displayname
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 1,972
- 1,091
Hapo ndipo watakubali kwamba kila kitu kitapita lakini NENO litasimama!!666
Kitabu cha ufunuo kimeandika kila kitu hakutakwepo na kuuza wala kununua bila microchip
Kwa ufupi tu kuhusi microchip,
Ndio kifaa pekee kinachoweza mtambua mtu kwa taarifa zake na kumpa uwezo wakuaccess vitu kadha wa kaza kama huduma za bank, simu nk.
Hizo chips hata sasa zipo na zinatumika na almost watu woote tunazo na twazitumia tofauti ni kwamba sasa hakuna kulazimishana pia kwa sasa hazijawekwa kwenye miili yetu (nitaeleza itakavyoanzwa wekwa katika miili yetu)
Kadi za benk zina hiyo chips ukienda katika atm pale kinachokufanya wewe uweze toa pesa ni taarifa zako ambazo zimewekwa katika hiyo chip. Hali kazalika na simu ipo hiyo chips ila mwaita simcard, ni taarifa zako zakupa nafasi ya kutambulika. Mwakumbuka tulishurutishwa sajiri namba za simu....
Kuhusu kuanda tumika kwa hizo microchip kwenye miili yetuu hasa katika mkono na paji la uso. Nilipata fika nchini Uholanzi (wenyeuzoefu na nchi za wenzetu mtakubaliana na mi) wenzetu matumizo ya pesa kwa maana ya kuishika "cash" yamepungua na yanazidi pungua saana. Wao wana kadi za zao za benki iwe mastercard au visa etc. Hivyo wanaaccess na kuzitumia pesa pasipo kuzishika akipanda treni au bus au tax ana swap tu kadi yake na pesa inakatwa juu kwa juu. Hata akienda kula hotelin au kulala au supermarket au hospitali mtindo ni ule ule wakuto kushika pesa ni mwenendo wa kadi tu.
Inakujaje sasa kuanza tumika microchips kwa kuwekwa katika miili yetu. Kama unavyofahamu kadi za benki hupotea aidha kwa kuanguka, kuibiwa kuungua nk. Hivyo njia salama ya kuepukana na usumbufu wa kupoteza kadi na kwenda kufuatilia sijui polisi kisha benki husika. Kuepuka hayo utaanzishwa utaratibu ambao ni mzuri machoni mwa adha ya upotevu, nikimaanisha watasema tekenolojia imekua ili kuepuka kupotea kwa kadi na kukosa huduma muhimu kwa wakati basi tunaweka hiyo chip ambaya ni kadogo kama punje ya mchele (hiyo katika picha ni kubwaa kweli sijui ni version ipi ya chip hizo) hivyo wengi watapenda huduma hiyo ya kuweka microchip kwenye mkono au paji la uso. Na hasa paji la uso, ili ukifika katika atm badala ya kuangaika sijui kuingiza kadi neno siri hapo wewe utakuta kamera/kifaa kitakachotoa mwanga ukikitazama au gusa na mkono wenye hiyo chip ndipo atm itakupa option ya kiasi cha pesa utakazo. Halikazalika katika kupanda treni au magari au madukani hospitali. Utakutana na mashine kama zile za supermarket mhudumu atamulika sehemu iliyopo hiyo microchip kama bakoni nayo itakutambua na kuruhusu lipa kiasi cha pesa ulichotumia.
Hivyo mwisho wa siku mfumo wa kushika pesa tena hautakuwepo, tutakuwa na pesa katika hali tete yaani ( softcopy au electronic).
Na hapo ndipo ukienda dukani au popote ukitaka huduma kama huna hiyo chip mzee imetafuna kwako... watakwambia "no services" itakuwa hata utakapopeleka sandalusi lenye pesa hawatokuhudumia.
Hapo ndipo utakuja amini kama kitabu cha Mwanzo kipo basi Ufunuo kutimia ni lazima!
Na wasilisha;
#displayname