Kumbukumbu 2014: Tea Said Tewa (1924 - 1998)

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,906
30,247
KUMBUKUMBU: TEWA SAID TEWA (1924 - 1998)

Tewa Said Tewa ni mtoto wa Dar es Salaam.

Mimi nimekuwa nikimuona toka utoto wangu na kumbukumbu zangu za awali kabisa za Tewa Said Tewa ni kumuona Mtaa wa Pemba akiwa ndani ya gari lake la Kiwaziri Humber nyeusi.

Nilikuja kumfahamu vizuri sasa mimi nishakuwa mtu mzima na nikawa karibunae sana kiasi alinieleza historia yake yote ya maisha yake katika siasa kuanzia kuupigania uhuru hadi alipokuwa waziri na mwisho wa kuangushwa kwake kutoka uongozi.

Mzee Tewa akawa mwalimu wangu katika kuzijua siasa za Dar es Salaam ya mwaka 1950 wakati wa kudai uhuru na siasa zilizokuja kutamalaki baada ya uhuru kupatikana.

Tewa Said alikuwa na umbo la kupendenza na sura jamil.
Tewa Said alikuwa mvazi mzuri.

Tulikuwa tukikaa kwenye veranda yake nyumbani kwake Magomeni Mikumi akinifungulia album yenye picha zake akiwa kijana wakati waziri wa serikali, balozi China na Rais wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS).

Nilipendezwa na zile suti zake.

Picha zake kwa jumla zikimwonyesha katika baraza la kwanza la mawaziri na picha nyingine akiwa katika shughuli tofauti.

Hakika ukItazama picha zile utasema ule ulikuwa wakati wa enzi zake.

Alipofariki dunia mwaka 1998 mimi sikuwapo Dar es Salaam nilikuwa nje ya nchi kwa hiyo sikuhudhuria maziko yake.

Kitu cha kushangaza ni kuwa kwa kile kipndi cha takriban mwezi mmoja nilipokuwa sipo Tanzania watu maarufu watatu waliopigania wa Tanganyika walifariki kwa kufuatana mmoja baada ya mwingine, Dossa Aziz, Zuberi Mtemvu na Tewa Said Tewa.

Kwa haraka niliporejea nchini nilipitia magazeti kuangalia taazia zilizoandikwa kuhusu watu hawa.

Nilisikitika sana kwani hapakuwa na taazia yoyote ya maana na aliyeandikiwa taazia alikuwa mmoja tu nae ni Dossa Aziz na walioandika taazia ile ilioenesha walikuwa hawamjui Dossa.

Zuberi Mtemvu na Tewa Said hawakuandikiwa taazia yoyote.
Nilinyanyua kalamu na kuwaandikia taazia stahili yao hao wote na zote zilichapwa katika magazeti.

Hawa wote walikuwa wazee wangu wakinifahamu si mimi tu bali hata wazazi wangu.

Tewa ni mmoja katika wale wazalendo 17 walioasisi TANU lakini katika picha ile maarufu ya waasisi wa TANU yeye na Ally Sykes hawamo.

Sababu ya kutokuwepo kwao ni kuwa wao walikuwa wanyakazi wa serikali na kuna na Government Circular No. 5 ya serikali ya kikoloni hawakuwa na ruhusa ya kujiingiza katika siasa.

Tewa ni kati ya watu wa mwanzo kumpokea Nyerere na kufahamiana na Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka wa 1952.

Tewa alikuwa mwanachama wa kikundi kilichojiita Wednesday Tea Club ambacho kiliwajumuisha vijana wa wakati ule waliokuwa katika TAA na kazi kubwa ya kikundi hiki ilikuwa kukutana nyumbani kwa Abdulwahid au Dossa kila siku ya Jumatano kunywa chai pamoja na kupiga siasa.

Kwa ajili hii Tewa alishuhudia yote katika harakati za kudai uhuru kwa macho yake si kama mtazamaji bali kama mchezaji wa kikosi cha kwanza.

Mzee Tewa akinihadithia habari za Julius Nyerere anasema kuwa alifuatwa na Abdulwahid Sykes usiku nyumbani kwake Mtaa wa Pemba siku moja kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa TAA wa mwaka 1953 uliomwingiza Nyerere katika uongozi wa TAA.

Tewa anasema Abdulwahid alikwenda kwake kwa minajili ya kuzungumza kuhusu uchaguzi ule ambao yeye Abdulwahid Sykes alikuwa anapambana na Nyerere.

Jinsi mipango ilivyokuwa imepangwa uchaguzi ule ilikuwa sawa na kukamilisha ratiba ya mkutano tu kwani viongozi wa juu wa TAA, yeye mwenyewe Abdulwahid, Ally, Dossa na John Rupia walikuwa wamekubaliana kuwa Nyerere apewe nafasi ile kwa Abdulwahid kumpisha kiti.

Mara nyingi sana Mzee Tewa kila tukizungumza habari za Nyerere na TANU alikuwa akikirudia kisa hili kama vile kasahau kuwa alinishanieleza.

Tewa anasema, “Abdulwahid alikuja kwangu usiku na akaniambia kuwa Tewa, kesho tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka ya kuendesha nchi hii.
Kuanzia hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna namna tena ya kumnyang’anya madaraka tuliyompa.

Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini kila kitu kitakwenda sawa.”
Mzee Tewa alikuwa akisema kuwa, “Abdulwahid ndiye aliyechelewesha kuundwa kwa TANU.

Ilikuwa TANU tuiunde toka 1950 na tungefanya vile Nyerere asingetuwahi angekuwa keshachelewa lakini Abdu kwa miaka minne mfulululizo alikataa kuitisha mkutano wa TAA hadi 1954.

Kila tukimwambia habari ya mkutano anasema, "Tusubiri mambo bado.”
Mzee Tewa alikuwa mwalimu wangu na hivi niandikapo ni kama vile namuona na mimi kama mwanafunzi anaetaka kuonekana hodari sikuacha kumvurumishia maswali.

Nilimuuliza,“Hivi baba inawezekanaje mtu mmoja akasimamisha kuitishwa kwa mkutano wa chama?”

Mzee Tewa alinijibu kwa kusema, “Abdu alikuwa na akili sana na sisi sote tukimtegemea yeye katika uendeshaji wa chama lakini kikubwa zaidi ni kuwa tukimtegemea zaidi katika kufadhili mambo mengi ya chama.

Sasa yeye akisema tusubiri ilibidi iwe hivyo. Hawa akina Sykes katika TAA na TANU walikuwa na nguvu sana maana licha kuwa viongozi walitoa fedha zao kupambana na Waingereza na hilo toka enzi ya baba yao.

Tewa Said baada ya kupatikana uhuru mwaka wa 1961 na sasa akiwa waziri wa serikali, mwaka wa 1962 alishiriki katika kuitisha mkutano uliokujajulikana kama Muslim Congress.

Tewa Said alihusika sana katika kufanikisha mkutano huu.

Mkutano huu ulihudhuriwa na jumuia zote za Kiislam zilizokuwapo wakati ule kama East African Muslim Welfare Society (EAMWS), Daawat Islamiyya, Jamiatul Islamiya fi Tanganyika na Muslim Education Union.

Mkutano huu uliamua pamoja na mambo mengine kuanzisha idara ya elimu chini ya EAMWS. Mkutano huu ulitayarisha mipango ya kujenga shule Tanganyika nzima na mwishowe kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya Mashariki.

Mkutano ule ukamchagua Tewa Said Tewa kuwa mwenyekiti wa EAMWS kwa upande wa Tanganyika.

Kwa kitendo hiki nyota ya Tewa ikazidi kung’ara si Tanganyika tu bali Afrika ya Mashariki nzima.

Wenzake katika harakati hizi maarufu sana alikuwa Badru Kakunguru wa Uganda na Prince Karim Aga Khan.

Lakini Mzee Tewa alinieleza ushindi ule wake na usuhuba wake na watu mashuhuri kama hawa ukaja kumsababishia matatizo makubwa baadae.
Nakumbuka kama jana vile siku Mzee Tewa aliponieleza kisa hiki.

Alinyanyuka pale tukipokuwa tumekaa akaingia chumbani kwake akatoka na jalada akanikabidhi akisema, “Mohamed haya niliyoandika humu sijamwonyesha yeyote wewe utakuwa mtu wa kwanza kusoma maisha yangu ya siasa.

Tafadhali nenda na jalada hili kasome kisha unirudishie.”

Iko siku kaja mtu kwangu akanambia, “Mohamed, Mzee Tewa anasema anakupenda sana na akashangaa anasema hayo mapenzi yake kwako ni maajabu ya Mwenyezi Mungu kwani yeye na baba yako hawakuwa na mkabala mwema toka utoto wao lakini ajabu wewe mwanae umekuja kuwa rafiki yake.”

Maneno haya aliyasema Mzee Tewa alipofikishiwa habari za kifo cha baba yangu na huyu mpashaji habari wangu.”

Nilisoma lile jalada na kwa kweli niliyokuta mle yalinikosesha raha sana.

Nilianza kumtazama Mzee Tewa sasa kwa sura nyingine kabisa na mapenzi yangu kwake yakazidi kupita kiasi.Ikawa sasa nimepata tafsriri halisi ya maneno, “siasa ni mc mchezo mchafu.”

Mzee wangu Ahmed Rashad Ali yeye akiongeza akisema,”Jinsi unavyokuwa mchafu zaidi ndiyo unavyokuwa bingwa.”

Insha Allah iko siku nitakuja andika na kuyaweka wazi kwa ajili ya faida ya kizazi kijacho mengi alonambia Mzee Tewa na yale niliyosoma katika lile jalada lake alilonipa.
Mwaka 1964 Tewa Said Tewa aliongoza ujumbe wa EAMWS akifuatana na Mufti wa Tanganyika na Unguja Sheikh Hassan Bin Amir na Sheikh Said Omar Abdallah, maarufu kwa jina la Mwinyibaraka (Mwinyibaraka alikuwa msomi wa Chuo Cha Oxford, Uingereza), Aziz Khaki na wengineo wakafanya ziara ya nchi za Kiislam na walionana na Gamal Abdi Nasser ambae aliwapa msaada wa kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam, Tanzania.

Huyu Aziz Khaki alikuwa mtu muhimu sana katika EAMWS yeye alikuwa katibu lakini zaidi alikuwa kama mwakilishi wa Aga Khan ndani ya jumuia hiyo.
Mwalimu Nyerere alialikwa katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu na yeye kwa mkono wake ndiye aliweka jiwe lile akiwa katika ya Tewa Said Tewa na Sheikh Hassan bin Amir.

Sherehe ilikuwa kubwa na mabalozi wa nchi zote za Kiislam walihudhuria sherehe ile.

Haukupita muda Tewa Said Tewa Nyerere akamtoa Tewa katika baraza la mawaziri na kumfanya balozi wa Tanzania China. Hii ilikuwa mwaka 1965.
Tewa inaelekea hakuipenda nafasi ile akajiuzulu na kurudi nyumbani kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka ule.

Katika uchaguzi ule wa mwaka 1965 ambao Bibi Titi aligombea wote Bi Titi na Tewa walianguka tena kwa kushindwa na watu ambao wala hawakuwa maarufu wala hawakuwa na nguvu yoyote ya siasa.

Bibi Titit alibwagwa na mtu mmoja akijulikana kama A. M. Mtanga na Tewa akaangushwa na mtu aliyeitwa na Ramadhani Dollah.
Huyu Dolla alikuwa mbunge kwa kipindi kimoja uchaguzi wa 1970 aliangushwa na mwisho aliishia jela.

Baada ya kishindo kile Tewa sasa akajikita katika kuhakikisha kuwa anafanikisha ujenzi wa Chuo KIkuu Cha Waislam.

Lakini hakufanikiwa kwani ghafla akajikuta yuko katikakati ya kile kilichokujajulikana kama “mgogoro wa EAMWS wa mwaka 1968” mgogoro ambao ulidumu kwa takriban miezi mitatu na mwishowe serikali ikakipiga chama kile marufuku na Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa usiku wa manane kurudishwa kwao Unguja na BAKWATA ikaundwa kushika nafasi ya EAMWS.

Ujenzi wa Chuo Kikuu na mradi wa kujenga shule za msingi na sekondari ambazo Tewa alikuwa akizisimamia chini ya EAMWS vyote vikafa.

Kwa kipindi kirefu kuanzia mwaka 1968 Mzee Tewa aliishi maisha ya upweke hadi miaka ya 1990 kwa sababu ya mwelekeo mpya wa siasa Mzee Tewa alianzisha taasisi iliyokuja kujulikana kama Muzdaliffa Muslim Academy iliyokuwa na makao yake makuu Msikiti wa Manyema, Dar es Salaam.

Kipindi cha miaka ya 1990 kilikuwa kipindi kigumu kwa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi kuliibuka migogoro mingi ya kidini. Sasa watu waliopata kuwa viongozi katika taasisi za dini walijaribu sana kutoa michango jinsi ya kuyaendea haya matatizo.

Mzee Tewa alijitokeza sana katika kutoa mchango wake.

Mwaka 1991 Kanisa Katoliki katika kuadhimisha miaka 25 ya “World Peace Day” walifikisha salamu zilizotoka kwa Papa na aliyezfikisha salamu zile kwa Waislam wa Tanzania alikuwa Balozi wa Papa Tanzania, Monseigneur Agostino Machetto akifuatana na Secretary of the Apostolic, Father Gabriele Gaccia na Father Peter Smith.

Tewa Said Tewa ndiye aliyepokea salamu hizi kwa niaba ya Waislam wa Tanzania. Picha za sherehe hii ilipamba magazeti yote.

Inaelekea Tewa Said Tewa hakuwa na bahati na uongozi mara zikatokea vurugu za kuvunjwa mabucha ya nguruwe mjini Dar es Salaam na serikali ikapiga marufuku taasisi zote za Kiislam isipokuwa BAKWATA na Tewa akarudia tena maisha yake ya upweke.

Mara nyingi nilipokwenda nyumbani kwake kumsalimia nilimkuta mnyonge na mwenye fikra lakini hakuacha kuniombea dua na kunihimiza nisiwache kumtembelea.

Akiwa katika hali kama hii siku moja akanipa jalada lingine nikasome.
Nilipigwa na butwaa. Mzee Tewa alikuwa amefasiri kutoka kwa Kiingereza kuja Kiswahili “Homer” na “Ulysses.”

Mzee wangu Tewa Said Tewa alipofariki nilikuwa niko nje ya Tanzania na habari za kifo chake kilifikia kwa wakati.

Nilisikitika sana hasa nikikumbuka nyakati nilizokuwanae faragha pale nyumbani kwake Mikumi akinisomesha siasa za nchi yetu na kunihadithia madhila yaliyomkuta kwa ajili ya kuutumikia umma kwa uadilifu.

Miaka miwili iliyopita nilikuwa naandika kitabu na nikahitaji picha.

Nilipokwenda kuwaona watoto na wajukuu wa Mzee Tewa kuomba picha hakuna aliyekuwa anajua maktaba ya mzee wao iko wapi.

Nilionyeshwa picha moja tu ya Tewa iliyotundikwa ukutani iliyopigwa Makka mwaka wa 1964 wakati Tewa alipokwenda hija.

Nilijaribu kuwaongelesha kuhusu mzee wao na kwa masikitiko makubwa nilikuja kubaini kuwa vijana wale hawakuwa wanajua chochote kuhusu huyu shujaa wa uhuru wa Tanganyika.

Mohamed Said
6 Oktoba 2011

1657028626054.png
 
View attachment 2281861
Shukran

Sent from my SM-G935T using JamiiForums mobile app
 
Asante sana Mzee Mohamed kwa kutujuza habari za wazee wetu.
 
Shukrani kwa kidogo hiki kumuhusu Mzee wetu Tewa Said;Tulikosea sana kumruhusu mkoloni aliyetutawala kutuandikia Historia ya nchi yetu sababu aliandika wale waliokuwa na manufaa kwake na wengine ambao ilibidi wawemo waliandikwa juu juu na hawakuandikwa vya kutosha kwa waliyoyafanya.
 
Ahsante umemuelezea vizuri shujaa wetu hakika ni watu wa kuenziwa.
 
nasoma mara nyingi makala zako za kutuelimisha sisi vijana,ninapata vitu vingi shukran sana kwa elmu unayotoa

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom