Hatma ya Muslim University of Morogoro na Maono ya Aga Khan kuwasaidia Waislamu kujenga Chuo Kikuu

Kinyungu,
Tunasubiri majibu kutoka kwa muhusika.
Mtasubiri hadi Yesu arudi. Chuo ni chenu hakuna aliyewazuia kujenga halafu unasema mnasubiri majibu ya Serikali. Hii haingii akilini. Je hiyo serikali isipojibu? Hamtajenga? Je ikisema imeshawapeni kile cha Morogoro mtafanyaje?

Jiongezeni sheikh
 
Mtasubiri hadi Yesu arudi. Chuo ni chenu hakuna aliyewazuia kujenga halafu unasema mnasubiri majibu ya Serikali. Hii haingii akilini. Je hiyo serikali isipojibu? Hamtajenga? Je ikisema imeshawapeni kile cha Morogoro mtafanyaje?

Jiongezeni sheikh
Hawakujenga wao, walipewa majengo ya chuo cha Tanesco, labda tuseme umeme ulikatika.
 
Mtasubiri hadi Yesu arudi. Chuo ni chenu hakuna aliyewazuia kujenga halafu unasema mnasubiri majibu ya Serikali. Hii haingii akilini. Je hiyo serikali isipojibu? Hamtajenga? Je ikisema imeshawapeni kile cha Morogoro mtafanyaje?

Jiongezeni sheikh
Kinyungu,
Kwanza ningependa ufahamu mimi si sheikh kabisa.

Muhimu sana ukanifahamu nilivyo Ili tuwe na uwelewano mzuri.

Hapa huzungumzi na sheikh.
Elimu yangu yote ni sekula.

Subra Ina manufaa makubwa sana.

Serikali inapokuwa haijibu kuna faida pia kwa upande wetu.

Tunajiuliza kwa nini?

Jibu ni kuwa serikali imetambua tunasema kweli na imeingia uoga.

Haiwezi kukiri kuwa ndani ya Wizara ya Elimu au NECTA kuna matatizo yanayotakiwa kurekebishwa.

Prof. Hamza Njozi aliandika kitabu cha mauaji ya Mwembechai na dhulma za serikali.

Hapakuwa na uongo katika kitabu kile.

Kitabu kikapigwa marufuku.

Tulikuwa na uwezo wa kuviingiza vitabu vile kwa njia za panya lakini hatukufanya hivyo.

Tulivuta subra kuipa nafasi serikali ijitafakari na itambue inakabiliana na Waislam wa aina gani.

Serikali inatuelewa na inatuheshimu.
Inatambua matatizo yaliyomo ndani yake na inajitahidi kurekebisha.

Hili ni jibu kwetu la aina yake.
Juu ya haya bado tunasubiri majibu.
 
Mbona sikuelewi 🤣🤣point yako ipo wapi?

Niambie chuo cha kikristo mara sijui Harvard vyuo vipo vingi kwma huikubali Iran ni sawa ,siwezi kulazimisha

Kwa hiyo vyuo vya Iran havina reputation ?🤣🤣Ndio maana nimekuambia hao marafiki hauna na umeandika uongo mtupu hapo...Vyuo ni Harvard , OXFORD sio!?

Jaribu kutembea hata china hapo Dubai nenda hata Ethiopi ,Mali ,Egypt ,libya vipo vyup vikubwa tu level za mbele ....Akili yako nishaisomw tangu ulipoanza kutaja watu hakuna hicho kitu ni uongo.

Kwa hiyo turkey pawe na chuo cheny reputation halafu Iran pakosea chuo chenye reputation?

Chuo kinaweza kuitwa sir johnson na kisiwe cha kikristo haswa nchi kama uingereza hata hostel ziitwe Magufuli sio za wakristo ni jina tu ,chuo na shule za dini
Zinajulikana kuanzia utaratibu wao na hakuna bifu sisi tunasoma kokote..


Elimu ni fardhi hata uende nchi za mbali ni moja ya maamrisho yetu...


Waislamu hwachagui vyuo ila hawawezi kusoma kweny vyuo vyenye sheria za dini ya kikristo kama malezi yao...

Kuna Mtanzania juzi amesoma nje amegundua n kuvuna gesi je unajua kasomes chuo gani?
Okay.
 
Kuna wakati hatuhitaji kutumia lugha ngumu sana kufikisha ujumbe, kama chuo kipo na kinaendelea, basi tutakitambua kwa matunda yake huku mitaani basi. Kuongeza taasisi nyingine ni muhimu kama inahitajika, ila kama ni kushindana kwa kuonesha idadi tu, nalo ni jema tu. Matunda ya chuo ndo yatakipa hatima yoyote chuo chetu.
 
Geza...
Hili ndilo kwanza nalisikia.
Mimi si Mzaramo mimi Mmanyema.

Wala sijapata kumchukia mtu katika maisha yangu.

Sikuumbwa hivyo.
Alhamdulilah.

Huna la kusema kuhusu waraka niliokuwekea la ubaguzi?

Unadhani ningekosa radhi ya waalimu wangu pale chuoni ningeweza kufanya haya ya kuandika vitabu, research papers na kuzungumza katika Vyuo Vikuu Afrika, Ulaya na Marekani?

Au hujui kuwa kitabu cha Abdul Sykes mtu wa kwanza kukipitia alikuwa mwalimu wangu wa historia Prof. Fredrick Kaijage?

Hii ni dalili ya mwanafunzi dhaifu aliyekuwa akipewa alama za chini na walimu wake?

Mimi nina radhi ya waalimu wangu wote walionisomesha kuanzia darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu Dar-es-Salaam na Cardiff.

Nina radhi ya wazazi wangu.

Huwezi kunivunjia heshima yangu kwa maneno ya kipuuzi.

View attachment 2857222
Kulia: Dr. Ibrahim Msabaha, Prof. Emmanuel Bavu na Mohamed Said
View attachment 2857224
Kulia: Paul Sozigwa, Mohamed Said na Prof. Bavu Prof. Bavu alinitembelea nyumbani kwangu
Ulitaka kucheza karata za udini kupewa maksi! Kumbe Prof anafuata Maadili ya Taaluma! Uzuri hujabadilika itikadi za udini zipo palepale!
 
Ulitaka kucheza karata za udini kupewa maksi! Kumbe Prof anafuata Maadili ya Taaluma! Uzuri hujabadilika itikadi za udini zipo palepale!
Geza...
Hapana si kweli.

Unaweza hata wewe kwa kunisoma hapa ukajua uwezo wangu.

Nadhani unafahamu kuwa nimekuwa Mwandishi Bora hapa JF Jukwaa la Historia miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.

Bahati mbaya ametaka kunifedhehesha nami nimempa majibu.

Hakurejea tena.
Ama udini sina.

Nilichofanya nimetaka kuikoa historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Huu si udini.

Laiti ningekuwa mbaguzi nisingealikwa vyuo mbalimbali kuzungumza wala publishers kama Oxford University Press wasingenitia katika miradi yao na kuchapa kazi zangu.
 
Geza...
Hapana si kweli.

Unaweza hata wewe ukanipa kwa kunisoma hapa ukajua uwezo wangu.

Bahati mbaya ametaka kunifedhehesha nami nimempa majibu.

Hakurejea tena.
Wacha chuki za kidini tangu UDSM mpaka leo umeng'ang'ana tu?
 
Hata hivyo Morogoro Muslim University inamilikiwa na taasisi bimafsi inayoitwa African Muslim ambayo pia inamiliki taasisi kadhaa za kielimu kama mashule na vyuo.

Kinacho muuma ni taasisi ya mashia ile iliyopigwa chini,kwa sasa taasisi nyingi ni za sunni,hata bakwata imejaa suni,mashia wakina mzee mudy na nduguye ponda wana ile taasisi ya sura ya imam,hao ndio siasa kali radical muslims,ambao wanatamani hii nchi iwe chini ya sharia kali za kiislam,wanaochukia wakristo.

Huyu mzee ni terrorist symphathizer…vurugu zote za waisla hapa nchini huyo mzee ndio moja ya wapanga mikakati,vurugu za mwembe yanga,kuvunja mabucha ya wakristo magomeni,ku enforce watoto wakike washule kuvaa hijabu n.k
 
Mangungo II,
Naomba nikufunze uandishi na heshima katika mjadala.
Kwanza mjadala nia yake ni kuelimishana si kutoleana kejeli na jeuri.

Mathalani ungeweza kuandika hivi:
''Mzee angewahimiza Waislam kuwapeleka watoto shule.''

Hapo nimeondoa, ''Huyu Mzee.''

Sentensi ina maana ile ile iliyokusudiwa lakini kuna adabu na kuheshimiana.

Unasema, ''Haya makelele...''
Haipendezi si uungwana.

Mimi sipigi kelele na haiwezekani niwe napiga kelele kwa ilm ya somo hili ninavyoijua.

Nataka nikuambie kitu kuwa Waislam si kama unavyowaeleza.

Waislam wamepigania uhuru wa Tanganyika hadi umepatikana kwa salama.

Wameishi na Nyerere ndani ya majumba yao wakati Nyerere hana ndugu mjini Dar es Salaam.

Wametaka kujenga Chuo Kikuu 1968 serikali ikavunja taasisi yao.

Waislam si watu wa leo akasimama mtu ati anawaeleza umuhimu wa elimu na kuwapeleka watoto wao shule.

Hii ni kejeli kubwa.

Watu waliokuwa wanajenga Chuo Kikuu hawahitaji kuhimizwa kuhusu elimu.

Waislam tuna historia ya kutukuka na mimi nimeiandika na inasomwa kwingi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Nimeizungumza historia hii kwa mialiko katika Vyuo Vikuu na katika media ndani na nje ya Tanzania.

Nimeandika '' research papers'' kadhaa na zimechapwa katika academic journals.

Mimi niko hapa kazi niiyojipa ni kusomesha historia ya kweli ya nchi yetu ili watu waifahamu.

Hii ndiyo sababu nakuandikia maneno haya kutaka kukufanya ujaribu kusikiliza yale ambayo hukuwa unayajua.

Wewe unaandika uso wako umeuficha.
Mimi naandika jina langu linafahamika na uso na sauti yangu iko wazi.

Sijajificha.

Jiulize kwa nini sijajificha kisha jiulize wewe mwenyewe kwa nini unaogopa kutambulika unaficha uso wako na jina lako?
Unajifichia kwenye kichaka Cha uandishi wa heshima.

Huyo mzee Mwinyi sijatumia neno mzee pia nimetumia neno ALHAJ nayo ni neno ambalo humpa mtu "heshima"

Wewe kuwa mzee usitake kutufanya sisi vijana tuonekane si lolote si chochote na kwamba eti hatuna adabu Wala heshima. Hizo tabia za WAzee wapenda ubabe na kujikweza kwa mambo rahisi.

Mimi nitakuambia ukweli tu Sina haja kuongea kinafiki Wala kubembelezana. Ukiona unakejeli na jeuri Hilo ni tatioz lako binafsi, Mimi halinihusu. Ujumbe mujarabu niliokusudia niumefikisha.

Narudi Tena sambaza kampeni ya kuwaamhia waislamu wapeleke watoto shule Bora sio madrassa tu wapeleke watoto vyuo Bora sio kule M.U.M.

Halafu waje baadae waseme wanaonewa wakati hawafit demand iliyo kwenye skilled, semi-skilled, non-skilled labor.

Nakuheshu sana kwa umri wako wa miaka 60 ila nikuambie usitake kutumia kigezo Cha umri wako kulazimisha hoja zako zikubalike hata kama Zina UKAKASI.

Waambie wenzio katika Imani wapeleke watoto shule na vyuo Bora.

Huwezi ukawa unashikilia mambo ya kale sijui TULIONEWA hivi na vile. Why kwanini Sasa usipige kampeni kweli kweli Ili hii jamii Yako huko mbele iwe na dominance kubwa kwenye hayo mambo mnayoyataka. Fursa mnazo Sasa ila mnakalia mambo ya kale yatawasaidia Nini!?.
 
Unajifichia kwenye kichaka Cha uandishi wa heshima.

Huyo mzee Mwinyi sijatumia neno mzee pia nimetumia neno ALHAJ nayo ni neno ambalo humpa mtu "heshima"

Wewe kuwa mzee usitake kutufanya sisi vijana tuonekane si lolote si chochote na kwamba eti hatuna adabu Wala heshima. Hizo tabia za WAzee wapenda ubabe na kujikweza kwa mambo rahisi.

Mimi nitakuambia ukweli tu Sina haja kuongea kinafiki Wala kubembelezana. Ukiona unakejeli na jeuri Hilo ni tatioz lako binafsi, Mimi halinihusu. Ujumbe mujarabu niliokusudia niumefikisha.

Narudi Tena sambaza kampeni ya kuwaamhia waislamu wapeleke watoto shule Bora sio madrassa tu wapeleke watoto vyuo Bora sio kule M.U.M.

Halafu waje baadae waseme wanaonewa wakati hawafit demand iliyo kwenye skilled, semi-skilled, non-skilled labor.

Nakuheshu sana kwa umri wako wa miaka 60 ila nikuambie usitake kutumia kigezo Cha umri wako kulazimisha hoja zako zikubalike hata kama Zina UKAKASI.

Waambie wenzio katika Imani wapeleke watoto shule na vyuo Bora.

Huwezi ukawa unashikilia mambo ya kale sijui TULIONEWA hivi na vile. Why kwanini Sasa usipige kampeni kweli kweli Ili hii jamii Yako huko mbele iwe na dominance kubwa kwenye hayo mambo mnayoyataka. Fursa mnazo Sasa ila mnakalia mambo ya kale yatawasaidia Nini!?.
Mangungo...
Hapana sijajificha popote si hapa JF au penginepo.

Nafahamika kwa jina langu halisi na kwa picha na sauti.

Wewe ndiye uliyejificha.

Hakuna anaekujua kwa sura au kwa jina lako halisi na pengine haya ndiyo yanayokufanya ukawa ''jasiri'' kuandika kama hivi uandikavyo.

Kama kweli wewe ni hodari na shujaa jitokeze kama nilivyojitokeza mimi.
Kuhusu wewe kuniambia mimi ukweli.

Ukweli gani utakaokuwanao wewe ushindane na ukweli wangu?

Mimi nimeandika kitabu cha Abdul Sykes kimebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika achilia mbali kubadili historia ya Julius Nyerere.

Kitabu kinakwenda tolea la tano sasa toka kitoke 1998.

Mimi kitabu changu kipo katika Cambridge Journal of African History na kimepitiwa na wasomi mabingwa wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.

Nimekizungumza kitabu hiki Northwestern University, Chicago, USA.
Hawa ndiyo mabingwa wa African History ulimwenguni.

Mimi ni mmoja wa waandishi 500 ulimwenguni walioandika Dictionary of African Biography (DAB) mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York (2011).

Ukweli gani utakuwanao wewe ambao utaandika uchapwe na kusomwa Vyuo Vikuu?

Niwaambie Waislam wapeleke watoto shule.
Mimi nikizungumza maneno hayo nitaonekana hamnazo.

Wewe utasamehewa kwa kuwa huna ulijualo.

Mwaka wa 1962 Sheikh Hassan bin Ameir aliitisha Muslim Congress na agenda ilikuwa elimu.

Azimio la mkutano huu ilikuwa EAMWS kujenga shule Tanganyika nzima na Chuo Kikuu.

Historia ya Chuo Kikuu sina haja ya kuirejea tena hapa.

Serikali iliipiga marufuku EAMWS na Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa na kufukuzwa Tanganyika BAKWATA ikaundwa.

Leo 2024 unasema niwaambie Waislam wapeleke watoto shule.

Unadhani hawajui faida ya elimu watu waliokuwa wanajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968?

Unasema MUM si chuo cha maana.
Sikushangai.

Unazungumza kuhusu hoja.
Unajua nimeandika ''research papers'' na vitabu vingapi?

Unajua kwa siku ninaandika maneno mangapi?

Unajua nimechapa makala ngapi katika majarida ya kimataifa na hapa nyumbani?

Mambo ya kale yapi?

Waislam wamefanya maandamano dhidi ya dhulma za NECTA mwaka wa 2012 na baada ya maandamano yale haki ikapatikana.

Ushahidi uliofikishwa serikalini ulitosheleza.

1704338259763.png

1704338319734.png

1704338392734.png

Northwestern University, Evanston, Chicago​
 
Nya...
Umekusudia African Muslim Agency ya Kuwait?

Hawa ndiyo wanaendesha shule za sekondari.

Kuhusu MUM historia yake inafahamika.
Fanya utafiti kidogo utajua.

Bahati mbaya sana wengi wenu hapa mnadhani mnajua kumbe hamjui na mfano mzuri ni kama hivi.
Hawa African Muslim Agency ndo wamiliki na wanaoendesha MUM.
Nina uhakika kutoka kwao wao wenyewe baada ya kuhudhuria kikao cha Bodi.
Bakwata hawana chao tena pale
 
Mtume Muhammad ndie aliwarudisha nyuma kielimu waarabu na waislamu baada ya kuamuru vitabu vyote vichomwe ibaki Quran peke yake. Enzi hizo waarabu walikuwa mbele kisayansi kuliko wazungu.
 
Back
Top Bottom