezi kabisa kumgusa. Yule jamaa kwa sasa ni untouchable, hata Ghasia kwa kutoa kauli kama hiyo inabidi aangalia mgongo wake. I am sure kwa serikali iliyopo sasa hakuna mweye uwezo wa kumtikisa Vithlani. Uchunguzi wa tuhuma dhidi yake utaedelea hado atakapokufa, na hatafikishwa popote!
 
Mbona wasimfikishe sasa mahakamani kama hawajashindwa? hizi ndio siasa za majungu, kila kukiwa na jambo serikali au waziri wanasema wanalifanyia kazi hadi lini maneno yasiyo na mfupa yataendelea hivi. Baraza letu la mawaziri limejaa porojo sana na amana waliyopewa ya kulinda mali ya wananchi na mali ya taifa sidhani kama wanayotena!!!

Hiyo ndiyo michanga ya macho ndugu yangui!!..haitaisha leo wala kesho!
Wewe fikiria huu msemo umeshausikia mara ngapi kutoka kwa viongozi wetu "uchunguzi unafanyika na pindi utakapokamilika tutachukua hatua madhubuti "

Kwa sisi wazalendo hii tunaiona kama staili ya kufunika makaa ya moto mpaka hapo yatakapopoa halafu libeneke linaendelezwa kama kawa!

Naona ndugu zangu kuwa wakati sasa umefika kupeana time frame na progressive report katika uchunguzi! hasa inapokuwa ni uchunguzi unaohusu mambo mazito kama haya juu ya Taifa letu.

Ama sivyo yatapita kama yale ya dawa za kulevya....

Wembe
 
Yaani Tanzania sasa imegeuka nchi ya uchunguzi na tume period! Hata muda wa kukaa tupange maendeleo ya mbele haupo tunabaki tumeeee, uchunguziiiii, kamatiiiiii, yaani naona kihindi hindi tu!
 
Back
Top Bottom