Upandikizaji wa kwanza wa uume wafanywa na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Hospitali ya Chuo Kiku cha Aga Khan imesema imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katikakanda ya Afrika mashariki na kati .

Upasuaji huo maalum umefanyiwa kwa mwanaume katika umri wa miaka ya 40 ambaye alikuwa na hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari, kwa kitaalamu Erectile dysfunction (ED) tatizo ambalo limemsumbua kwa miaka kadhaa kulingana na taarifa ya hospitali hiyo .

Tatizo hilo hutokea wakati ambapo mwanaume hawezi kushiriki katika tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo na mgonjwa huyo alikuwa amepokea aina nyingine za matibabu bila hali yake kuboreka .

‘Upandikazaji huu huchukua takribai saa moja na unahusisha kuweka kifaa maalumu (Prosthesis) ambacho kinapachikwa kwenye uume na kumwezesha mtu kufanya tendo la ndoa wakati wowote bila kuhitajika kutumia dawa nyingine’ amesema Dkt.Ahmed Yousef aliyeongoza upasuaji huo.

Upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda huu kwa sababu unahitaji utaalamu wa kipekee na ufahamu wa kitengo cha tiba ya Urolojia.

Inakadiriwa kuwa asilimia 15-20 ya wanaume wana matatizo ya Erectile dysfunction (ED) na mshindo wa mapema(Premature Ejaculation) na wengi wanateseka kimya kimya kwa sababu ya hali hizo.

Chanzo: BBC
 
Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa mwanaume wa miaka 40 ambaye alikuwa hana urijali 'Erectile dysfunction (ED) tatizo ambalo hupelekea mwanaume kushindwa kushiriki tendo la ndoa.


Source: EastAfricaRadio

FL3NcDCX0AA-FK-.jpg
 
NADHANI SASA IDADI YA MASHOGA ITAPUNGUA NA ILE YA TRANS GENDER ITAONGEZEKA ZAIDI
 
"Tatizo hilo hutokea wakati ambapo mwanaume hawezi kushiriki katika tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo"

Hapa wahanga ni vijana wengi wanaoshindia chips wapunguziwe bei tu wakapandikizwe
 
Back
Top Bottom