Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Ni kweli alikuwa Nyegezi( NSTI wakati huo). Haikuwa 1997 bali 1990. Alikuwa anasoma diploma ya Journalism. ShyRose sasa hivi atakuwa amenusa 40 au zaidi.

Kwani kuwa mjumbe wa UVCCM lazima uwe na vigezo gani?
Yeye anasema ni Kamanda wa vijana kama alivyo Kingunge na Pinda wiki hii kapewa nae ukamanda kwao Mpanda.
 
Masauni hakuwa chaguo la JK wala Ridhiwani. Hawa baba na mwanae walimtaka Beno Malisa, rafika wa karibu wa Ridhiwani, ili wawe wanatawala wao kupitia mgongoni. Baada ya kampeni kali kati ya kundi lao na la Hussein Bashe, ndipo ikafanyika 'compromise' na kuwaweka Malisa na Bashe wagombee u-Makamu na Masauni wa waZenji wenzake wawili wagombee Uenyekiti.

Kwenye mkutano wa uchaguzi kule Dodoma kampeni kali zilikuwa kati ya Malisa na Bashe, na waliteka wajumbe wengi. Ilikuwa wazi kuwa atakayechaguliwa kati ya Malisa na Bashe basi atakuwa anaungwa mkono na wajumbe wengi na atakuwa na nguvu kuliko Mwenyekiti wake.
Hata kwenye uongozi wake imeonekana wazi kuwa Malisa na Ridhiwani wanam-sideline 'Mwenyekiti' Masauni kwenye events, mfano ile ya Arusha.

Hivyo Masauni alichaguliwa kwa matumaini kuwa atasema 'asante Mzee Kikwete' na atakuwa 'yes man' kwa Ridhiwani. Hilo ameligomea, hivyo wameibua hoja ya umri, ambayo kwa UVCCM wengi wapunguza umri wao ili wapate madaraka ndani ya UVCCM.
Na kama kawaida yaonekana Mzee JK na Ridhiwani wanamtumia Mzee Makamba kuleta fitina...

Au kama vp turudishe ASP, vijana wawe ASPYL (ASP Youth League), na Bara iendelee na UVCCM ya Vikwete...

Ule mpasuko alioubashiri unatimia sasa, movie inaendelea hii habari ni muendelezo wa upinzani ndani ya CCM baina ya CCM mafisadi na CCM wa nyerere au wanaowapinga mafisadi. Huyu kijana inadaiwa yuko upande wa wasiokuwa wanataka mafisadi sasa anaonekana atakuja kuwa kikwazo kwa CCM.
 
bravo kaka. yaliyotabiriwa na wenye uchungu na nchi sasa yatatimia?ni jambo la kusubiri na kuona.
 
Kwani kuwa mjumbe wa UVCCM lazima uwe na vigezo gani?
Yeye anasema ni Kamanda wa vijana kama alivyo Kingunge na Pinda wiki hii kapewa nae ukamanda kwao Mpanda.
Nafasi zote za kuchaguliwa UVCCM ni lazima uwe chini ya miaka 35 wakati unagombea. Makamanda wa vijana wa CCM sio wajumbe wa vikao hivi.
 
MS yeye akili waga anayo sema tu anazidiwa na mapenzi au atakuwa na chuki binafsi,ktk hil la UvCCM mi namuunga mkono JMK kwa kupangua migogoro huu wa sasa cha mtoto.
 
bravo kaka. yaliyotabiriwa na wenye uchungu na nchi sasa yatatimia?ni jambo la kusubiri na kuona.

Inasemekana CCM zanzibar wanasema kuwa wanakusudia kumsusia Kikwete zanzibar na kwa kweli mwaka huu kama uchaguzi utafanyika kikwete anaweza kupatwa na bumbuwazi wa jinsi kura atakazozipata zanzibar. Mkuu kaya kuna fununu zinasema anataka kuhakikisha anashinda zanzibar kwa vyovyote lakini hana support ya CCM zanzibar kwani hawamtaki.
 
Nimjuavyo Jk Tangu achukue uenyekiti ndani ya CCM na Urais wa Tz, Mgogoro wa Uvccm uliopo sawa na gunia la usufi na sio chuma, yaani ni mwepesi kwake kuutatua, ataumaliza na utaisha salama salmin. 1) mgogoro wa SS na Lowasa and Rostam, Ameutatua 2) Zanzibar sio nchi. sasa kama hadithi, kautatua 3)tUCTA, nayo huo umeyayuka bila hata mabomu ya machozi 4)waraka wa wakatoliki na waislam. ameutatua na sasa kila kiongozi wa dini wamemkubali anaebisha asubiri wiki chache zijazo
Hakika quinine na muarobaini si dawa sahihi ya hii malaria sugu!!!....jamani tusaidizane dawa nyingine ipi nzuri yasije panda kichwani!!
 
Kwenye hizi picha za wajumbe mbona naona kuna vijeba wa umri? Kina Shy Rose Bhanji ni teen wa miaka mingapi? Kweli natamani nipate vyeti vya kuzaliwa vya baadhi ya watu halafu nipate zile kadi za mama zao na zao za clinic !!! Yaani tafadhalini, tuwe wakweli?

Ila ni shangwe kubwa sana hii, ni ushindi kwa watanzania ni kwa vile tu wengi tunatishiwa nyau na hatutaki kuamka!! Hiki Chama hakitatufikisha popote zaidi ya kuendelea kutujengea classes za walio nacho na wasio nacho, watoto wa vigogo na watoto wa walala hoi. Wote huu ni upuuzi!!! Ule umoja wa kitaifa unapotea sasa!!!

UVCCM nao unaongozwa kwa remote control!!! Ndoto za kambi ya Ben Malisa zimetimia!!! Ridhiwan J.K hoyeeeeeeee, umeshinda!!!
 
Nimjuavyo Jk Tangu achukue uenyekiti ndani ya CCM na Urais wa Tz, Mgogoro wa Uvccm uliopo sawa na gunia la usufi na sio chuma, yaani ni mwepesi kwake kuutatua, ataumaliza na utaisha salama salmin.
1) mgogoro wa SS na Lowasa and Rostam, Ameutatua
2) Zanzibar sio nchi. sasa kama hadithi, kautatua
3)tUCTA, nayo huo umeyayuka bila hata mabomu ya machozi
4)waraka wa wakatoliki na waislam. ameutatua na sasa kila kiongozi wa dini wamemkubali

anaebisha asubiri wiki chache zijazo
MS,kwa nini usikishauri chama chako wabadili katiba ili kumfanya Mwenyekiti wa maisha maana uongozi wa chama atakuwa anauweza sana na hakuna linalomshinda. Utakuwa umekifanyia chama chako msaada mkubwa.
 
Siijui katiba ya CCM na UVCCM lakini nataka kujua JK amehudhuria kama nani? Mwenyekiti wa CCM ambaye ni mlezi wa UVCCM? Mwenyekiti wa CCM ni mlezi wa vyama vyote vya CCM ikiwemo UWT? Au ndio kuonyesha kuwa anajali vijana? Au ni kwenda kuchochea mgawanyiko? Kwa maoni yangu JK angekuwa na busara asingeenda huko kwa sababu mwanae ndio mchochezi wa yote hayo kama inavyodaiwa; basi kwenda kwake ni kumpigia debe kijana wake awe mwnyekiti wa UVCCM.
 
daah! niliwahurumia sana jana hwa vijana
lakini pia inaonekana mwenye nchi hakuwa anawapenda
 
kikwete hakuwa msaada wowote
yeyey na mwanae lao moja hakuna kitu hapo
 
Wewe Malaria Sugu vipi umelogwa?????

Ametatua mgogoro upi???????? Nenda katibiwe hiyo malaria itakuuwa
 
Je ni Kweli alighushi vyeti vyake vya kuzaliwa, jamani hili si ni kosa la Jinai au. Sasa kwa nini Jeshi la Polisi lisimkamate na Kumfungulia Mashtaka
 
Je ni Kweli alighushi vyeti vyake vya kuzaliwa, jamani hili si ni kosa la Jinai au. Sasa kwa nini Jeshi la Polisi lisimkamate na Kumfungulia Mashtaka

Wangelianza kuwakamata akina mkulo, Mathayo, Nchimbi na wengineyo kabla ya kumkamata huyu kijana au sheria za Tanzania zinawahusu watu fulani tu wengine wanakuwa exempted???
 
Nimjuavyo Jk Tangu achukue uenyekiti ndani ya CCM na Urais wa Tz, Mgogoro wa Uvccm uliopo sawa na gunia la usufi na sio chuma, yaani ni mwepesi kwake kuutatua, ataumaliza na utaisha salama salmin.
1) mgogoro wa SS na Lowasa and Rostam, Ameutatua
2) Zanzibar sio nchi. sasa kama hadithi, kautatua
3)tUCTA, nayo huo umeyayuka bila hata mabomu ya machozi
4)waraka wa wakatoliki na waislam. ameutatua na sasa kila kiongozi wa dini wamemkubali

anaebisha asubiri wiki chache zijazo

You a failure already MS:
Mgogoro wa UVCCM tayari umeangusha viongozi, mmoja wao aliingia kwa pendekezo lake JK. Katatua nini hapo? Resignations are a huge slap on JK's face.
 
Nafasi zote za kuchaguliwa UVCCM ni lazima uwe chini ya miaka 35 wakati unagombea. Makamanda wa vijana wa CCM sio wajumbe wa vikao hivi.

Ni miaka 35 au chini ya hapo utakapokuwa unamaliza term ya uongozi, ndio maana Nape alikataliwa kugombea japo alikuwa na miaka 30 na miezi kadhaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom