Tatizo kubwa la nchi hii Siasa imeingia kila mahali, na isitoshe Wanasiasa wanaingilia sana uhuru wa mahakama , Ikiwa Hakimu kama huyu anafanya kwa utashi wa kisheriani sawa, lakini inapotokea kuwa Hakimu anafanya hivi kuwafurahisha wanasiasa hilo ni jambo baya sana na ni Hatari kwa Usalama wa Taifa. Hizi mahakama zetu kwanza zimejaa rushwa, Wananchi wananyimwa haki zao, serikali inatambua na kila siku inapiga kelele Kuwa mahakama inanuka rushwa lakini bado inaikumbatia, Na hakuna linalofanyika, Mfano ukifika baadhi ya Mahakama dau la rushwa liko wazi hawaangalii chohote wanakueleza kabisa mheshimiwa fulani bila kiasi fulani hajamaliza mambo!!! TAKUKURU inafanya nini?
Tusike mahali tubadilike siyo kila kitu tunashabikia kwa sababu ya UCCM na Uchadema Maslahi ya nchi kwanza.
AMANDLA.
ALUTA!!!